Wimbo wa Injili | Heri Wanaompenda Mungu (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

19/01/2026

1

Ni wale tu wanaompenda Mungu ndio wanaoweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ni wao tu ndio mashahidi wa Mungu, na ni wao tu ndio waliobarikiwa na Mungu, na ni wao tu ndio wanaoweza kupokea ahadi za Mungu. Wale wanaompenda Mungu ndio wandani wa Mungu; ndio watu ambao wanapendwa na Mungu, na wanaweza kufurahia baraka pamoja na Mungu. Ni watu wa aina hii tu ndio watakaoishi milele, na ni wao tu watakaoishi milele katika utunzaji na ulinzi wa Mungu.

2

Mungu anastahili kupendwa na watu, na Anastahili upendo wa watu wote, lakini sio watu wote wanaoweza kumpenda Mungu, na si watu wote wanaoweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kushikilia mamlaka pamoja na Mungu. Kwa sababu wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutoa juhudi zao zote kwa kazi ya Mungu, wale wanaompenda Mungu kwa kweli wanaweza kutembea mahali popote chini ya mbingu bila ya mtu yeyote kuwa na ujasiri wa kuwapinga, na wanaweza kushika mamlaka duniani na kuwatawala watu wote wa Mungu.

3

Watu hawa wamekusanyika pamoja kutoka kote duniani. Ni watu kutoka kote duniani wanaozungumza lugha tofauti na ni wenye rangi tofauti za ngozi, lakini maana ya kuwepo kwao ni sawa, wote wana moyo unaompenda Mungu, wote wana ushuhuda sawa, na wana maazio na matamanio sawa. Wale wanaompenda Mungu wanaweza kutembea ulimwenguni kote wakiwa huru, na wale walio na ushuhuda kwa Mungu wanaweza kusafiri katika ulimwengu mzima. Watu hawa wamependwa na Mungu, wamebarikiwa na Mungu, na wataishi milele ndani ya mwangaza Wake.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp