Wimbo wa Injili | Mwenyezi Mungu Ameketi katika Kiti Tukufu Cha Enzi (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Mfalme wa ushindi anakaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Ametimiza ukombozi na kuwaongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye Anashikilia kila kitu mikononi Mwake. Kwa hekima Yake ya uungu na uweza Amejenga Sayuni na kuifanya imara. Kwa uadhama Wake Anaihukumu dunia yenye dhambi; Yeye amepitisha hukumu juu ya mataifa na watu wasiohesabika, ardhi na bahari na viumbe vyote hai ndani yake, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao.

2

Mungu hakika atawakasirikia na humo mtafunuliwa uadhama wa Mungu, ambaye hukumu Yake ni ya papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Moto wa ghadhabu Yake hakika utaziteketeza dhambi zao zilizo mbaya sana na watafikwa na janga wakati wowote; watakosa njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao, na watajiletea maangamizi. Wana washindi, wapendwa wa Mungu hakika watakaa katika Sayuni, wasiondoke kamwe kutoka hapo. Watu wasiohesabika wataisikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa uangalifu matendo Yake, na sauti za sifa zao kamwe hazitakoma.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 3

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp