Christian Dance | Watu Wote wa Mungu Wamsifu Mwenyezi Mungu | Sauti za Sifa 2026

24/01/2026

1

Kuna Mwana wa Adamu anayeonyesha ukweli kila siku, na huyu ni Mwenyezi Mungu.

Tumeisikia sauti ya Mungu na hatimaye tumemkaribisha Bwana—furaha kuu iliyoje!

Kuuona uso wa Mungu wa kweli kumekuwa jambo ambalo hatukulitamani kamwe!

Ee, tumebarikiwa kama nini!

Sifa, sifa, sifa kuu! Tazama nani anayecheza kwa furaha sana!

Mioyo yetu imejaa furaha na iko huru kabisa!

2

Tumenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

na tunahudhuria karamu ya ufalme wa mbinguni.

Tunakula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, na kuelewa kweli nyingi sana—

mioyo yetu imeangazwa kweli!

Maneno ya Mungu yananiwezesha kujijua na kuona kina cha upotovu wangu,

naanguka mbele ya Mungu kwa majuto makubwa mno.

Sifa, sifa, sifa kuu! Tazama nani anayecheza kwa furaha sana!

Mioyo yetu imejaa furaha na iko huru kabisa!

3

Kumfuata Kristo na kutimiza wajibu wangu

kunafanya maisha yangu yawe ya thamani na ya maana.

Katika kufanya wajibu wangu, ninapitia kazi ya Mungu

na kupata nuru ya Roho Mtakatifu; maisha yangu yanakua kwa kasi!

Baada ya kutakaswa kupitia hukumu, ninaweza kumtii Mungu kweli—

hii ni baraka ya Mungu!

Sifa, sifa, sifa kuu! Tazama nani anayecheza kwa furaha sana!

Mioyo yetu imejaa furaha na iko huru kabisa!

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp