Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

09/06/2017

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mungu mwenye mwili Amekamilisha kazi ya "ujio wa siri wa Mwana wa Adamu" Aliyetabiriwa katika Biblia, na hivi karibuni Ataonekana kwa umma katika kila taifa na sehemu ulimwenguni. Watu wote katika kila taifa na sehemu walio na kiu cha kuonekana kwa Mungu watatarajia kuonekana kwa Mungu hadharani. Hakuna nguvu zinazoweza kuzuia au kuangamiza ufalme wa Mungu, na mtu yeyote ambaye anapinga Mungu ataadhibiwa na ghadhabu ya Mungu, kama vile inavyosemwa katika maneno ya Mungu: “Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya matrilioni ya watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui mara tena. Wakati umewadia! Ninataka kazi Yangu ianze, Ninataka kuwa kiongozi mkuu juu ya mwanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!” "Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, gadhabu, na adhabu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!" Kazi ya kipekee ya Mungu imebaini wapinga Kristo wote, manabii wa uongo, na wanaodanganya. Imewafichua waumini wa uongo watakao tu neema ya Mungu na kula mikate na kupata ujazo. Neno la Mungu la hukumu ni kama upanga mkali, wenye makali kuwili ambao huuchoma moyo wa mtu na roho, na kusababisha wale ambao huchukia kukemewa, wanaokataa maneno safi, na ambao hawana upendo wa kweli kuonyesha hulka yao. Kwa maneno ambayo Mungu anonyesha wakati wa ujio wake wa siri kufanya kazi, tunaona ukweli wa upinzani wa wanadamu kwa Mungu na uasi dhidi ya Mungu, ambalo linadhihirika hasa katika mambo matatu:

1. Kwamba wanadamu mara nyingi hutenda dhambi na hupinga na kuasi dhidi ya Mungu ni hasa kwa sababu, kutokana na upotoshwaji wa watu na Shetani, asili yao imemilikiwa na sumu za aina mbalimbali za Shetani, na wamekuwa wale ambao hupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Hivyo wao hutenda dhambi kila siku, na mara nyingi hukiri dhambi zao, lakini bado hawawezi kutoroka kutoka kwa utumwa na minyororo ya asili yao ya kishetani. Asili ya mtu ambaye huasi dhidi ya Mungu ndicho kiini cha dhambi zake.

2. Wanadamu wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa sana. Mioyo ya watu haijajazwa na kitu kingine ila falsafa za Shetani, sheria za Shetani za maisha, na njia za Shetani za kufikiri, vikiwafanya kutoweza kuelewa au kujua kwamba neno la Mungu ni ukweli. Bila kupashwa nuru na kuangazwa kwa Roho Mtakatifu, wanadamu hawawezi kukubali ukweli. Hata kama watu wapotovu wanaamini katika Mungu, watu tu hukubali kuwa kuna Mungu; hawakiri kwamba Mungu ni kweli. Kwa hiyo, wanadamu wapotovu mara nyingi hupitisha hukumu kwa Mungu, humshambulia Mungu, kumpinga Mungu na kuasi dhidi ya Mungu.

3. Wanadamu wamepotoshwa kwa kiasi kikubwa na Shetani. Hata wale ambao wameamini katika Mungu kwa miaka mingi hawatawahi kamwe kumjua Mungu bila hukumu yake na kuadibu, au kazi ya wokovu ya nyama ya kuwa mwili. Katika imani yao katika Mungu, wanaweza tu kufurahia neema ya Mungu na kukubali kuwa Mungu kweli Yupo. Hawawezi kwa kweli kumjua Mungu. Wanaweza tu kujazwa na mafundisho ya kidini na dhana, wakiwa milele na kiburi na kujiona kuwa waadilifu, na hata kuthubutu kumhukumu Mungu, kumshutumu Mungu, na kuikufuru kazi ya Mungu. Mambo haya si kitu kipya, lakini hutokea mara nyingi katika dunia ya kidini, jambo linalotoa wito kwa tafakari kubwa ya watu, na maneno ya Yesu yametimia kabisa: "Si kila mtu aliyeniambia, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbingu; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako tumetoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo Nitakapowaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu." Sisi sote tumeona wazi kuwa katika dunia ya kidini, kuna watu wengi sana wanaofanya kazi kwa jina la Bwana lakini hupinga na kushutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Wale wote ambao wanaamini katika Mungu, lakini hukubali tu kuwa kuna Mungu na hawajui kwamba Mungu ndiye ukweli, huenda wakamkataa Mungu, kumshambulia Mungu, na kukufuru dhidi ya Mungu. Kuwa na ujuzi haba wa Biblia na mafundisho ya dini, wanaamini kuwa wao wanaumiliki ukweli na kumjua Mungu. Hata huthubutu kukufuru dhidi ya kazi ya Roho Mtakatifu na kumbisha Kristo aliyepata mwili. Kitu cha pekee kinachowangoja ni hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa uadilifu, adhimu, na kwenye ghadhabu. Katika siku ya kuwasili Mungu kwa umma, yote yatafichuliwa! Kutoka kwa watu wanaoihubiri Injili katika maeneo mbalimbali, mara nyingi tumesikia kwamba wengi wa wale ambao wakati fulani waliipinga kazi ya Mwenyezi Mungu, au ambao waliingilia na kuwakinga watu kumkubali Mwenyezi Mungu, waliadhibiwa na kulaaniwa kwa viwango mbalimbali. Inaweza kusemwa kuwa hili, kwa kiasi fulani, limetekeleza wajibu bayana na wa kutia hamasa kwa jukumu la kazi yetu ya injili. Baada ya kusikia habari kama hizo, hatungeweza kujizuia kuusifu uadilifu wa Mungu; zaidi ya hayo, tulimshukuru Mungu kwa kusikiliza sala zetu. Aidha, upendezwaji na uchaji kwa kuwa Mungu aliinuka kwa hiari katika mioyo yetu. Mungu hatawatupa kondoo ambao ni mali Yake, wala kumwachilia yeyote mwenye kufanya maovu na kumpinga Yeye. Mungu yuko kila mahali na ni mwenye kudura, na kazi ya Mungu haiwezi kuzuiliwa kwa nguvu yoyote ya uadui. Mungu ametuonyesha visa vingi vya uovu ukiadhibiwa. Tunaamini kuwa hili pia ni onyo la kimya kwa kila mmoja wetu. Hivyo, tumekusanya matukio mengi ya watu wakiadhibiwa, upeo ambao umeenea kwa Kanisa Katoliki na madhehebu na makundi mbalimbali ya Kikristo. Kipindi cha muda ni kutoka tu mwaka wa 1993 hadi 2002, na maeneo yamejumuisha mikoa 24 na miji ya manisipaa. Kwa jumla tumekusanya visa zaidi ya elfu kumi vya watu wakiadhibiwa kwa kumpinga Mwenyezi Mungu, ambapo kati yavyo tumechagua visa zaidi ya mia nane na sabini vilivyo vya mfano mmoja. Lakini visa hivi pekee vyatosha kwa watu wote kujifunza mafundisho kutoka kwazo (taz. Kesi Wakilishi za Adhabu kwa Kumpinga Mwenyezi Mungu). Kutoka kwa visa hivi vya kushangaza vya wale walioadhibiwa kwa kumpinga Mungu, tumebainisha aina nne kuu za watu ambao walikuwa shadidi kiasi katika upinzani wao kwa Mungu: Ya kwanza: Watu hawa walidanganywa na wengine au kutawaliwa na watumishi waovu kutokana na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu na kushindwa kutambua. Hivyo, wao waliwafuata kwa kufanya maovu, na kuiga maneno yao, wakizungumza maneno mengi katika upinzani dhidi ya Mungu na kufanya matendo maovu na kuwazuia watu kuikubali kazi ya Mungu. Mungu alitoa adhabu hafifu tu kwa watu hawa, na hakusitisha maisha yao. Baadhi yao walipata magonjwa ya ajabu, na wengine wakapatwa na ajali au familia zao kukumbwa na majanga. Mungu aliwapa watu wa aina hii nafasi ya kutubu. Bila shaka, pia kulikuwa na baadhi ya wale hasa wakaidi ambao bado hawakuamka baada ya kuadhibiwa; waliendelea kufanya maovu na kwa hivyo walitengwa. La pili: Wengi wa watu hawa walikuwa viongozi wa madhehebu mbalimbali na makundi ya makanisa. Walikuwa wanakabiliwa na uchaguzi kati ya nafasi zao na Mungu. Kwa minajili ya nafasi zao, waliacha njia ya kweli, kwa makusudi wakaipinga kazi ya Mungu, na kuwadhibiti watu waliokuwa chini yao. Ili milele wafurahie fadhila zilizoletwa na nafasi zao, waliwadanganya na kuwanasa watu. Ilionekana kwamba wangepoteza nafasi zao kama wangepoteza watu wao, na hawakuweza kuishi bila nafasi yao. Kwa hiyo, walifanya chochote walichoweza ili kushindana na Mungu kwa ajili ya watu Wake wateule, wakiita kondoo wa Mungu kondoo wao. Walikuwa mfano wa wapinga Kristo. Kile walichokishughulikia ni nafasi zao na maisha. Mioyo yao ikawa zaidi na zaidi migumu. Walifurahia neema ya Mungu na bado wao pia walitaka kuwadhibiti watu wa Mungu waliochaguliwa, bila hata kuwapa uhuru wa kuchagua ambao walistahili. Hawa walikuwa ndio watumishi waovu sana waliotabiriwa na Bwana Yesu. Mungu pia aliadhibu watu hawa kwa viwango tofauti kulingana na tabia zao, na pia akawapa nafasi ya kutubu. Lakini baadhi yao walikwenda hata zaidi, na wakapendelea kufa badala ya kutubu. Hivyo Mungu akamaliza maisha yao. Kwa wale ambao walijizuia wenyewe au kuacha kufanya maovu baada ya kuadhibiwa, Mungu aliyahurumia maisha yao na bado anawasubiri kutubu.

La tatu: Watu hawa walikuwa zamani wamemilikiwa na roho wabaya, ama, wakati mwingine, waliwategemea roho wabaya kuonyesha nguvu za kimiujiza. Watu hawa waliamini katika kazi ya roho wabaya ndani yao, lakini hawakuwa na ujuzi hata kidogo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, walipohubiriwa kazi mpya ya Mungu, iliamsha upinzani mkali ndani yao. Aina hii ya watu walikuwa hasa maadui wa kazi ya Roho Mtakatifu, na walichukia ukweli ulioonyeshwa na Mungu zaidi ya yote. Katika madhehebu yote na makundi ya kidini, sauti ya upinzani wao kwa Mungu ndiyo iliyokuwa kubwa zaidi, matendo yao yalikuwa maovu zaidi, na upinzani wao kwa Mungu wenye fujo na ari zaidi. Watu hawa walikuwa ndio zana za roho waovu, maadui wa Mungu, na washiriki wa Shetani, na hivyo wote waliishia kulaaniwa, na waliandikiwa kuteseka milele na kuangamia.

La nne: Watu hawa walioadhibiwa walikuwa ndio msingi wa Kanisa la Utatu wa Binafsi. Walifanya huduma na walitoa maisha yao hasa kwa Chama cha Kikomunisti na walikuwa katika uadui kwa wale wote ambao kweli wanamwamini Mungu. Wakiungwa mkono na nguvu ya serikali, waliwatesa wale ambao kwa kweli walimfuata Mungu na kushuhudia kwa Mungu, wakitumika kama zana za serikali. Walishikilia "bakuli ya mchele" iliyotolewa na Chama cha Kikomunisti, walizungumza na kutoa maisha yao kwa ajili ya Chama cha Kikomunisti, na kuwa wasemaji wa Chama cha Kikomunisti katika ulimwengu wa kidini. Chama cha Kikomunisti kilikuwa, kwa kweli, bwana wao. Watu hawa walishikilia vyeo vya uongozi vya makanisa katika maeneo mengi, na waliwadhibiti waumini wasiojua katika mikono yao. Watu hawa walikuwa si kitu bali mashetani waliompinga Mungu. Kwa kweli walikuwa si waumini katika Ukristo. Ingawa walienea kote kwa muda, walikuwa wameandikiwa kulaaniwa na kuangamizwa.

Watu hawa maarufu katika Kanisa Katoliki na madhehebu na makundi mbalimbali ya Kikristo wote waliadhibiwa na Mungu, na hata walilaaniwa na kufa, kwa sababu waliishutumu kazi ya Mungu na kuzuia mapenzi ya Mungu kutekelezwa. Je, si hili ni jambo muhimu kwa watu kulijadili? Kama Yule waliyempinga hakuwa Mungu, ni nani angeweza kuwaadhibu na kuchukua maisha yao? Kama kweli walikuwa mali ya Mungu, ni nani angekuwa na uwezo wa kuchukua maisha yao mbali na mkono wa Mungu? Je, hutambui kwamba Mungu ni mwenye haki?

Kutoka visa vya aina hizi nne za watu na matendo yao, tunaweza kuona wazi kwamba, katika asili yao, hawakupenda ukweli. Walishikilia mtazamo wa uadui kwa kazi ya Mungu ya kumwokoa na kumbadilisha mtu kwa njia ya hukumu na kuadibu, walichukia sana neno la Mungu linalofichua asili ya mtu na kudunga roho ya mtu, na hata walikasirika kana kwamba ujio wa Mungu ulikuwa umekatiza ndoto zao nzuri. Hivyo mioyo yao ya kulalamika dhidi ya Mungu na asili yao ya uasi dhidi ya Mungu ilikuwa imefichuliwa kabisa. Hata walimshutumu, wakamkufuru, na kumpinga Mungu kifidhuli, kama wamejawa na majivuno ya ufidhuli. Walikuwa waovu sana zaidi ya Mafarisayo waliomtesa Bwana Yesu miaka elfu mbili iliyopita. Matendo yao maovu yalisababisha wao kuadhibiwa na kulaaniwa. Wengi wao waligundua kwamba tabia ya Mungu kwa kweli si ya kukosewa wakati tu kifo kilipokuja. Lakini waliweza kulia tu na kusaga meno yao kwa giza. Ukweli umebainisha kwamba wale wamsulubishao Kristo kwa mara nyingine tena watahukumiwa!

Mwenyezi Mungu alisema: “Ufalme unapanuka katikati ya ubinadamu, unachipua katikati ya ubinadamu, unasimama katikati ya ubinadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu ako nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; ubinadamu utaguswa vipi? Umeona na macho yako hali ya mwanadamu; hakika bado huna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbiakimbia kwa ajili Yangu Nitawaadhimisha, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Umewahi kuzikubali baraka ulizopewa? Umewahi kutafuta ahadi ulizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, utapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, hutapoteza mwangaza unaokuongoza, katikati ya giza. Hakika utakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika utakuwa mshindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, utasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika utakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso unayovumilia, utarithi baraka zinazotoka Kwangu, na hakika utayaangazia yote ulimwenguni na utukufu Wangu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp