Best  Swahili Worship Song "Nitampenda Mungu Milele" | Kusogea Mbele na Upendo wa Mungu (Swahili Dubbed)

Best Swahili Worship Song "Nitampenda Mungu Milele" | Kusogea Mbele na Upendo wa Mungu (Swahili Dubbed)

4458 |07/06/2017

I

Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kukurudia Wewe.

Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.

Majaribu mengi na uchungu, dhiki nyingi sana.

Mara nyingi nilitoa machozi na kuhuzunika sana,

mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.

Lakini hujaniacha kamwe.

Uliniongoza kupitia taabu nyingi, Ukanilinda katika hatari nyingi.

Sasa najua kuwa Umenipenda.

II

Ee Mungu! Unaniongoza katika maisha mapya.

Nikifurahia maneno Yako, nimeelewa mapenzi Yako.

Maneno Yako yanihukumu na kuniadhibu, na kutakasa upotovu wangu.

Kupitia majaribu nimejifunza kukutii Wewe.

Ninapokua katika neno Lako, nimekuja kukujua Wewe.

Niko tayari kufanya wajibu wangu kwa ushahidi Wako na utukufu.

Nitakupenda Wewe wakati wote.

Nikibarikiwa au kulaaniwa, nitafurahia kuwa chini ya rehema Yako.

Nitakupa upendo wa kweli, na sitakufanya Ungoje.

Nitakupa upendo safi, tafadhali furahia upendo wangu.

Nitakupa upendo wangu wote, na kuacha Upate upendo wangu.

Nitakupenda wakati wote; kukuridhisha ni tamanio langu.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi