Watu Kote Ulimwenguni Wajifunza Kichina | Ukariri na Kwaya: Hakuna Moyo Ulio Bora Kuliko wa Mungu | Sauti za Sifa 2026

18/01/2026

1

Nikiwa nimechagua kumpenda Mungu, ninamwacha achukue chochote Atakacho.

Licha ya kuhisi huzuni kidogo, silalamiki.

Akiwa na tabia potovu, mwanadamu anastahili hukumu na kuadibiwa.

Neno la Mungu ndilo ukweli; sipasiwi kuyaelewa vibaya mapenzi Yake.

Mara kwa mara hujitafakari na kugundua kuwa nina mchanganyiko mwingi sana;

nisipofuatilia ukweli, tabia yangu haiwezi kubadilika.

Ingawa nimevumilia maumivu mengi, ni heshima kufurahia upendo wa Mungu.

Kupitia kuteseka, ninajifunza utii. Hakuna moyo ulio bora kuliko wa Mungu.

2

Nikiwa na Mungu mchana na usiku, ninatambua jinsi Alivyo mzuri.

Ufichuzi na hukumu ya maneno Yake hunionyesha ukweli wa upotovu wangu.

Ninapokubali uchunguzi wa Mungu, ninafunuliwa kuwa mwasi sana.

Ninafungua moyo wangu kwa ushirika, na ninapata ufahamu wazi wa ukweli.

Ninatetemeka na kuhisi hofu kubwa kwa fikira ya kuikosea tabia Yake;

Ninajionya nisiasi tena na kuumiza moyo Wake.

Ingawa ninachagua kumpenda Mungu, nimetiwa uchafu na maoni yangu mwenyewe.

Lazima nitie bidii kupiga hatua na kufikia roho kama ya Petro.

Bila kujali jinsi Mungu anavyouona upendo wangu,

tamanio langu la pekee ni kumridhisha Yeye.

Ingawa nimevumilia maumivu mengi, ni heshima kufurahia upendo wa Mungu.

Kupitia kuteseka, ninajifunza utii. Hakuna moyo ulio bora kuliko wa Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp