Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 465

25/08/2020

Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwengine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, Ninakuambia kama awali: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp