Wimbo wa Injili | Utukufu wa Mungu Wang’aa Kutoka Mashariki
25/05/2020
Ni wakatitu Mungu apitapo katika mbingu na nchi mpya tu ndipo
Anachukua sehemu nyingine ya utukufu Wake
na kuufichua kwanza katika nchi ya Kanaani,
Akisababisha nuru iiangazie dunia nzima,
iliyozama katika giza totoro la usiku,
ili kuruhusu dunia nzima ije katika nuru hiyo.
Acha watu wote duniani kote waje wapate nguvu kutoka kwa uwezo wa nuru,
wakiruhusu utukufu wa Mungu uongezeke
na kuonekana upya kwa kila taifa.
Acha binadamu wote watambue kwamba Mungu alikuja zamani katika ulimwengu wa wanadamu
na Alileta utukufu Wake kutoka Israeli hadi Mashariki zamani;
kwani utukufu Wake unang’aa kutoka Mashariki,
ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo.
Lakini Mungu aliondoka tokea Israeli
na kutoka huko ndipo Aliwasili Mashariki.
Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo
giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru,
na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba
Mungu alishaondoka Israeli zamani
na Ameanza kuinuka upya huko Mashariki.
Kwa kuwa Aliwahi kushuka huko Israeli
na baadaye Akaondoka kutoka huko,
Mungu hawezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine,
kwa kuwa kazi Yake inauongoza ulimwengu mzima
na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja toka Mashariki hadi Magharibi.
Kwa sababu hii Mungu Ameshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani.
Angependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani,
na kwa hiyo Anaendelea kutoa matamko katika nchi ya Kanaani
ili kuudhibiti ulimwengu mzima.
Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani,
na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi.
Angependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani,
na kwa hiyo Anaendelea kutoa matamko katika nchi ya Kanaani
ili kuudhibiti ulimwengu mzima.
Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani,
na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi,
na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video