Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Hukumu ya Mungu kwa Mataifa na Watu Wasiohesabika” | Sauti za Sifa 2026
19/01/2026
1
Ufalme Wangu umetimia kabisa, na umeshuka hadharani ulimwenguni; hili linaashiria kwamba hukumu Yangu imeshuka kikamilifu. Maafa ya kila aina yatashuka, moja baada ya lingine; nchi zote na maeneo yote yatapitia maafa: Tauni, njaa, mafuriko, ukame na matetemeko ya ardhi viko kila mahali. Maafa haya hayatendeki tu katika sehemu moja au mbili, wala hayataisha baada ya siku moja au mbili; badala yake, yataenea katika eneo kubwa zaidi na zaidi, na yatakuwa makali zaidi na zaidi. Katika wakati huu kila namna ya tauni za wadudu zitaibuka moja baada ya nyingine, na tukio la watu kuwala watu litatokea kila mahali. Hii ni hukumu Yangu juu ya nchi na watu wasiohesabika.
2
Jina Langu lazima lienee katika kila upande na kila mahali, ili kwamba kila mtu alijue jina Langu takatifu na anijue Mimi. Jina Langu litaenea kwa upana maafa yanaposhuka, na msipokuwa waangalifu na kuchunga, mtapoteza sehemu yenu ya haki. Je, hamwogopi? Jina Langu linaenea kwa dini zote, na kwa matabaka mbalimbali, mataifa yote, na madhehebu yote. Hii ni kazi Yangu inayofanywa kwa njia ya utaratibu, kwa muunganiko wa karibu; yote hutendeka kwa mipango Yangu ya busara. Ninatamani tu kwamba muweze kwa karibu kufuata hatua Zangu katika kila hatua kuenda mbele.
kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 65
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video