Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 480

Baadhi ya watu husema, “Paulo alifanya kazi kubwa kiasi cha ajabu, na alibeba mizigo mikubwa ya makanisa na aliwachangia mno. Nyaraka kumi na tatu ya Paulo zilizingatia miaka 2,000 ya Enzi ya Neema, na ni za pili tu baada ya Injili Nne. Nani anaweza kulinganishwa naye? Hakuna ambaye anaweza kufumbua maandiko ya Ufunuo wa Yohana, ilhali nyaraka za Paulo zinatoa maisha, na kazi ambayo alifanya ilikuwa na manufaa kwa makanisa. Ni nani mwingine angeweza kutimiza mambo kama haya? Na kipi ambacho Petro alikifanya?” Mwanadamu anapowapima wengine, ni kwa mujibu wa michango yao. Mungu anapompima mwanadamu, ni kwa mujibu wa asili yake. Miongoni mwa wale ambao hutafuta uzima, Paulo alikuwa mtu ambaye hakujua kiini chake mwenyewe. Hakuwa kwa njia yoyote mnyenyekevu ama mtiifu, wala kujua kiini chake, ambacho kilikinzana na Mungu. Na kwa hivyo, alikuwa mtu ambaye hakuwa amepitia matukio ya kina, na alikuwa mtu ambaye hakuweka ukweli katika vitendo. Petro alikuwa tofauti. Yeye alijua kutokamilika kwake, udhaifu, na tabia yake potovu kama kiumbe wa Mungu, na hivyo alikuwa na njia ya vitendo ambayo angebadilishia tabia yake; hakuwa mmoja wa wale ambao walikuwa tu na mafundisho ya kidini lakini hawakuwa na uhalisi. Wale ambao hubadilika ni watu wapya ambao wameokolewa, ni wale ambao wana sifa zinazostahili katika kufuatilia ukweli. Watu ambao hawabadiliki ni wa wale ambao hawafai kwa sasa kiasili; ni wale ambao hawajaokolewa, yaani, ni wale ambao wamechukiwa na kukataliwa na Mungu. Hawatawekwa kwenye ukumbusho na Mungu bila kujali jinsi kazi zao ni kubwa. Wakati unapolinganisha haya na harakati yako mwenyewe, kama wewe hatimaye ni mtu wa aina sawa na Petro au Paulo inapaswa kuwa dhahiri kibinafsi. Kama bado hakuna ukweli kwa yale unayotafuta, na kama hata leo bado wewe ni mwenye kiburi na jeuri kama Paulo, na bado wewe ni mwepesi wa kusema bila kusema ukweli na mwenye kujitukuza kama yeye, basi bila shaka wewe ni aliyeharibika tabia na ambaye hushindwa. Kama wewe hutafuta jinsi sawa na Petro, kama unatafuta vitendo na mabadiliko ya kweli, na usiwe mwenye kiburi au mkaidi, bali utafute kutekeleza majukumu yako, basi utakuwa kiumbe wa Mungu ambaye anaweza kufikia ushindi. Paulo hakujua kiini chake mwenyewe ama upotovu, vile vile hakujua kutotii kwake. Hakuwahi kutaja uasi wake kwa Kristo unaostahili dharau, wala yeye hakuwa mwenye kujuta kupindukia. Yeye tu alipeana maelezo mafupi, na, ndani katika moyo wake, hakujiwasilisha kwa Mungu kikamilifu. Ingawa alianguka barabarani akielekea Dameski, yeye hakuangalia nafsi yake kwa kina. Aliridhika tu kwa kuendelea kufanya kazi, na hakuzingatia kujijua mwenyewe na kubadilisha tabia yake ya zamani kuwa jambo la muhimu zaidi ya masuala yote. Yeye aliridhika tu kwa kusema ukweli, na kukimu wengine kama dawa ya dhamiri yake mwenyewe, na kwa kutowatesa tena wanafunzi wa Yesu kujifariji na kujisamehe kwa dhambi zake za zamani. Lengo ambalo yeye alifuatilia tu lilikuwa taji ya wakati ujao na kazi ya muda pekee, lengo ambalo alifuatilia lilikuwa neema tele. Yeye hakutafuta ukweli wa kutosha, wala hakutafuta kuendelea ndani katika kiini cha ukweli ambao hakuwa hapo awali ameufahamu. Na kwa hivyo elimu yake ya nafsi yake inaweza semwa kuwa ya uwongo, na hakukubali kuadibu au hukumu. Kwamba aliweza kufanya kazi haina maana alikuwa na elimu ya asili yake au kiini; lengo lake lilikuwa la vitendo vya nje pekee. Lile ambalo daima alijitahidi kwalo, zaidi ya hayo, halikuwa mabadiliko, laikini elimu. Kazi yake kwa ujumla ilikuwa matokeo ya kuonekana kwa Yesu njiani kuelekea Dameski. Hakikuwa kitu ambacho alikuwa ameamua kukifanya hapo awali, wala haikuwa kazi ambayo ilikuwa imetokea baada ya yeye kukubali upogoaji wa tabia yake ya zamani. Bila kujali jinsi ambavyo alifanya kazi, tabia yake ya zamani haikubadilika, na hivyo kazi yake haikulipia dhambi yake ya zamani lakini ilikuwa tu na wajibu fulani kwenye makanisa ya wakati huo. Kwa mtu kama huyu, ambaye tabia yake ya zamani haikubadilika—hivyo ni kusema, ambaye hakupata wokovu, na hata zaidi alikuwa bila ukweli—alikuwa hawezi kabisa kukuwa mmoja wa wale waliokubaliwa na Bwana Yesu. Hakuwa mtu ambaye alikuwa amejazwa na upendo na heshima kwa Yesu Kristo, wala hakuwa mtu ambaye alikuwa na ustadi katika kutafuta ukweli, na wala hakuwa mtu ambaye alitafuta fumbo la kupata mwili kwa Yesu Kristo. Alikuwa tu mtu ambaye alikuwa na ujuzi katika utata, na ambaye hangeweza kusalimu amri kwa yeyote ambaye alikuwa mkuu kwake au aliyekuwa na ukweli. Aliwaonea kijicho watu ama ukweli ambao ulikuwa tofauti naye, ama wenye uadui naye, na kupendelea watu wenye vipawa ambao walionyesha picha nzuri na kumiliki maarifa makubwa. Hakupenda kuingiliana na watu maskini ambao walitafuta njia ya ukweli na waliojali kuhusu ukweli pekee, na badala yake alijihusisha na viongozi mashuhuri kutoka mashirika ya kidini ambao walizungumza kuhusu mafundisho ya dini pekee, na walikuwa na elimu tele. Hakuwa na upendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, na hakujali kuhusu harakati za kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Badala yake, yeye alipendelea kanuni hizo na mafundisho ya dini ambayo yalikuwa juu kuliko ukweli wa ujumla. Katika kiini chake cha kiasilia na uzima wa kile alichotafuta, hastahili kuitwa Mkristo ambaye alifuatilia ukweli, wala mtumishi mwaminifu katika nyumba ya Mungu, kwa kuwa unafiki wake ulikuwa mwingi sana, na kutotii kwake kulikuwa kukubwa sana. Ingawa anajulikana kama mtumishi wa Bwana Yesu, hakustahili kamwe kuingia kwenye lango la ufalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake tangu mwanzo hadi mwisho hayawezi kuitwa yenye haki. Anaweza tu kuonekana kama mtu ambaye alikuwa mnafiki, na aliyefanya udhalimu, ilhali ambaye alimfanyia Yesu kazi. Ingawa hawezi kuitwa mwovu, yeye anaweza ipasavyo kuitwa mtu ambaye alifanya udhalimu. Alifanya kazi nyingi, ilhali ni lazima asihukumiwe juu ya wingi wa kazi aliyofanya, lakini tu kwa ubora na umuhimu wa kazi hiyo. Ni kwa njia hii tu ndiyo inawezekana kufikia kwenye kiini cha suala hili. Yeye siku zote aliamini: Mimi nina uwezo wa kufanya kazi, mimi ni bora kuliko watu wengi; mimi ni mwenye kujali kuhusu mzigo wa Bwana kuliko mtu yeyote, na hakuna anayetubu sana kama ninavyotubu, kwa kuwa mwanga mkuu uling’aa kwangu, na nimeuona mwanga mkuu, na hivyo toba yangu ni kuu kuliko ya yeyote mwingine. Wakati huo, hivi ndivyo alivyofikiria moyoni mwake. Mwishoni mwa kazi yake, Paulo alisema: “Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu.” Mapambano yake, kazi, na safari zilikuwa kwa ajili ya taji la haki, na yeye hakusonga mbele; ingawa yeye hakuwa wa juu juu tu katika kazi yake, inaweza kusemwa kuwa kazi yake ilikuwa kwa ajili tu ya kusahihisha makosa yake, na kusahihisha shutuma za dhamiri yake. Yeye tu alitumaini kukamilisha kazi yake, kumaliza safari yake, na kupigana vita vyake haraka iwezekanavyo, ili kwamba aweze kupata tuzo lake la haki alilotamani kwa haraka. Alilotamani halikuwa kukutana na Bwana Yesu na uzoefu wake na elimu ya kweli, lakini kukamilisha kazi yake haraka iwezekanavyo, ili kwamba aweze kupokea tuzo ambayo kazi yake ilikuwa imemwezesha kupata wakati alipokutana na Bwana Yesu. Alitumia kazi yake kujifariji, na kufanya makubaliano kwa ajili ya kupewa taji siku zijazo. Alichotafuta sio ukweli ama Mungu, lakini taji tu. Harakati kama hii inawezekanaje kuwa ya kiwangogezi? Motisha yake, kazi yake, gharama aliyolipa, na juhudi zake zote—ndoto zake za ajabu zilienea kote, na alifanya kazi kabisa kulingana na mapenzi yake. Katika ukamilifu wa kazi yake, hapakuwa na hiari kidogo ya gharama aliyolipa; alikuwa anashiriki kwenye mapatano tu. Juhudi zake hazikufanywa kwa hiari ili kutimiza wajibu wake, bali zilifanywa kwa hiari ili kutekeleza lengo la mapatano. Je, kuna thamani yoyote kwa jitihada kama hizo? Nani ambaye anaweza kusifu juhudi zake chafu? Nani ambaye ana moyo wa kujua juhudi kama hizi? Kazi yake ilijawa na ndoto za mbeleni, zilijawa na mipango ya ajabu, na hazikuwa na njia ya kubadilishia tabia ya kibinadamu. Ukarimu wake mwingi ulikuwa wa unafiki; kazi yake haikuleta maisha, lakini ilikuwa unyenyekevu bandia; lilikuwa tendo la maafikiano. Jinsi gani kazi kama hii kumwongoza mwanadamu kwenye njia ya kupata tena wajibu wake wa awali?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp