Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 80

Yohana 21:16-17 Akasema kwake tena mara ya pili, Simioni, mwana wa Yona, unanipenda mimi? Akasema kwake, Ndiyo, Bwana, unajua kwamba mimi nakupenda. Akasema kwake, Walishe kondoo wangu. Akasema kwake mara ya tatu, Simioni, mwana wa Yona, Unanipenda Mimi? Petro alisikitika kwa sababu alimwambia mara ya tatu, Unanipenda Mimi? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua vitu vyote, unajua kwamba mimi nakupenda. Yesu akamwambia, Walishe kondoo wangu.

Katika mazungumzo haya, Bwana Yesu alimwuliza Petro mara kadhaa kuhusu jambo moja: “Petro, je, unanipenda?” Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi ambacho Bwana Yesu alihitaji kutoka kwa watu kama vile Petro baada ya kufufuka Kwake, wanaoamini Kristo kwa kweli na kulenga kumpenda Bwana. Swali hili lilikuwa aina fulani ya uchunguzi, na aina fulani ya kuhoji, lakini hata zaidi lilikuwa hitaji na tarajio la watu kama Petro. Aliitumia mbinu hii ya kuuliza maswali ili watu waweze kuwaza na kuwazua kujihusu na kuangalia katika maisha yao wenyewe: Mahitaji ya Bwana Yesu kwa watu ni yapi? Je, nampenda Bwana? Mimi ni mtu anayempenda Mungu? Nafaa vipi kumpenda Mungu? Hata ingawa Bwana Yesu aliuliza tu swali hili kwa Petro, ukweli ni kwamba katika moyo Wake, Alitaka kutumia fursa hii ya kumwuliza Petro ili kuuliza swali la aina hii kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta kumpenda Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa Petro alibarikiwa kuwa mwakilishi wa mtu wa aina hii, ili kupokea swali hilo kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe.

Likilinganishwa na “nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani,” ambalo Bwana Yesu alimwambia Tomaso baada ya kufufuka Kwake, Yeye kumwuliza Petro swali mara tatu: “Simioni, mwana wa Yona, unanipenda mimi?” waruhusu watu kuweza kuhisi kwa njia bora zaidi ule ukali wa mwelekeo wa Bwana Yesu na umuhimu Aliouhisi wakati huu wa kuuliza maswali hayo. Kuhusiana naye Tomaso wa kushuku pamoja na asili yake ya udanganyifu, Bwana Yesu alimruhusu yeye kufikisha mkono wake na kuzigusa zile alama Zake za msumari, jambo ambalo lilimfanya yeye kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Adamu aliyefufuka na akatambua utambulisho wa Bwana Yesu kama Kristo. Na ingawa Bwana Yesu hakumkemea kwa ukali Tomaso, wala hakuonyesha kwa matamshi hukumu yoyote ilio wazi kwake, Alimjuza kwamba Alimwelewa kupitia kwa hatua za kimatendo, huku pia akionyesha mtazamo Wake na uamuzi wa aina hiyo ya mtu. Mahitaji na matarajio ya Bwana Yesu ya mtu wa aina hiyo hayawezi kuonekana kutokana na kile Alichosema. Kwa sababu watu kama Tomaso hawana katu imani ya ukweli. Mahitaji ya Bwana Yesu kwao yanapatikana tu katika, lakini mwelekeo Alioufichua kwa watu kama Petro ni tofauti kabisa. Hakuhitaji kwamba Petro aunyoshe mkono wake na kuzigusa hizo alama Zake za misumari, wala hakumwambia Petro: “usiwe bila imani, ila mwenye imani.” Badala yake, Alimwuliza Petro kwa kurudia swali lilo hilo. Hili lilikuwa swali la kuchokonoa fikira, na lenye maana ambalo halina budi kumfanya kila mfuasi wa Kristo kuhisi majuto, na woga, lakini pia kuhisi ile hali ya moyo wa wasiwasi, na huzuni ya Bwana Yesu. Na wakati wakiwa katika maumivu na mateso makali, wanaweza kuelewa zaidi wasiwasi wa Bwana Yesu Kristo na utunzaji Wake; wanatambua mafundisho Yake ya dhati na mahitaji makali kuhusu watu wasio na kasoro, waaminifu. Swali la Bwana Yesu linawaruhusu watu kuhisi kwamba matarajio ya Bwana kwa watu yaliofichuliwa kupitia kwa maneno haya mepesi si ya kuamini tu na kumfuata Yeye, lakini kutimiza yote kwa kuwa na upendo, kumpenda Bwana wako, kumpenda Mungu wako. Upendo wa aina hii ni wa utunzaji na utiifu. Ni wanadamu kuishi kwa ajili ya Mungu, kufa kwa ajili ya Mungu, kujitolea kila kitu chao kwa ajili ya Mungu, na kutumia na kutoa kila kitu chao kwa ajili ya Mungu. Upendo wa aina hii pia ni kumpa Mungu tulizo, kumruhusu Yeye kufurahia ushuhuda, na kumruhusu Yeye kupumzika. Ni fidia ya wanadamu kwa Mungu, uwajibikaji wao, na wajibu wao, na ni njia ambayo wanadamu lazima wafuate kwa maisha yao yote. Haya maswali matatu yalikuwa mahitaji na ushawishi ambao Bwana Yesu alitoa kwa Petro na watu wote ambao wangefanywa kuwa watimilifu. Ni maswali haya matatu ndiyo yaliyomwongoza na kumpa motisha Petro kukamilisha njia yake ya maisha, na yalikuwa maswali haya wakati ule wa Bwana Yesu kuondoka ambayo yalimfanya Petro kuanza njia yake ya kufanywa mtimilifu, na yaliyomwongoza, kwa sababu ya upendo wake kwa Bwana, kuutunza moyo wa Bwana, kumtii Bwana, kumpa tulizo Bwana, na kuyatoa maisha yake yote na kila kitu chake chote kwa sababu ya upendo wake.

Katika Enzi ya Neema, kazi ya Mungu ilikuwa kimsingi ya aina mbili ya watu. Wa kwanza alikuwa aina ya aliyeamini Kwake na kumfuata, ambaye angetii amri Zake, ambaye angeweza kuuvumilia msalaba na kuushikilia hadi katika njia ya Enzi ya Neema. Mtu wa aina hii angepata baraka za Mungu na kufurahia neema ya Mungu. Aina ya pili ya mtu alikuwa kama Petro, mtu ambaye angefanywa kuwa mtimilifu. Hivyo basi, baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alifanya kwanza mambo haya mawili yenye maana sana. Kwanza lilikuwa ni kwa Tomaso, na jingine lilikuwa kwa Petro. Mambo haya mawili yanawakilisha nini? Yanawakilisha nia za kweli za Mungu katika kuwaokoa binadamu? Yanawakilisha uaminifu wa Mungu kwa binadamu? Kazi Aliyoifanya na Tomaso ilikuwa ni kuwapa onyo watu wasiwe wanashuku, lakini kuamini tu. Kazi Aliyofanya na Petro ilikuwa ni kuipatia nguvu imani ya watu kama vile Petro, na kuweka wazi mahitaji ya aina hii ya watu, ili kuonyesha ni shabaha zipi wanafaa kuwa wakifuatilia.

Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alijitokeza kwa watu aliofikiria walifaa, Akaongea na wao, na kuwapa wao mahitaji, huku akiacha nyuma nia Zake, na matarajio Yake kwa watu. Hivi ni kusema, kama Mungu mwenye mwili, haijalishi kama ulikuwa katika wakati Wake akiwa mwili, au katika mwili wa kiroho baada ya kusulubishwa msalabani na kufufuliwa—haja Yake kwa wanadamu na mahitaji kwa wanadamu hayakubadilika. Alijali kuwahusu wanafunzi hawa kabla ya kufika msalabani; ndani ya moyo Wake, Alikuwa wazi katika hali ya kila mmoja, Alielewa upungufu wa kila mmoja, na bila shaka ufahamu Wake wa kila mtu ulikuwa namna ile ile baada ya Yeye kuaga dunia, kufufuka, na kuwa mwili wa kiroho kama hali ilivyokuwa Alipokuwa katika mwili. Alijua kwamba watu hawakuwa kwa kikamilifu na uhakika kuuhusu utambulisho Wake kama Kristo, lakini katika kipindi Chake akiwa mwili Hakuwa anatoa amri kali kuhusu watu. Lakini baada ya kufufuliwa Alijitokeza kwao, na Akawafanya wawe na hakika kabisa kwamba Bwana Yesu alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alitumia hoja hiyo ya uwepo Wake na kufufuka Kwake kama maono na motisha kubwa zaidi kwa muda mrefu katika ufuatiliaji wa wanadamu. Kufufuka kwake kutoka kifo hakukuwapa nguvu tu wale wote Waliomfuata, lakini pia kuliweka katika taathira kazi Yake ya Enzi ya Neema miongoni mwa wanadamu, na hivyo basi wokovu wa injili ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema kwa utaratibu ukaenea katika kila pembe ya binadamu. Unaweza kusema kwamba kutokea kwa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake kulikuwa na umuhimu wowote? Kama ungekuwa Tomaso au Petro wakati huo, na ukumbane na kitu hiki kimoja katika maisha yako ambacho kilikuwa na maana sana, ni athari ya aina gani ambayo kitu hicho kingekuwa nayo kwako? Je, ungeona huu kama msukumo wako katika kumfuata Mungu? Ungeona hali hii kama nguvu endeshi zako wewe kumfuata Mungu, kujaribu kumridhisha Yeye, na kufuatilia upendo wa Mungu katika maisha yako? Ungeweza kutumia jitihada za maisha yako yote ili kueneza maono haya makubwa zaidi? Ungefanya kueneza wokovu wa Bwana Yesu kuwa kazi unayokubali kutoka kwa Mungu? Hata ingawa hamjapitia haya, zile hali mbili za Tomaso na Petro tayari zinatosha kwa watu wa kisasa kuwa na ufahamu wazi kuhusu mapenzi ya Mungu na kumhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kuwa na maisha ya binadamu, na baada ya Yeye kuona uharibifu wa tabia wa wanadamu na hali ya maisha ya binadamu, Mungu katika mwili alihisi kwa kina ile hali ya kutojiweza, huzuni, na ukatili wa wanadamu. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake. Haya pengine ni mambo ambayo huwezi kuelewa, lakini Naweza kufafanua wasiwasi na utunzaji wa Mungu katika damu kwa kila mmojawapo wa wafuasi Wake kwa kauli hii: kujali kwingi. Hata ingawa kauli hii inatokana na lugha ya binadamu, na hata ingawa ni kauli yenye ubinadamu sana, inaonyesha kwa kweli na kufafanua hisia za Mungu kwa wafuasi Wake. Na kwa kujali kwingi kwa Mungu kwa ajili ya binadamu, kwa mkondo wa yale yote ambayo wewe umeyapitia utaanza kuhisi kwa utaratibu yote haya na kuyaonja. Hata hivyo, hali hii inaweza kutimizwa tu kwa kuelewa kwa utaratibu tabia ya Mungu kwa msingi wa kufuatilia mabadiliko katika tabia yako wewe binafsi. Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi. Kupitia kwa Kuonekana Kwake Aliipatia nguvu imani ya watu wote, na kupitia kwa Kuonekana Kwake alithibitishia ulimwengu hoja kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele, na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp