Watu Kote Ulimwenguni Wajifunza Kichina | Kwaya: Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima | Sauti za Sifa 2026

18/01/2026

1

Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho kila mtu anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu uzima unaweza kutoka tu kwa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayemiliki kiini cha uzima, na ni Mungu Mwenyewe pekee aliye na njia ya uzima. Na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na chemchemi isiyoisha ya maji ya uzima yaliyo hai. Tangu uumbaji wa dunia, Mungu amefanya kazi nyingi sana inayobeba pamoja nayo uhai wa uzima, Amefanya kazi nyingi ambayo inamletea mwanadamu uzima, na Amelipa gharama kubwa inayomwezesha mwanadamu apate uzima. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kufufuliwa.

2

Mungu kamwe hajawahi kukosa kuwepo moyoni mwa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa wanadamu wakati wote. Yeye ndiye msukumo wa maisha ya mwanadamu, mzizi wa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, na rasilimali tele ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu baada ya kuzaliwa. Yeye huwawezesha watu kuzaliwa upya, na kuwawezesha kuishi kwa ushupavu katika jukumu lao binafsi. Akitegemea uwezo Wake, na nguvu Yake ya uzima isiyozima, mwanadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, huku nguvu ya uzima wa Mungu imekuwa ikitoa tegemezo daima miongoni mwa wanadamu, na Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa.

3

Nguvu za uzima za Mungu zinaweza kushinda nguvu zozote; hata zaidi ya hayo, zinapita nguvu yoyote. Uzima Wake ni wa milele, nguvu Zake ni zisizo za kawaida, na nguvu Zake za uzima haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote aliyeumbwa au nguvu za adui. Nguvu za uzima wa Mungu zipo, nazo hutoa mng'ao mkuu unaonawiri bila kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa mno, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Vitu vyote vinaweza kupita, lakini uzima wa Mungu bado utakuwepo. Hii ni kwa sababu Mungu ndiye chanzo cha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, na mzizi unaotegemewa na kila kitu ili kiendelee kuishi.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp