Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 103

14/07/2020

Ikiwa katika hii hatua Mungu mwenye mwili Anapitia ugumu au Anatekeleza huduma Yake, Anafanya hivyo ili kukamilisha maana ya kupata mwili, kwani huku ndiko Mungu kupata mwili kwa mara ya mwisho. Mungu Anaweza kuwa mwili mara mbili tu. Hakuwezi kuwepo mara ya tatu. Kuwa mwili kwa mara ya kwanza Alikuwa ni wa kiume, wa pili ni wa kike, na kwa hivyo sura ya mwili wa Mungu imekamilika katika akili za mwanadamu; aidha, huku kuwa mwili mara mbili tayari kumemaliza kazi ya Mungu katika mwili. Mara ya kwanza, Mungu mwenye mwili Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, ili kukamilisha maana ya kupata mwili. Mara hii vilevile Ana ubinadamu wa kawaida ila maana ya huku kupata mwili ni tofauti: ni kwa kina, na kazi Yake ni ya umuhimu mkubwa. Sababu ya Mungu kuwa mwili tena ni kukamilisha maana ya kupata mwili. Mungu Akiikamilisha kabisa hii hatua ya kazi Yake, maana nzima ya kupata mwili, yaani, kazi ya Mungu katika mwili, itakuwa imekamilika, na hakutakuwa na kazi nyingine ya kufanywa katika mwili. Yaani, tangu sasa Mungu Hatawahi tena kuja katika mwili kufanya kazi Yake. Ni kwa kuokoa na kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu pekee ndiko Mungu Hufanya kazi ya kupata mwili. Kwa maneno mengine, si jambo la kawaida kwa Mungu kuwa na mwili, ila tu ni kwa minajili ya kazi. Kwa kuja kufanya kazi Akiwa kwenye mwili, Anamwonyesha Shetani kuwa Mungu ni mwili, mtu wa kawaida—lakini Anaweza kuitawala dunia kwa ushindi, Anaweza kumshinda Shetani, kumkomboa mwanadamu na kumshinda mwanadamu! Lengo la kazi ya Shetani ni kuwapotosha wanadamu, ilhali lengo la Mungu ni kuwaokoa wanadamu. Shetani huwateka wanadamu katika shimo lisilo na mwisho, ilhali Mungu Huwaokoa kutoka humo shimoni. Shetani huwafanya wanadamu wote wamwabudu, ilhali Mungu Huwafanya wawe wafuasi wa utawala Wake, kwani Yeye ndiye Bwana wa viumbe wote. Kazi hii yote hutekelezwa kupitia Mungu kupata mwili mara mbili. Mwili Wake kimsingi ni muungano wa ubinadamu na uungu na huwa na ubinadamu wa kawaida. Kwa hivyo, bila Mungu kuwa mwili, Mungu Asingeweza kufikia matokeo katika ukombozi wa mwanadamu, na bila ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake, kazi Yake katika mwili bado Isingefaulu. Kiini cha kupata mwili kwa Mungu ni kwamba lazima awe na ubinadamu wa kawaida; kwani ingekuwa vinginevyo, ingekuwa kinyume na madhumuni asili ya Mungu ya kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp