Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 526

Mwanadamu anaishi katika mwili, ambayo ina maana anaishi katika kuzimu ya binadamu, na bila hukumu na adabu ya Mungu, mwanadamu ni mchafu kama Shetani. Mwanadamu atawezaje kuwa mtakatifu? Petro aliamini kwamba adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu! Petro aliomba, “Ee Mungu! Mradi tu Wewe unaniadibu na kunihukumu, nitajua kwamba Wewe hujaniacha. Hata kama Huwezi kunipa furaha au amani, na kufanya niishi katika mateso, na kunirudi mara nyingi, bora tu Hutaniacha moyo wangu utakuwa na amani. Leo hii, adabu Yako na hukumu umekuwa ulinzi wangu bora na baraka yangu kubwa. Neema unayonipa inanilinda. Neema unayoweka juu yangu leo ni kielelezo cha tabia Yako ya haki, na ni adabu na hukumu; zaidi ya hayo, ni majaribu, na, zaidi ya hapo, ni maisha ya mateso.” Petro alikuwa na uwezo wa kuweka kando raha ya mwili na kutafuta mapenzi zaidi na ulinzi zaidi, kwa sababu alikuwa amepata neema nyingi kutoka kwa adabu na hukumu ya Mungu. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kumahiri wote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba. Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso, na hata nimekuwa karibu na kifo, mateso hayo yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu. Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu, basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani. Mwili wa binadamu una faida gani? Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha, ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha, ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami. Kama ingekuwa vile, ni jinsi gani ningeendelea kuishi? Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya himaya ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Jinsi gani, Nieleze, ningeweza kuendelea kuishi? Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia. Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha? Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu, hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho. Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe; jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe? Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako, ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi, yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha, na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.”

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp