Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

"Ivunje Laana" (6) - Je, Utiifu kwa Wachungaji na Wazee wa Kanisa ni Sawa na Kumtii Mungu?

Dondoo za Filamu   538  

Utambulisho

Waumini wengine huamini kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini wamechaguliwa na kuteuliwa na Bwana, na kwamba wote ni watu wanaomtumikia Bwana. Hivyo wanaamini kwamba kuwatii tu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumtii Bwana, na kwamba kuwaasi au kuwahukumu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumpinga Bwana. Wao huamini hata kuwa, katika makanisa, wachungaji na wazee wa kanisa peke ndio huelewa Biblia na huweza kuelezea Biblia, na almradi kile kinachohubiriwa au kufanywa na wachungaji na wazee wa kanisa kinakubaliana na Biblia na kina msingi katika Biblia, basi watu wanapaswa kuwatii na kuwafuata. Hivyo aina hii ya utiifu kwa wachungaji na wazee wa kanisa inakubaliana na ukweli? Je, ufahamu wa maarifa ya Biblia unawakilisha ufahamu wa ukweli na maarifa ya Mungu? Tunapaswa kuchukua mtazamo upi hasa kwa wachungaji na wazee wa kanisa ambao unafuata mapenzi ya Mungu?