Swahili Gospel Song 2020 | "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu"

Swahili Gospel Song 2020 | "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu"

1028 |16/04/2020

Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake.

Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika njia ambayo ni ya asili Kwake,

Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu

kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine.

Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe.

Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu,

na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini.

Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana.

Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu,

au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi;

ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi.

Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana

na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi,

na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi.

Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu,

utawala na kupata nuru kwa mwanadamu.

Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua.

Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine.

Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi kupitiwa mwanadamu.

na haijawahi kupitiwa mwanadamu.

Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali,

na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha,

ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya.

Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi