Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 441

Unapojitayarisha kwa ajili ya maisha, lazima ulenge kula na kunywa maneno ya Mungu, lazima uweze kuzungumzia maarifa ya Mungu, maoni yako ya maisha ya binadamu, na hasa, maarifa yako ya kazi iliyofanywa na Mungu wakati wa siku za mwisho. Kwa kuwa unafuatilia uzima, ni lazima ujitayarishe na vitu hivi. Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, lazima utathmini uhalisi wa hali yako mwenyewe kulingana na vitu hivi. Yaani, unapogundua dosari zako wakati wa uzoefu wako wa kweli, lazima uweze kupata njia ya kutenda, uweze kupuuza nia na fikira zako zisizo sahihi. Ukijitahidi daima kupata vitu hivi na utake kuvitimiza kwa dhati, basi utakuwa na njia ya kufuata, hutahisi mwenye utupu, na hivyo utaweza kudumisha hali ya kawaida. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayebeba mzigo katika maisha yako mwenyewe, aliye na imani. Mbona watu wengine hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo baada ya kuyasoma? Je, si kwa sababu hawawezi kuelewa vitu muhimu kabisa? Je, si kwa sababu hawayachukulii maisha kwa uzito? Sasabu ya wao kutoelewa vitu muhimu na kukosa njia ya kutenda ni kuwa wanaposoma maneno ya Mungu, hawawezi kuyahusisha na hali zao wenyewe, wala hawawezi kuwa na ujuzi wa hali zao wenyewe. Watu wengine husema: “Mimi huyasoma maneno ya Mungu na kuyahusisha na hali yangu mwenyewe, na najua kwamba mimi ni mpotovu na mwenye ubora duni wa tabia, lakini siwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu.” Umeona tu mambo ya nje kabisa; kuna vitu vingi halisi ambavyo huvijui: jinsi ya kuweka kando raha za mwili, jinsi ya kuweka kando kujidai, jinsi ya kujibadili, jinsi ya kuviingia vitu hivi, jinsi ya kuboresha ubora wako wa tabia, na kuanzia kutoka kipengele kipi. Unaelewa tu mambo machache ya nje, na yote unayoyajua ni kwamba kweli umepotoka sana. Unapokutana na ndugu zako, unazungumzia jinsi ulivyopotoka, na inaonekana kwamba unajijua na unabeba mzigo mkubwa kwa ajili ya maisha yako. Kwa kweli, tabia yako potovu haijabadilika, jambo linalothibitisha kwamba hujapata njia ya kutenda. Ikiwa unaongoza kanisa, lazima uweze kuelewa hali za kina ndugu na kuzionyesha. Je, itatosha kusema tu: “Ninyi watu ni wasiotii na wenye maendeleo kidogo mno!” La, lazima uzungumze hasa kuhusu jinsi kutotii kwao na wao kuwa wenye maendeleo kidogo mno kunavyodhihirishwa. Lazima uzungumzie hali zao za kutotii, mienendo yao ya kutotii, na tabia zao za kishetani, na lazima uyazungumzie mambo haya kwa namna ambayo wanashawishika kabisa kuhusu ukweli katika maneno yako. Tumia mambo ya hakika na mifano kutoa hoja zako, na useme hasa jinsi wanavyoweza kujiondoa kwa tabia ya uasi, na uonyeshe njia ya kutenda—hivi ndivyo jinsi ya kuwashawishi watu. Ni wale tu wanaofanya hivi ndio wanaoweza kuwaongoza wengine; ni wao tu walio na uhalisi wa ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp