Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 449

Hao watu wapumbavu na mafidhuli hawajafanya kila wawezalo wala kutimiza wajibu wao tu, bali wameinyosha mikono yao wakitaka neema, kana kwamba wanastahili wanachoitisha. Na iwapo watashindwa kupata wanachokiomba, wanakuwa wakosa imani zaidi. Watu kama hawa wataitwaje wastaarabu? Ninyi ni sampuli mbaya isiyokuwa na urazini, isiyoweza kabisa kutimiza wajibu mnaotakiwa kutimiza wakati wa kazi ya usimamizi. Thamani yenu imeshuka pakubwa. Kwa kutonilipa kwa kuwaonea imani tayari ni tendo la uasi mkuu litoshalo kuwahukumu na kuthibitisha uoga, uovu, uzembe na uduni wenu. Mnawezaje kuendelea kustahili kunyoosha mikono yenu? Mmeshindwa kuwa hata msaada kidogo kwa kazi Yangu, mmeshindwa kuahidi imani yenu, na mmeshindwa kunitolea ushuhuda. Tayari haya ni makosa na kushindwa kwenu, na bado mnanivamia, mnanisemea uongo na kulalama kuwa Mimi si mwenye haki. Je, huu ndio uaminifu wenu? Haya ndiyo mapenzi yenu? Ni kazi gani nyingine mnayoweza kufanya zaidi ya hii? Mmechangia vipi katika kazi yote ambayo imeishafanywa? Mmegharamia kiasi gani? Ni huruma kubwa kwamba bado Sijawawekea lawama, na bado mnanipa visingizio na kulalama faraghani kunihusu. Kweli mna hata chembe ndogo ya ubinadamu? Japo wajibu wa mwanadamu umetiwa doa na fikira za mwanadamu na mitazamo yake, ni sharti ufanye wajibu wako na kuwa mwaminifu kwa imani yako. Unajisi katika kazi ya mwanadamu ni suala la hulka yake, ilhali, ikiwa mwanadamu hafanyi wajibu wake, unajisi huu unaonyesha uasi wake. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndiko huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Wacha niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hupitia mijadala tu katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika vitendo vya ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp