Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 214

Mungu Anamfanyaje mwanadamu kuwa mkamilifu? Tabia ya Mungu ni gani? Na ni nini kilicho ndani ya tabia Yake? Haya yote lazima yaeleweke; hii ni kusambaza jina la Mungu, ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kumtukuza na kumsifu Mungu, na bila shaka mwanadamu atafikia mabadiliko katika tabia ya maisha yake kwa msingi wa kumjua Mungu. Zaidi mwanadamu anavyopitia kushughulikiwa na kusafishwa, ndivyo nguvu yake inavyoongezeka, na hatua za Mungu zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo mwanadamu anavyofanywa mkamilifu. Leo, katika uzoefu wa mwanadamu, kila hatua ya kazi ya Mungu inayagonga mawazo ya mwanadamu, na kila hatua haiwezi kuwazwa na akili ya mwanadamu, na kuzidi matarajio ya mwanadamu. Mungu Anakimu mahitaji yote ya mwanadamu, na kwa kila njia yote huwa yanakinzana na mawazo ya mwanadamu, na ukiwa mdhaifu, Mungu Ananena maneno Yake. Ni kwa njia hii tu ndio Anaweza kukupa uhai wako. Kwa kuzigonga fikira zako, unakuja kukubali kazi ya Mungu, na kwa njia hii pekee ndio unaweza kuondoa upotovu wako. Leo hii, kwa upande mmoja Mungu mwenye mwili Anafanya kazi katika uungu, na kwa upande mwingine Anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida. Usiikane kazi yoyote Anayoifanya Mungu, na unapaswa kutii lolote Analosema Mungu au kufanya Akiwa katika ubinadamu wa kawaida, na haijalishi jinsi Alivyo wa kawaida, unapaswa kutii na kuelewa. Ni wakati tu umepata uzoefu wa hakika ndipo utajua kwa uhakika kwamba Yeye ni Mungu, na kukoma kuwa na mawazo, na kumfuata mpaka mwisho. Kuna hekima katika kazi ya Mungu, na Anajua jinsi mwanadamu Anaweza kuwa na ushuhuda Kwake. Anajua pale ambapo udhaifu wa uhai wa mwanadamu upo, na maneno Anayozungumza yanaweza kukugonga pale penye udhaifu wako upo, lakini pia Anatumia maneno Yake makuu na yenye busara kukufanya uwe na ushuhuda Kwake. Hayo ndiyo matendo ya kimiujiza ya Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu haiwezi kufikiriwa na akili ya mwanadamu. Hukumu ya Mungu inafunua aina za upotovu ambazo mwanadamu, kwa kuwa ni mwili, amejawa nao, na vitu vipi ndivyo umuhimu wa mwanadamu, na humwacha mwanadamu bila mahali pa kujificha aibu yake.

Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp