Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 396

02/09/2020

Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo kwayo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na unaweza kuwa mzingatifu wa upendo wa Mungu. Ni yale ambayo kwayo unaishi katika maneno ya Mungu, na hakuna kingine kinachoushughulisha moyo wako, na unaweza kuyafahamu mapenzi ya Mungu leo, na unaongozwa na nuru ya Roho Mtakatifu leo ili kutimiza wajibu wako. Maisha kama hayo kati ya mwanadamu na Mungu ndiyo maisha ya kiroho. Kama huwezi kuifuata nuru ya leo, basi umbali umefunguka katika uhusiano wako na Mungu—huenda hata ukawa umevunjwa—na huna maisha ya kiroho ya kawaida. Uhusiano wa kawaida na Mungu hujengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya Mungu leo. Je, una maisha ya kiroho ya kawaida? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Wewe ni mtu anayeifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama unaweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo, na unaweza kufahamu mapenzi ya Mungu ndani ya maneno Yake, na kuingia katika maneno haya, basi wewe ni mtu ambaye hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi wewe bila shaka ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na kutokana na hayo, watu hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na kila mara wao huwa baridi. Leo, wewe hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Wewe uko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka kwa hali baridi? Wale wote ambao huamini katika maneno ya Mungu, ambao huchukulia kazi ya Mungu kama msingi, na hufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo—wao wote wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama wewe huamini kwamba maneno ya Mungu ni kweli na sahihi kwa dhahiri, na kama wewe huamini maneno ya Mungu bila kujali kile Yeye husema, basi wewe ni mtu ambaye hufuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii utatimiza mapenzi ya Mungu.

Ili kuingia katika mkondo wa Roho Mtakatifu lazima uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu, na lazima kwanza ujiondoshe kwa hali yako baridi. Watu wengine kila mara hufuata walio wengi, na mioyo yao imetangatanga mbali sana na Mungu; watu hao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na viwango ambavyo wao hufuatilia ni vya chini sana. Ukimbizaji wa kumpenda Mungu tu na kupatwa na Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Kuna watu ambao hutumia tu dhamiri yao kulipa mapenzi ya Mungu, lakini hili haliwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu; kadri viwango unavyofuatilia vilivyo juu zaidi, ndivyo vitakavyokuwa vinawiana na mapenzi ya Mungu. Kama mtu aliye wa kawaida, na ambaye hufuatilia upendo wa Mungu, kuingia katika ufalme kuwa mmoja wa watu wa Mungu ni siku za usoni zenu za kweli, na maisha ambayo ni yenye thamani na maana sana; hakuna aliyebarikiwa kuliko ninyi. Mbona Nasema hili? Kwa sababu wale wasiomwamini Mungu huishi kwa ajili ya mwili, na wao huishi kwa ajili ya Shetani, lakini leo ninyi huishi kwa ajili ya Mungu, na huishi kufanya mapenzi ya Mungu. Ndiyo maana Nasema maisha yenu ni yenye maana sana. Ni kundi hili tu la watu, ambao wameteuliwa na Mungu, wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana sana: Hakuna mwingine duniani anaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya thamani na maana hivyo. Kwa sababu mmeteuliwa na Mungu, na mmekuzwa na Mungu, na, aidha, kwa sababu ya upendo wa Mungu kwenu, mmefahamu uzima wa kweli, na mnajua namna ya kuishi maisha yenye thamani sana. Hili si kwa sababu ukimbizaji wenu ni mzuri, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu; ni Mungu aliyefungua macho ya roho zenu, na ni Roho wa Mungu aliyegusa mioyo yenu, kuwapa ninyi bahati nzuri ya kuja mbele Yake. Kama Roho wa Mungu hangekuwa amekupa nuru, basi hungekuwa na uwezo wa kuona kilicho cha kupendeza kuhusu Mungu, wala haingewezekana kwa wewe kumpenda Mungu. Ni kwa sababu kabisa Roho wa Mungu amegusa mioyo ya watu ndiyo mioyo yao imeelekea kwa Mungu. Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp