Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena
Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mungu mwenye mwili Amekamilisha kazi ya "ujio wa siri wa Mwana wa Adamu" Aliyetabiriwa katika Biblia, na hivi karibuni Ataonekana kwa umma katika kila taifa na sehemu ulimwenguni. Watu wote katika kila taifa na sehemu walio na kiu cha kuonekana kwa Mungu watatarajia kuonekana kwa Mungu hadharani. Hakuna nguvu zinazoweza kuzuia au kuangamiza ufalme wa Mungu, na mtu yeyote ambaye anapinga Mungu ataadhibiwa na ghadhabu ya Mungu, kama vile inavyosemwa katika maneno ya Mungu: “Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya matrilioni ya watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui mara tena. Wakati umewadia! Ninataka kazi Yangu ianze, Ninataka kuwa kiongozi mkuu juu ya mwanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!” "Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, gadhabu, na adhabu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!"
09/06/2017