Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"

Video za Nyimbo na Ngoma   13313  

Utambulisho

I

Mwenyezi Mungu mwenye mwili

Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,

kama tu vile jua la haki likichomoza;

mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.

Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma

Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,

Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.

Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.

Mungu uliyekuwa na kiu naye, Mungu niliyemngoja,

leo anaonekana kwetu kwa utendaji.

Tuliutafuta ukweli, tulitamani sana haki;

ukweli na haki vimekuja miongoni mwa wanadamu.

Unampenda Mungu, nampenda Mungu;

mwanadamu amejaa sana matumaini mapya.

Watu wanatii, mataifa yanamwabudu

Mungu mwenye mwili wa utendaji.


II

Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli na kuleta hukumu,

Akifichua tabia ya Mungu yenye haki.

Kwa hukumu, kuadibu na majaribu ya maneno,

Anashinda na kukamilisha kikundi cha washindi.

Maneno ya Mungu, ya gadhabu na uadhama,

yanahukumu na kuutakasa uovu wa mwanadamu,

yakiharibu kabisa enzi ya giza.

Ukweli na haki vinatawala duniani.

Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;

Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.

Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,

Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.

Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;

Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.

Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,

Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.

Ufalme wa Kristo unapatikana miongoni mwa wanadamu.


Kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu