Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu
(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hiyo ni kusema, Agano Jipya na la Kale na Biblia ya Enzi ya Ufalme–Neno Laonekana Katika Mwili–kilichoonyeshwa na Bwana Yesu wa siku za mwisho aliyekurudi, Mwenyezi Mungu, ndizo imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova Mungu ya kuagiza sheria na amri na kuyaongoza maisha ya mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria; Agano Jipya linarekodi kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu wakati wa Enzi ya Neema; na Neno Laonekana Katika Mwili yote ni ukweli kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu wakati wa Enzi ya Ufalme, pamoja na maelezo ya kazi ya hukumu ya Mungu wakati wa siku za mwisho. Imani za msingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu ni matamko yote ya Mungu wakati wa hatua tatu za kazi, yaani, ukweli wote ulioonyesha na Mungu wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hizo ndizo imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.
Ukristo ulizaliwa na kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, lakini Bwana Yesu Kristo unaomwamini alifanya tu kazi ya ukombozi tu katika Enzi ya Neema. Kwa sababu Bwana Yesu mwenye mwili alisulubiwa na alitumika kama sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kumwokoa mtu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumtoa kutoka kwa hukumu na laana ya sheria, mtu alikuwa aje tu mbele ya Mungu na kukiri dhambi zake na kutubu ili kusamehewa dhambi zake na kufurahia neema karimu na baraka nyingi zilizofadhiliwa na Mungu. Hii ilikuwa kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu. Ingawa dhambi za mwanadamu zilisamehewa na ukombozi wa Bwana Yesu, mtu hakufutiwa asili yake ya dhambi, alikuwa bado amefungwa na kudhibitiwa nayo, na hangeweza kuepuka kufanya dhambi na kumpinga Mungu kwa kuwa mwenye kiburi na majivuno, akijitahidi kuwa na umaarufu na pato, kuwa na wivu na mgomvi, kusema uongo na kuwadanganya watu, kufuata mienendo miovu ya ulimwengu, na kadhalika. Mwanadamu hakuwa amejikomboa kutoka kwa utumwa wa dhambi na kuwa mtakatifu, na hivyo Bwana Yesu alitabiri mara nyingi kwamba angekuja tena kutekeleza kazi ya hukumu ya siku za mwisho, akisema: “Tazama, Naja upesi” (Ufunuo 22:12). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48). Pia imeandikwa katika Waraka wa Kwanza wa Petro kwamba “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ni Bwana Yesu aliyerejea. Yeye ameonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa binadamu, Ametekeleza kazi ya hukumu akianzia kwa nyumba ya Mungu, na Ametimiza kikamilifu unabii wa Biblia. Neno Laonekana Katika Mwili kilivyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni “neno ambalo Roho anayaambia makanisa” (Ufunuo 2:7) iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo, na ni maelezo ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kazi ya hukumu inayofanywa na Mwenyezi Mungu ni hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu, na pia ni hatua yake ya msingi na muhimu. Kama mtu anataka kuokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni, ni lazima akubali kazi ya Mungu ya hukumu, na katika hili kumetimizwa maneno ya Bwana Yesu: “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20). Ni kama tu mtu anakubali na kupitia hukumu na kuadibiwa kwa maneno ya Mungu anapoweza kufahamu utakatifu na haki ya Mungu, kujua kiini na asili ya upotovu wa mwanadamu na Shetani na ukweli wake wa kweli, kwa kweli kutubu mbele ya Mungu, kujiondolea mwenyewe dhambi zote, kufanikisha utakatifu, kuwa yule anayemtii Mungu na kumwabudu Mungu, na kuchumwa na Mungu. Ni hapo tu atakapokuwa na sifa kamili kuzirithi ahadi na baraka za Mungu, na kupata hatima nzuri.
Mungu alianza kazi ya kumwokoa mwanadamu kufuatia kuumba Kwake dunia, na mpango wa usimamizi Wake kwa wokovu wa binadamu hautakamilika hadi Yeye amalize kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Kutoka kwa maneno na ukweli wote ambao Mungu ameuelezea katika hatua tatu za kazi, tunaweza kikamiifu kuona kwamba, iwe ni kazi ya Mungu kufanyika kwa kutumia mtu hapo mwanzo wakati wa Enzi ya Sheria, au kazi Yake Alipokuwa mwili mara mbili katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, yote ni matamko na maonyesho ya ukweli ya Roho mmoja; katika kiini, ni Mungu mmoja ambaye hunena na kufanya kazi. Kwa hiyo, mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa Biblia na kutoka Neno Laonekana Katika Mwili.
(2) Kuhusu Neno Laonekana Katika Mwili
Neno Laonekana Katika Mwili ni matamshi ya kibinafsi ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, na ni ukweli wote ambao Mungu ameuonyesha ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu wakati wa kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Ukweli huu ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, ufunuo wa maisha na kiini cha Mungu, na maonyesho ya tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho. Ndizo njia ya pekee ambayo mtu anaweza kupitia ili kumjua Mungu na kutakaswa na kuokolewa. Maneno yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni kanuni kuu ya vitendo vya mtu na mwenendo, na hakuna methali za juu zaidi kwa maisha ya mwanadamu.
Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu husoma maneno ya Mungu katika Neno Laonekana Katika Mwili kila siku, kama vile tu Wakristo wa Ukristo husoma Biblia. Wakristo wote huchukua maneno ya Mungu kama mwongozo wa maisha yao na kama methali ya juu mno kuliko zote katika maisha. Katika Enzi ya Neema, Wakristo wote walisoma Biblia na kusikiliza mahubiri ya Biblia. Mabadiliko yalitokea hatua kwa hatua katika tabia za watu, na walifanya dhambi chache zaidina zaidi. Kadhalika, kupitia kusoma kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa maneno ya Mungu, Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu hatua kwa hatua huelewa ukweli na kuachana na utumwa wa dhambi, hawatendi tena dhambi na kumpinga Mungu, na kuwa wa ulingano na Mungu. Ukweli unathibitisha kwamba ni kwa kusoma maneno Mungu tu ndipo mtu anapoweza kutakaswa na kubadilishwa na kuishi kwa kudhihirisha picha ya mtu halisi. Huu ni ukweli ambao hakuna yeyote anayeweza kuukana. Maneno ya Mungu yaliyoandikwa katika Biblia yalionyeshwa Mungu alipofanya kazi katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, wakati Neno Laonekana Katika Mwili ni maneno yanayoonyeshwa na Mungu katika kazi ya siku za mwisho. Chanzo cha yote mawili ni kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu zimetimiza unabii katika Biblia kikamilifu, na Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, kama vile tu Bwana Yesu alivyosema: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). Hiyo, pia, ilitabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo kwamba, “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho anayaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). “Na nikaona katika mkono wa kuume wa Yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu ambacho kiliandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba. … tazama, Simba wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na kuifungua ile mihuri saba” (Ufunuo 5:1, 5).
Leo, sisi sote tumeona ukweli mmoja: Maneno yote yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, na yana mamlaka na nguvu–ni sauti ya Mungu. Hakuna anayeweza kukana au kubadilisha hili. Neno Laonekana Katika Mwili chapatikana bila vizuizi kwenye mtandao kwa watu wa nchi na maeneo yote kutafuta na kuchunguza. Hakuna yeyote ambaye huthubutu kukataa kwamba hayo ni maneno ya Mungu, au kwamba ni ya ukweli. Maneno ya Mungu yanaendesha ubinadamu mzima kuendelea mbele, watu wameanza hatua kwa hatua kuamka katikati ya maneno ya Mungu, na wao wanaendelea hatua kwa hatua kuelekea kuukubali ukweli na maarifa ya ukweli. Enzi ya Ufalme ni enzi ambapo maneno ya Mwenyezi Mungu hutawala duniani. Kila moja ya maneno ya Mungu litatimizwa na kukamilishwa. Kama tu vile waumini wote katika Mungu hukiri Biblia leo, watu ambao wanaamini katika Mungu watakiri hivi karibuni kwamba Neno Laonekana Katika Mwili ni maneno ya Mungu katika siku za mwisho. Leo, Neno Laonekana Katika Mwili ni msingi wa imani za Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kwa hakika utakuwa msingi wa kuwepo kwa wanadamu wote katika enzi ijayo.
(3) Kuhusu Majina ya Mungu na Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Kufuatia upotovu wake na Shetani, mwanadamu huishi chini ya miliki ya Shetani na upotovu wake umeongezeka kwa kina kuliko wakati uliopita. Mwanadamu hawezi kujiondolea minyororo ya dhambi, na huhitaji wokovu wa Mungu. Kwa mujibu wa mahitaji ya wanadamu wapotovu, Mungu amefanya hatua tatu za kazi katika Enzi ya Sheria, katika Enzi ya Neema, na katika Enzi ya Ufalme. Katika Enzi ya Sheria, Mungu alifanya kazi ya kuagiza sheria na amri na kuongoza maisha ya mwanadamu. Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili, juu ya msingi wa kazi Yake katika Enzi ya Sheria, akatekeleza kazi ya kusulubiwa na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu kwa mara nyingine tena amepata mwili na, juu ya msingi wa kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, hutekeleza kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu, huonyesha ukweli wote wa kwa ajili ya utakaso na wokovu wa mwanadamu, na hutuletea njia pekee kwa ajili ya ufuatiliaji wa utakaso na wokovu. Ni kama tu tukichuma hali halisi ya ukweli kama maisha yetu, tukiwa wale ambao humtii na kumwabudu Mungu, tutakapokuwa na sifa kamili kuongozwa katika ufalme wa Mungu na kupokea ahadi na baraka za Mungu. Hatua tatu za kazi ya Mungu ya wokovu wa mwanadamu zimeunganika kwa karibu, kila hatua ni ya lazima, kila moja huenda juu mno na kuwa na kina zaidi ya ile ya mwisho, zote ni kazi ya Mungu mmoja, na ni hatua hizo tatu tu za kazi ya Mungu ambazo ni kazi kamili ya wokovu wa wanadamu.
Majina matatu–Yehova, Yesu, na Mwenyezi Mungu–ni majina tofauti ambayo Mungu ameyachukua katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Mungu huchukua majina tofauti kwa sababu kazi Yake inatofautiana katika enzi tofauti. Mungu hutumia jina jipya kuanza enzi mpya na kuwakilisha kazi ya enzi hiyo. Jina la Mungu lilikuwa Yehova katika Enzi ya Sheria, na Yesu katika Enzi ya Neema. Mungu hutumia jina jipya–Mwenyezi Mungu–katika Enzi ya Ufalme, akitimiza unabii katika Kitabu cha Ufunuo: “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika… Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu Wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, na nitaliandika jina la Mungu Wangu juu yake, na jina la mji wa Mungu Wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu: na nitaliandika juu yake jina Langu jipya” (Ufunuo 3:7, 12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena Mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1: 8). Ingawa majina ya Mungu na kazi katika enzi hizo tatu ni tofauti, kuna Mungu mmoja tu katika kiini, na chanzo ni kimoja.
Kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu hasa hushirikisha hatua tatu za kazi. Yeye ametumia majina tofauti katika kila enzi, lakini kiini cha Mungu hakibadiliki kamwe. Hatua tatu za kazi hufanywa na Mungu mmoja; hivyo, Yehova, Yesu, na Mwenyezi Mungu ni Mungu yule yule mmoja. Yesu alikuwa ni kuonekana kwa Yehova, na Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na hivyo Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli ambaye aliziumba mbingu na ardhi na vitu vyote, huamrisha vitu vyote, na hushikilia ukuu juu ya kila kitu, na Yeye ndiye yule wa milele na Muumba pekee.
Katika hatua tatu za kazi ya kumwokoa mwanadamu, Mungu ameifichua tabia Yake yote kwa mwanadamu, akituruhusu tuone kwamba tabia ya Mungu si huruma na upendo tu, lakini pia haki, uadhama, na ghadhabu, kwamba kiini Chake ni utakatifu na haki, na ni ukweli na upendo, kwamba tabia ya Mungu na mamlaka na nguvu za Mungu hazimilikiwi na kiumbe chochote kilichoumbwa au kisichoumbwa. Tunaamini kuwa maneno yote ambayo Mungu ameyasema tangu wakati wa uumbaji hadi mwisho wa dunia ni ukweli. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno ya Mungu kamwe hayatatoweka, na kila mojawapo litatimizwa!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?