Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 162

23/07/2020

Kuzungumza kuhusu uovu wa Shetani hivi sasa kulimfanya kila mtu kuhisi kana kwamba watu huishi kwa huzuni sana na kwamba maisha ya mwanadamu yamejaa bahati mbaya. Lakini mnahisi vipi sasa kwani Nimezungumza kuhusu utakatifu wa Mungu na kazi ambayo anafanya kwa mwanadamu? (Furaha sana.) Tunaweza kuona sasa kwamba kila kitu Mungu anafanya, kila kitu ambacho anapanga kwa uangalifu kwa mwanadamu ni safi kabisa. Kila kitu anachofanya Mungu ni bila kasoro, kumaanisha ni bila dosari, hakihitaji yeyote kukosoa, kutoa mawaidha ama kufanya mabadiliko yoyote. Kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa kila mtu hakina shaka; Anaongoza kila mtu kwa mkono, Anakuchunga kwa kila muda na Hajawahi kuondoka upande wako. Watu wanapokua katika mazingira haya na kukua na usuli wa aina hii, tunaweza kusema kwamba watu kwa kweli wanakua katika kiganja cha mkono wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa bado mnahisi hisia za hasara? (La.) Je, kuna yeyote anayehisi kuvunjika moyo bado? (La.) Kwa hivyo kuna yeyote anayehisi kwamba Mungu amewaacha wanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa Mungu amefanya? (Anawahifadhi wanadamu.) Wazo na utunzaji mkuu nyuma ya kila anachofanya Mungu hayapingwi. Hata zaidi, wakati Mungu anapofanya kazi Yake, hajawahi kuweka sharti ama mahitaji yoyote kwa yeyote kati yenu kujua gharama anayokulipia, kwa hivyo uhisi shukrani kwake kwa kina. Je, Mungu amewahi kufanya chochote kama hiki kabla? (La.) Katika miaka yenu mirefu yote, kimsingi kila mtu amekutana na hali nyingi hatari na kupitia majaribu mengi. Hii ni kwa sababu Shetani yupo kando yako, macho yake yakikutazama kila wakati. Anapenda janga linapokupata, wakati maafa yanakupata, wakati hakuna chochote kinaenda sawa kwako, na anapendelea unaponaswa na wavu wa Shetani. Kuhusu Mungu, anakulinda kila wakati, kukuweka mbali na bahati moja mbaya baada ya nyingine na kutokana na janga moja baada ya jingine. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua maisha na hatima ya kila mtu. Lakini, je, Mungu ana dhana iliyovimbishwa ya cheo chake, kama wanavyosema watu wengine? Kukuambia “Mimi ni mkuu kabisa wa wote, ni Mimi ninayechukua watamu wenu, lazima nyote mniombe huruma na kutotii kutaadhibiwa na kifo.” Je, Mungu amewahi kutishia wanadamu kwa njia hii? (La.) Ashawahi kusema “Wanadamu ni wapotovu kwa hivyo haijalishi Ninavyowashughulikia, utendeaji wowote holela utatosha; Sihitaji kupanga mambo vizuri sana kwa sababu yao.” Je, Mungu anafikiria kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo Mungu ametenda kwa njia hii? (La.) Kinyume na haya, utendeaji wa Mungu wa kila mtu ni wenye ari na ambao umewajibika, umewajibika zaidi hata kuliko vile ulivyo kwa wewe mwenyewe. Sivyo hivi? Mungu haongei bure, wala hasimami juu akijifanya kuwa muhimu wala hadanganyi watu. Badala yake, Anafanya vitu ambavyo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya kwa uaminifu na kwa ukimya. Mambo haya yanaleta baraka, amani na furaha kwa mwanadamu, yanamleta mwanadamu kwa amani na kwa furaha mbele ya macho ya Mungu na ndani ya familia Yake na yanamletea mwanadamu akili sahihi, kufikiria sahihi, maoni sahihi na akili timamu wanapaswa kuwa nayo kuja mbele ya Mungu na kupokea wokovu wa Mungu. Kwa hivyo Mungu amewahi kuwa mdanganyifu kwa mwanadamu katika kazi Yake? (La.) Ashawahi kuonyesha maonyesho ya uongo ya ukarimu, Akimtuliza mwanadamu na mazungumzo ya kufurahisha, kisha kumpuuza mwanadamu? (La.) Je, Mungu ashawahi kusema kitu kimoja na kisha kufanya kingine? (La.) Je, Mungu ashawahi kupeana ahadi tupu na kujigamba, Akikuambia kwamba Anaweza kukufanyia hili ama kukusaidia kufanya lile, na kisha kutoweka? (La.) Hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, hakuna uongo. Mungu ni mwaminifu na kila kitu Anachofanya ni halisi. Yeye ndiye wa pekee ambaye watu wanaweza kutegemea na wa pekee ambaye watu wanaweza kuaminia maisha yao na yote wanayo Kwake. Kwa vile hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, tunaweza kusema kwamba Mungu ndiye wa kweli zaidi? (Ndiyo.) Bila shaka tunaweza, siyo? Ingawa, kuzungumza kuhusu maneno haya sasa, likitumika kwa Mungu ni dhaifu sana, cha ubinadamu sana, hakuna lolote tunaloweza kufanya kulihusu kwa vile hii ni mipaka ya lugha ya binadamu. Si sahihi sana hapa kumwita Mungu wa kweli, lakini tutatumia neno hili kwa sasa. Mungu ni mwaminifu. Kwa hivyo tunamaanisha nini kwa kuongea kuhusu vipengele hivi? Je, tunamaanisha tofauti kati ya Mungu na mwanadamu na tofauti kati ya Mungu na Shetani? Tunaweza kusema hivi. Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kuona chembe cha tabia potovu ya Shetani kwa Mungu. Je, Niko sahihi kusema hivi? Ninaweza kupata Amina kwa sababu ya hili? (Amina!) Hatuoni uovu wowote wa Shetani ukifichuliwa kwa Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya na kufichua ni muhimu sana na ya msaada sana kwa mwanadamu, yanafanywa kumkimu mwanadamu kabisa, yamejaa uhai na yanampa mwanadamu njia ya kufuata na mwelekeo wa kuchukua. Mungu hajapotoka, na zaidi ya hayo, kuangalia sasa kila kitu Mungu hufanya, tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu? (Ndiyo.) Kwa sababu Mungu hana upotovu wowote wa mwanadamu na hana chochote sawa na, au kinachofanana na tabia potovu ya mwanadamu ama kiini cha Shetani, kutoka mtazamo huu tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu hafichui upotovu wowote, na ufunuo wa kiini Chake katika kazi Yake yote ni thibitisho tunalohitaji kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu. Je, mnaona hili? Sasa, kujua asili takatifu ya Mungu, kwa sasa wacha tuangalie hivi vipengele viwili: 1) Hakuna tabia potovu ndani ya Mungu; 2) kiini cha kazi ya Mungu kwa mwanadamu kinamruhusu mwanadamu kuona kiini cha Mungu mwenyewe na kiini hiki ni kizuri kabisa. Kwa kuwa vitu ambavyo kila namna ya kazi ya Mungu inamletea mwanadamu ni vitu vizuri. Kwanza, Mungu anamhitaji mwanadamu kuwa mwaminifu—hili si zuri? Mungu anampa mwanadamu maarifa—hili si zuri? Mungu anamfanya mwanadamu aweze kutambua kati ya mema na maovu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuelewa maana na thamani ya maisha ya binadamu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuona ndani ya kiini cha watu, matukio na mambo kulingana na ukweli—hili si zuri? (Ndiyo ni zuri.) Na matokeo ya haya yote ni kwamba mwanadamu hadanganywi tena na Shetani, haendelei kudhuriwa na Shetani ama kudhibitiwa na yeye. Kwa maneno mengine, yanawaruhusu watu kujinusurisha kabisa kutoka upotovu wa Shetani, na hivyo kutembea polepole njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp