Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 81

22/06/2020

Bwana Yesu Ala Mkate na Kuonyesha Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake

Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?

Wanafunzi Wampa Bwana Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale

Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho. Naye akawaambia, Mbona mnasumbuka? na mbona mashaka yanaibuka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe: Niguseni, na kuona; kwa sababu roho haina mwili na mifupa, jinsi mnavyoniona mimi nikiwa nayo. Na baada ya yeye kunena hayo, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Na wakati walikuwa bado hawajaamini kwa furaha, na wakishangaa, akawaambia, Mnacho chakula chochote huku? Na wakampa kipande cha samaki wa kuokwa kwa asali. Na akakichukua, na kukila mbele yao.

Halafu tutaangalia dondoo zilizo hapo juu. Dondoo ya kwanza inamulika upya ulaji wa mkate na Bwana Yesu na unaeleza maandiko baada ya kufufuka Kwake na dondoo ya pili inaonyesha upya Bwana Yesu akila kipande cha samaki aliyekaushwa. Ni aina gani ya msaada ambao dondoo hii mara mbili inatupa kwa kuijua tabia ya Mungu? Unaweza kuwaza ni picha ya aina gani unayopata kutoka katika ufafanuzi huu wa Bwana Yesu akila mkate na kisha kipande cha samaki aliyekaushwa? Unaweza kufikiria, kama Bwana Yesu alikuwa Amesimama mbele yako wewe ukila mkate, unaweza kuhisi vipi? Au kama Angekuwa Akila pamoja nawe kwenye meza moja, huku Akila samaki kwa mkate na watu, ni hisia aina gani ambayo ungekuwa nayo wakati huo? Kama unahisi ungekuwa karibu sana na Bwana, kwamba yuko karibu sana na wewe, basi hisia yako i sahihi. Hivi ndivyo hasa tunda ambalo Bwana Yesu alitaka lizaliwe kutokana na kula Kwa mkate na samaki mbele ya umati wa watu baada ya kusulubishwa Kwake. Kama Bwana Yesu angekuwa ameongea tu na watu baada ya kufufuka Kwake, kama wasingeweza kuhisi mwili na mifupa Yake, lakini walihisi Alikuwa roho isiyoweza kufikika, wangehisi vipi? Hawangesikitishwa? Wakati watu wangesikitishwa, hawangehisi kwamba wameachwa? Hawangehisi ule umbali wa Bwana Yesu Kristo? Ni athari hasi ya aina gani ambayo umbali huu ungeweza kujenga katika uhusiano wa watu na Mungu? Watu wangehisi woga bila shaka, kwamba wasingethubutu kusonga karibu na Yeye, na wangekuwa na mwelekeo wa kumweka kwa mbali kiasi. Kuanzia hapo mpaka leo, wangekatiza uhusiano wao wa karibu na Bwana Yesu Kristo, na kurudi katika uhusiano kati ya wanadamu na Mungu aliye juu mbinguni, kama ilivyokuwa kabla ya Enzi ya Neema. Mwili wa kiroho ambao watu wasingeweza kuugusa au kuuhisi ungesababisha ukomeshaji wa ukaribu wao na Mungu, na ungefanya ule uhusiano wa karibu—ulioanzishwa wakati Bwana Yesu Kristo akiwa mwili bila ya umbali wowote kati Yake yeye na binadamu—ukose kuwepo. Hisia za watu kwa mwili wa kiroho ni za woga tu, kuepuka, na mtazamo usioeleweka. Hawathubutu kukaribia zaidi au kuwa na mazungumzo na Yeye, sikuambii hata kufuata, kuwa na imani, au kuwa na matumaini Kwake. Mungu hakupenda kuiona hisia ya aina hii ambayo wanadamu walikuwa nayo kwake Yeye. Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Kama familia yako binafsi, watoto wako wangekuona lakini wasingekutambua wewe, na hawakuthubutu kukukaribia lakini siku zote walikuepuka wewe, kama usingeweza kupata ufahamu wao kwa kila kitu ulichokuwa umewafanyia, ungehisi vipi? Halingekuwa jambo la uchungu? Je, hungevunjika moyo? Hivyo hasa ndivyo Mungu anavyohisi wakati watu wanamwepuka. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na pia anataka wanadamu kumwona Yeye kwa njia hiyo; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Sasa mnaweza kuelewa nia Yangu katika kudondoa dondoo hizi mbili kutoka katika maandiko pale ambapo Bwana Yesu anaula mkate na kuonyesha maandiko, na wanafunzi wanampa kipande cha samaki aliyechomwa ale baada ya kufufuka Kwake?

Inaweza kusemekana kwamba misururu ya mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Ilijaa huruma na huba ambayo Mungu anashikilia kwa binadamu, na akiwa amejaa shukrani na utunzaji wa makini Aliokuwa nao kwa minajili ya uhusiano wa karibu aliokuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi walijaa kumbukumbu za kitambo na tumaini Alilokuwa nalo kutokana na maisha ya kula na kuishi pamoja na wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili. Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumsikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika cheo kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao. Hivyo basi kama angekuwa amejitokeza kwa watu kupitia kwa mwili wa kiroho ambao wasingeweza kuuona ama kuugusa, hali hii kwa mara nyingine tena ingeweza kumweka binadamu mbali na Mungu, na ingewasababisha wanadamu kumwona Kristo kimakosa baada ya kufufuka Kwake kuonekana kuwa Amegeuka kuwa na majivuno, wa aina tofauti na wanadamu, na mtu ambaye asingeweza tena kushiriki meza na kula pamoja na binadamu kwa sababu wanadamu ni wenye dhambi, wananuka, na hawawezi kumkaribia Mungu hata kidogo. Ili kuondoa kutoelewana huku kwa wanadamu, Bwana Yesu alifanya mambo kadha wa kadha ambayo mara kwa mara Alifanya katika mwili, kama ilivyorekodiwa katika Biblia, “aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa.” Pia Aliwachambulia maandiko, kama Alivyokuwa amezoea kufanya. Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika, kwamba alikuwa bado Bwana Yesu. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuliwa, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele ya watu alikuwa bado Bwana Yesu. Mwenendo Wake na mazungumzo Yake na watu yalikuwa ya kawaida sana. Alikuwa angali bado na huruma na upendo, neema, na uvumilivu—Alikuwa bado Bwana Yesu aliyewapenda wengine kama Alivyojipenda Mwenyewe, ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu mara sabini mara saba. Kama kawaida, Alikula na watu, kuzungumza maandiko na wao, na hata muhimu zaidi, sawa tu na kama alivyofanya awali, Alifanywa kuwa mwili na damu na aliweza kuguswa na kuonekana. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi upendo huo, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi watulivu kwa njia tosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa imani ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba kwa jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na kuanza kutenda uponyaji na kupunga mapepo kwa jina la Bwana Yesu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp