Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 228

06/08/2020

Mwezi unaong’aa unapochomoza, usiku mtulivu unaangamizwa mara moja. Ingawa mwezi umepasuka, mwanadamu yumo katika hali ya uchangamfu, na anakaa kwa utulivu chini ya mwangaza wa mwezi, akifurahia eneo la kupendeza chini ya mwangaza. Mwanadamu hawezi elezea hisia zake; ni kama ana matamanio ya kuelekeza mawazo yake kwa wakati wa kale, ni kama anataka kuangalia mbele kwa mambo ya baadaye, ni kama anafurahia yanayojiri. Tabasamu linaonekana usoni mwake, na katika hali ya hewa ya kupendeza kunatokea harufu kavu; wakati upepo mwanana unapopuliza, mwanadamu anagundua harufu hiyo nzuri na anaonekana kuleweshwa nayo, akishindwa kujisimamisha. Huu ndio wakati haswa ambapo Mimi Mwenyewe Nimekuja miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu anahisi kwa hali ya juu harufu yenye uzuri tele, na kwa hivyo wanadamu wote wanaishi kati ya harufu hii. Niko na amani na mwanadamu, na mwanadamu anaishi kwa amani Nami, na hana uasi tena katika jinsi anavyonichukulia, Sipogoi tena upungufu wa mwanadamu, hakuna tena huzuni katika uso wa mwanadamu. Kifo hakitishii tena wanadamu wote. Leo, Naenda pamoja na mwanadamu katika enzi ya kuadibu, kuenda mbele pamoja na yeye upande kwa upande. Nafanya kazi Yangu, ambayo ni kusema, Naipiga fimbo Yangu chini miongoni mwa mwanadamu na inaanguka juu ya kile kilicho na uasi ndani ya mwanadamu. Katika macho ya mwanadamu, fimbo Yangu huonekana kuwa na nguvu spesheli: inaangukia wale wote ambao ni maadui Wangu na haiwasamehei kwa urahisi: miongoni mwa wale wote wanaonipinga, fimbo hiyo inafanya kazi yake ya kiasili; wale wote walioko mikononi Mwangu wanafanya wajibu wao kulingana na nia Yangu ya asili, na wala hawajawahi enda kinyume na matakwa Yangu au kubadilisha nia yao. Kutokana na hayo, maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika, mwanadamu atabadilika, jua litakua na mwangaza mdogo, mwezi utakuwa na giza zaidi, mwanadamu hatakuwa tena na siku za kuishi kwa amani, hakutakuwa tena na wakati wa amani katika nchi, mbingu haitawahi tena kuwa shwari, na kimya na haitawahi tena kuendelea. Vitu vyote vitafanywa vipya na kurudia hali vilivyoonekana mwanzoni. Nyumba zote duniani zitasambaratishwa, na mataifa yote duniani yatagawanywa; siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani. Siwapi watu fursa ya kutoa hisia zao, kwani Mimi sina hisia, na Nimekua katika kuchukia hisia za watu kwa kiasi. Ni kwa sababu ya hisia baina ya watu ndiposa Nimewekwa kando, na hivyo Nimekuwa “mwingine” machoni mwao; ni kwa sababu ya hisia kati ya binadamu ndiposa Nimesahaulika; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndipo anapochukua fursa ya kuchukua “dhamira” yake; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa kila mara amekuwa mwoga wa kuadibu Kwangu; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa ananiita mkosa haki na mdhulumu, na kusema kuwa Sisikizi hisia za mwanadamu Ninapofanya mambo Yangu. Je Nina mrithi duniani? Ni nani kamwe, kama Mimi, amewahi kufanya kazi usiku na mchana, bila kufikiria chakula au usingizi, kwa ajili ya mipangilio yangu yote ya usimamizi? Mwanadamu anawezaje kulinganishwa na Mungu? Anawezaje kuwa sambamba na Mungu? Inawezekanaje, Mungu, anayeumba, Awe sawa na mwanadamu, anayeumbwa? Ninawezaje kuishi na kufanya mambo pamoja na mwanadamu duniani? Nani anahofia moyo Wangu? Ni maombi ya mwanadamu? Wakati mmoja Nilikubali kujumuika na mwanadamu na kutembea pamoja na yeye—na ndio, hadi sasa mwanadamu anaishi chini ya ulinzi Wangu, lakini ni siku gani mwanadamu atajitenga kutoka kwa ulinzi Wangu? Hata ingawa mwanadamu hajawahi jali kuhusu moyo Wangu, nani anaweza kuendelea kuishi katika nchi isiyo na mwangaza? Ni kwa sababu tu ya baraka Zangu ndiposa mwanadamu ameishi mpaka leo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp