Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 407
Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Yesu pamoja na Mimi tunatoka katika Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizonazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; miili Yetu ina maumbo tofauti, na hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndio maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukipokea leo hii si kama kile cha wakati uliopita; hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na ingawa hawakuzaliwa kutoka katika familia moja, achilia mbali katika kipindi kimoja, Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, hii haipingi kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni Mungu katika miili, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja au hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Kiyahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo maana Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi ya nje ya miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini umbo na kuzaliwa kwa miili Yao hakufanani. Haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu yao, maana, hata hivyo, ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi zao zinaongozwa na Roho Zao, ili kwamba waweze kufanya kazi tofauti katika nyakati tofauti, wakiwa na miili Yao isiyokuwa na undugu wa damu. Kwa namna ile ile, Roho wa Yehova sio baba wa Roho ya Yesu na Roho wa Yesu sio mwana wa Roho wa Yehova. Ni wa Roho moja. Kama tu Mungu katika mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu. Hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, huu si ukuu wa Mungu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya...
Je, Jina la Yesu—“Mungu pamoja nasi,”—linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu?...
Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na...
Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni...