Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 37

08/06/2020

Mungu Lazima Aangamize Sodoma (Vifungu teule)

Mwa 18:26 Na Yehova akasema, Nikipata katika Sodoma watu hamsini wenye haki ndani ya mji huo, basi nitaacha pahali pote kwa sababu yao.

Mwa 18:29 Na akanena tena na yeye, na kusema, Iwapo watu arobaini wakapatikana humo. Naye akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:30 Na akamwambia, Iwapo watapatikana huko watu thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:31 Na akasema, Iwapo watapatikana huko watu ishirini. Naye akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Mwa 18:32 Na akasema, Iwapo watapatikana huko watu kumi. Naye akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaowachukia na Kukataa

Katika simulizi za Biblia, kulikuwepo na watumishi kumi wa Mungu kule Sodoma? La, hakukuwepo! Kulikuwepo na jiji lililostahili kusamehewa na Mungu? Mtu mmoja tu kwenye jiji hilo—Loti—ndiye aliye wapokea wajumbe wa Mungu. Matokeo ya haya ni kwamba kulikuwa na mtumishi mmoja tu wa Mungu kwenye jiji, na hivyo basi Mungu hakuwa na chaguo ila kumwokoa Loti na kuliangamiza jiji la Sodoma. Mabadilishano haya kati ya Ibrahimu na Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi tu, lakini yanaonyesha kitu fulani kikuu: Kuna kanuni za vitendo vya Mungu, na kabla ya kufanya uamuzi Atachukua muda mrefu akiangalia na kutafakari; kabla ya wakati kuwa sawa, bila shaka Hatafanya au kukimbilia hitimisho zozote. Mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu yanatuonyesha kwamba uamuzi wa Mungu wa kuangamiza Sodoma haukuwa mbaya hata kidogo, kwani Mungu alijua tayari kwamba kwenye jiji hakukuwa na watu arubaini wenye haki, na wala thelathini wenye haki, wala ishirini. Hawakuwa hata kumi. Mtu mwenye haki pekee kwenye jiji alikuwa Loti. Yote yaliyofanyika ndani ya Sodoma na hali zake ziliangaliwa na Mungu, na zilizoeleka kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Hivyo, uamuzi Wake usingekosa kuwa sahihi. Kinyume na haya, tukilinganisha uweza wa Mungu, binadamu hajali katu, ni mjinga na asiyejua neno, asiyeona mbali katu. Haya ndiyo tunayoona katika mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu. Mungu amekuwa akiwasilisha mbele tabia Yake kuanzia mwanzo hadi leo. Hapa, vilevile, kuna pia tabia ya Mungu tunayofaa kuona. Nambari ni rahisi, na hazionyeshi chochote, lakini hapa kuna maonyesho muhimu sana ya tabia ya Mungu. Mungu asingeangamiza jiji kwa sababu ya watu hamsini wenye haki. Je, haya ni kutokana na rehema ya Mungu? Ni kwa sababu ya upendo na uvumilivu Wake? Je mmeuona upande huu wa tabia ya Mungu? Hata kama kungekuwa na wenye haki kumi pekee, Mungu asingeangamiza jiji hili kwa sababu ya watu hawa kumi wenye haki. Je, haya yanaonyesha uvumilivu na upendo wa Mungu au la? Kwa sababu ya rehema, uvumilivu, na kujali kwa Mungu kwa wale watu wenye haki, Asingeliangamiza jiji hili. Huu ndio uvumilivu wa Mungu. Na hatimaye, ni matokeo gani tunayoyaona? Wakati Ibrahimu aliposema, “Iwapo watapatikana huko watu kumi,” Mungu akasema, “Sitauharibu kwa sababu yao.” Baada ya hapo, Ibrahimu hakusema tena—kwani ndani ya Sodoma hakukuwa na wenye haki kumi aliowarejelea, na hakuwa na chochote ziada cha kusema, na kwa wakati huo alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa ameamua kuangamiza Sodoma. Katika haya, ni tabia gani ya Mungu unayoiona? Ni aina gani ya utatuzi ambayo Mungu alifanya? Yaani, kama jiji hili lisingekuwa na wenye haki kumi, Mungu asingeruhusu uwepo wake, na bila shaka Angeliangamiza. Je hii si hasira ya Mungu? Je, hasira hii inawakilisha tabia ya Mungu? Je, hii tabia ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu? Je, huu ni ufunuo wa kiini cha haki ya Mungu, ambacho binadamu hafai kukosea? Baada ya kuthibitisha kwamba hakukuwa na wenye haki kumi kule Sodoma, Mungu alikuwa na hakika ya kuliangamiza jiji, na angewaadhibu vikali watu walio ndani ya hilo jiji, kwani walimpinga Mungu, na kwa sababu walikuwa wachafu na waliopotoka.

Kwa nini tumechambua vifungu hivi kwa njia hii? Kwa sababu sentensi hizi chache rahisi zinatupa maonyesho kamili ya tabia ya Mungu ya wingi wa rehema na hasira kali. Wakati sawa na kuthamini sana wale wenye haki na kuwa na rehema juu yao, kuwavumilia, na kuwajali, ndani ya moyo wa Mungu kulikuwa na chukizo kuu kwa wale waliokuwa ndani ya Sodoma ambao walikuwa wamepotoshwa. Je, hii ilikuwa, au haikuwa rehema nyingi na hasira kali? Ni kwa mbinu zipi Mungu aliliangamiza jiji? Kwa moto. Na kwa nini Aliliangamiza kwa kutumia moto? Unapoona kitu kikiungua kwa moto, au wakati uko karibu kuchoma kitu, ni nini hisia zako juu ya kitu hicho? Kwa nini unataka kukichoma? Unahisi kwamba hukihitaji tena, kwamba hutaki tena kukiangalia? Unataka kukiacha? Matumizi ya moto na Mungu yanamaanisha uwachaji, na chuki, na kwamba hakutaka tena kuiona Sodoma. Hii ilikuwa ni hisia iliyomfanya Mungu kuteketeza Sodoma kwa moto. Matumizi ya moto yanawakilisha namna ambavyo Mungu alikuwa amekasirika. Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na uhaki wa Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inaonyesha binadamu upande wa Mungu usiyovumilia kosa lolote. Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu anakuwa mwingi katika huruma Yake kwa binadamu; wakati binadamu amejawa na upotoshaji, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Na anakuwa na ghadhabu nyingi hadi kiwango kipi? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka vyote hivi havipo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka. Kwa maneno mengine, haijalishi mtu husika ni yupi, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemgeukia Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mwonekano wote au kuhusiana na matamanio yake ya kibinafsi, atapenda kuabudu na kufuata na kutii Mungu katika mwili wake au katika kufikiria kwake pindi tu moyo wake utakapokuwa mbali na ule wa Mungu, hasira ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, pindi inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo. Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. Hapa, yaonekana kawaida kwa watu kwamba Mungu angeliangamiza jiji, kwani ndani ya macho ya Mungu, jiji lililojaa dhambi lisingeweza kuwepo na kuendelea kubakia pale, na lilikuwa jambo la kueleweka kwamba jiji hilo liangamizwe na Mungu. Lakini katika kile kilichofanyika kabla ya na kufuatia uangamizaji Wake wa Sodoma, tunaiona tabia nzima ya Mungu. Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa viumbe walio na upole, na wenye wema; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali, kiasi cha kwamba Hawachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: wingi wa huruma na ghadhabu nyingi. Wengi wenu hapa mmepitia huruma ya Mungu, lakini wachache sana wameweza kutambua hasira ya Mungu. Huruma na upole wa upendo wa Mungu unaweza kuonekana kwa kila mmoja; yaani, Mungu Amekuwa mwingi wa huruma kwa kila mmoja. Ilhali ni nadra sana—au, inaweza kusemekana, kamwe—Mungu amekuwa na ghadhabu nyingi kwa watu binafsi au sehemu yoyote ya watu miongoni mwenu hapa leo. Tulia! Hivi karibuni au baadaye, hasira ya Mungu itaonekana na kupitiwa na kila mmoja, lakini kwa sasa bado muda haujawadia. Na kwa nini hivi? Kwa sababu wakati Mungu anakuwa na ghadhabu kila mara kwa mtu, yaani, wakati Anapoiachilia hasira Yake kuu kwao, inamaanisha kwamba Amekuwa akichukia na Akikataa kwa muda mrefu mtu huyu, kwamba Anadharau uwepo wake na kwamba Hawezi kuvumilia uwepo wake; pindi tu ghadhabu Yake inapomjia, watatoweka. Leo, kazi ya Mungu bado haijafikia hapo. Hakuna yeyote kati yenu ambaye ataweza kuivumilia pindi tu Mungu anapoghadhabika kupindukia. Mnaona, kisha, kwamba kwa wakati huu Mungu anayo huruma nyingi tu kwa watu wote, na ungali hujaona ghadhabu yake nyingi. Kama wapo wale wanaobakia wakiwa hawajashawishika, mnaweza kuuliza kuwa hasira ya Mungu ije kwenu, ili mweze kuipitia na kujua kama ghadhabu ya Mungu na tabia Yake isiyokosewa kwa binadamu ipo kwa kweli au la. Mtathubutu kufanya hivyo?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp