Swahili Christian Movie Based on True Story "Miaka 17? Hakika!" | The Power of Faith in God

13/09/2018

"Kijana! Je, unajua kwamba Chama cha Kikomunisti ni kikana Mungu na kiko kinyume na imani katika Mungu? Katika China, kuna Mungu yupi kwako kuamini? Mungu huyu wako yuko wapi?" "Usifikiri kwamba kwa sababu wewe ni mdogo, tutakuwa wenye huruma kwako! Ukiendelea kumwamini Mungu, utaishia kufa!" Wakiwa na fimbo za umeme mikononi, polisi wa Kikomunisti wa China wanamvamia kijana huyu ambaye amejawa na mavilio ya damu.

Jina la kijana huyu ni Gao Liang na alikuwa na umri wa miaka 17 mwaka huo. Alikuwa njiani akielekea nyumbani kutoka kueneza injili na ndugu mkubwa wakati ambapo alikamatwa na polisi wa Kikomunisti wa China. Polisi hawakumpa chochote cha kula wala kumruhusu alale kwa siku tatu na usiku tatu. Walimhoji, wakajaribu kupata kwa nguvu ushahidi kutoka kwake na kumtesa kwa ukatili. Pia walitumia fimbo za umeme ili kumshtua kwenye kidevu chake, mikono yake yote na sehemu zake nyeti Walijaribu kumlazimisha amsaliti Mungu na kuwapa habari kuhusu viongozi wa kanisa na rasilimali za kifedha za kanisa kupitia kumtisha. Hii ilihusisha kutishia kukamata wazazi wake na kuifanya shule yake imfukuze. Huku ikishindwa kufanikisha malengo yake, Serikali ya Kikomunisti ya Kichina ilimhukumu mwaka mmoja wa kuelimishwa tena kupitia kazi. Alipokuwa gerezani, Gao Liang hakuvumilia matakwa ya kazi pekee, ila pia alifedheheshwa na kuteswa. Katika gerezani, Gao Liang alipata uzoefu ambao unaweza kuitwa tu jahanamu duniani. Wakati wa kupogoloewa huku kuchungu, Gao Liang alimwomba Mungu na kumtegemea Mungu. Maneno ya Mwenyezi Mungu yalimpa nuru ili aelewe makusudi ya Mungu.Yalimpa imani na nguvu na kumwongoza ili kwamba apate kupitia mwaka huo mmoja ambao alikuwa gerezani. Mateso na kukamatwa na serikali ya Kikomunisti ya China yametiwa moyoni mwa Gao Liang. Anaona wazi na kwa undani alipitia kiini kiovu cha serikali ya Kikomunisti ya Kichina na upinzani wake kwa Mungu. Katika ulimwengu huu ambako nguvu za Shetani zinashikilia mamlaka, Mungu pekee ndiye anayempenda mwanadamu zaidi. Mungu pekee ndiye anaweza kumwokoa mwanadamu Imani yake na raghba yake ya kumfuata Mungu ilianza kuwa na azimio hata zaidi. Gao Liang anasema kuwa majaribio haya na mateso ni hazina ya thamani kwa ukuaji wa maisha yake na maendeleo yake. Ilikuwa zawadi maalum ambayo Mungu alimpa katika mwaka wake wa 17 ...

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Baadhi ya taarifa katika video hii zinatoka kwa:

Cork Hit 05 - Green Screen Green Screen Chroma Key Effects AAE( https://youtu.be/G_D5ZZQ2fJA ) by HD Green Screen/CC BY 3.0 ( https://creativecommons.org/licenses/by/3.0/ )

FireCracker 08 - Green Screen Green Screen Chroma Key Effects AAE( https://youtu.be/G_D5ZZQ2fJA )by HD Green Screen/CC BY 3.0 ( https://creativecommons.org/licenses/by/3.0/ )

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp