Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 103

30/06/2020

Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba

Shetani amekuwa akipotosha mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Ameleta kiwango kisichosemezeka cha maovu, amedanganya vizazi baada ya vizazi, na ametenda uhalifu wa kuchukiza ulimwenguni. Amedhulumu binadamu, amedanganya binadamu, ameshawishi binadamu ili ampinge Mungu, na ametenda vitendo vya maovu ambavyo vimetatiza na kuharibu mpango wa Mungu mara kwa mara. Ilhali, chini ya mamlaka ya Mungu, viumbe vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Yakilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata ingawaje Shetani anatembea miongoni mwa viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawaje mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na Shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawaje mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na mwenye umri ulioongezeka kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp