Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 601
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Watu wengi wangependa kunipenda kwa kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawawezi kujidhibiti wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunihadaa, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu. Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Ni kama kwamba viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kama kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawahi kufichua siri yake; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha ujuzi huu wa udanganyifu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio yeye kunidanganya. Je, hiki sicho chanzo halisi cha mwanadamu kunidanganya? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 21
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi...
Ili kuwa kiumbe halisi aliyeumbwa, sharti ujue Muumba ni nani, uumbaji wa mwanadamu ni wa umuhimu gani, jinsi ya kutekeleza majukumu ya...
Ili kuishi maisha ya kawaida ya kiroho, lazima mtu aweze kupokea mwanga mpya kila siku na afuatilie ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu. Ni...
Maisha yako yakiendelea, lazima daima uwe na kiingilio kipya na ufahamu mpya na wa juu zaidi, unaokua kwa kina na kila hatua. Hiki ndicho...