Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?
Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu huamini katika Mungu huyo huyo. Watu wanaoelewa historia ya dini wanajua kwamba Uyahudi wa Israeli ulizaliwa na kazi ambayo Yehova Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria. Ukristo, Ukatoliki, na Othodoksi ya Mashariki yote yalikuwa makanisa yaliyoibuka baada ya Bwana Yesu mwenye mwili kufanya kazi ya ukombozi. Vivyo hivyo, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwepo wakati Mungu alipopata mwili wakati wa siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu. Wakristo katika Enzi ya Neema walisoma Agano la Kale na Jipya la Biblia, na Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme sasa wanasoma Neno Laonekana Katika Mwili, ambalo lilikuwa likizungumzwa na Mungu binafsi katika siku za mwisho. Ukristo huzingatia kazi ya ukombozi ambayo Bwana Yesu alifanya wakati wa Enzi ya Neema, na Kanisa la Mwenyezi Mungu huikubali kazi ya hukumu ya siku za mwisho za Bwana Yesu aliyerudi, Mwenyezi Mungu. Tofauti kati ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kwamba Ukristo huzingatia kazi ambayo Mungu alifanya wakati wa Agano la Kale na Enzi ya Neema, wakati Kanisa la Mwenyezi Mungu huzingatia kazi ya hukumu ikianzia na nyumba ya Mungu ambayo Mungu ametekeleza wakati wa siku za mwisho. Tofauti kati ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu ni sawa na tofauti kati ya Ukristo na Uyahudi: Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alitekeleza kazi ya ukombozi wa watu juu ya msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Lakini makuhani wakuu, walimu wa sheria na Mafarisayo wa Kiyahudi hawakujua kwamba Bwana Yesu alikuwa ni Yehova aliyepata mwili, kwamba Alikuwa Masihi waliyekuwa wakimsubiri. Kwa ukaidi walishikilia sheria na amri za Agano la Kale zilizotangazwa na Yehova Mungu. Pia walimsulubisha Bwana Yesu wa huruma, ambaye alikuwa amewaokoa wanadamu, hivyo wakiikosea tabia ya Mungu. Kisha Mungu akauacha Uyahudi mzima, ambao ulishikilia sheria za Agano la Kale, na kuuelekeza wokovu Wake kwa Watu wa mataifa–ambao, baada ya kumkubali na kumfuata Bwana Yesu, waliunda makanisa ya Agano Jipya, ambayo pia yaliitwa Ukristo. Wakati huo huo, Wayahudi, ambao walishikilia tu kazi ya Bwana Mungu wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale na kukataa kazi ya ukombozi wa Bwana Yesu, waliunda kile kinachojulikana kuwa Uyahudi. Vivyo hivyo, juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi katika Enzi ya Neema, Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya hukumu akianzia na nyumba ya Mungu katika Enzi ya Ufalme. Watu wengi kutoka madhehebu yote ya Kikristo wanaopenda ukweli na kutamani sana kuonekana kwa Bwana husoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyatambua kuwa sauti ya Mungu. Wakiwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, walimkubali Mwenyezi Mungu na hivyo Kanisa la Mwenyezi Mungu likatokea. Kutokana na haya inaweza kuonekana kuwa Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu huamini katika Mungu yule yule—Bwana aliyeziumba mbingu na ardhi na vitu vyote. Ni kwamba tu jina na kazi ya Mungu ambazo watu hushikilia ni tofauti: Kanisa la Mwenyezi Mungu huzingatia jina jipya la Mungu wakati wa Enzi ya Ufalme, na hukubali kazi mpya inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho, wakati Ukristo hushikilia jina la Mungu wakati wa Enzi ya Neema, na hukubali kazi ya zamani ambayo Mungu alifanya wakati wa enzi za zamani. Hii ndiyo tofauti muhimu zaidi kati ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Mungu ambaye wote wawili huamini, hata hivyo, ni mmoja: Mungu pekee wa kweli aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote. Huu ni ukweli ambao hakuna yeyote anayeweza kuugeuza au kuukana!
Wakristo wengi wanaamini kwamba wao wanahitaji tu kuikubali kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ili kuingia katika ufalme wa mbinguni, na hawahitaji pia kuikubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Dhana kama hizo si sahihi kabisa. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi. Watu waliokolewa kwa sababu ya imani yao, na hawakuhukumiwa tena na sheria na kuuawa kwa sababu ya makosa yao. Lakini Bwana Yesu alizisamehe dhambi za mwanadamu tu, na hakuisamehe au kutatua asili ya mtu ya dhambi. Tabia za kishetani miongoni mwa watu–kiburi na hali ya majivuno, ubinafsi na ulafi, ukora na udanganyifu, na uasi na upinzani dhidi ya Mungu - bado ulikuwepo. Watu walikuwa bado hawajatakaswa kabisa, kuokolewa, na kuchumwa na Mungu. Hivyo, Bwana Yesu alisema mara nyingi kwamba ni lazima Arudi. Katika sehemu nyingi katika Biblia inatabiriwa kwamba Mungu sharti arudi na kufanya hukumu, kuwaleta watakatifu katika ufalme wa mbinguni. Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho ameonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu, na Ametekeleza kazi mpya ya hukumu kuanzia nyumba ya Mungu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi wa Bwana Yesu. Ni ili kutatua asili ya dhambi ya wanadamu, na kumruhusu mwanadamu kujikomboa kabisa kutoka kwa utumwa na vikwazo vya dhambi, kuishi kwa kudhihirisha sura ya mwanadamu halisi na kuchumwa na Mungu, na kuingia hatima nzuri iliyotayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Inaweza kusemwa kuwa kazi ya ukombozi iliyotekelezwa na Bwana Yesu ni msingi wa kazi ya wokovu wa Mungu ya siku za mwisho, wakati kazi ya hukumu ya siku za mwisho ni kiini na lengo la kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo hatua ya kazi ambayo ni ya maana sana na muhimu kwa wokovu wa wanadamu. Ni wale tu ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu ya siku za mwisho watakaokuwa na fursa ya kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni na kuwa wale wanaojipata mbele ya Mungu. Leo, watu wengine katika makundi na madhehebu mbalimbali ya ulimwengu wa kidini wameona kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu wakati wa siku za mwisho, na hivyo wamekubali na kuanza kumfuata Mwenyezi Mungu. Baadhi ya wasioamini pia wamemkubali Mwenyezi Mungu kwa sababu ya ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu. Watu hawa ambao huamini katika Mwenyezi Mungu hukamilisha Kanisa la Mwenyezi Mungu. Chini ya uongozi na uchungaji wa Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, kupitia kupata uzoefu na kuweka katika matendo maneno ya Mwenyezi Mungu, hatua kwa hatua huja kuelewa ukweli mwingi, na wameona kwa dhahiri chanzo na kiini cha upotovu wa wanadamu. Chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, watu hakika na kwa kweli wameonja tabia ya Mungu ya haki na isiyoweza kukosewa. Kwa sababu wanamjua Mungu, hatua kwa hatua wamepata kumwogopa Mungu na kujiepusha na uovu, na kuishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu. Pamoja na ufahamu wao wa ukweli, maarifa ya watu ya Mungu imeongezeka hatua kwa hatua, utii wao kwa Mungu umekuwa mkubwa zaidi kuliko wakati wowote, na wameweka ukweli zaidi na zaidi katika vitendo. Bila kutambua, watu hawa watakuwa wamejikomboa kikamilifu kutoka kwa dhambi na kupata utakatifu. Wakristo ambao hawakubali kazi mpya ya Mwenyezi Mungu, wakati huo huo, bado huamini Ukristo. Wao hushikilia jina la Bwana Yesu, kutii mafundisho ya Biblia, na kwa muda mrefu tayari wametupwa katika giza na Mungu, wakipoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu. Huu ni ukweli unaotambuliwa. Kama watu wakisisitiza kutotubu, na kwa upofu kumshutumu na kumpinga Bwana Yesu aliyerudi katika siku ya mwisho, Mwenyezi Mungu, na kukataa kuikubali kazi ya Mwenyezi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, basi mwishowe, wote wataondolewa na kazi ya Mungu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?