Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 139

06/08/2020

Mungu mwenye mwili hawezi kukaa na mwanadamu milele kwa sababu Mungu Ana kazi zingine nyingi za kufanya. Yeye hawezi kufungwa katika mwili; Yeye Anavua mwili ili Afanye kazi ambayo Anahitaji kufanya, ingawa yeye Anafanya kazi hiyo kwa mfano wa mwili. Wakati Mungu Anakuja duniani, Yeye hasubiri hadi Afike hali ambayo mwanadamu wa kawaida anapaswa kufika maishani kabla ya kufa na kuondoka. Haijalishi mwili wake ni wa umri gani, wakati kazi Yake imemalizika, Anaondoka na kumwacha mwanadamu. Hakuna kitu kama umri Kwake, Yeye hahesabu siku zake kulingana na maisha ya mwanadamu. Badala yake Yeye hukamilisha maisha Yake katika mwili kulingana na hatua ya kazi Yake. Baadhi ya wanadamu wanaweza kuhisi kwamba Mungu, ambaye Anakuja katika mwili, lazima akue mpaka afikie hatua fulani, Awe mwanadamu mzima, kufikia umri wa uzee, na kuondoka tu wakati mwili umeshindwa. Haya ni mawazo ya mwanadamu; Mungu Hafanyi kazi kwa namna hiyo. Yeye Anakuja katika mwili kufanya kazi Anayostahili kufanya, si kuishi maisha ya mwanadamu ya kuzaliwa kwa wazazi, kuwa mtu mzima, kutengeneza familia na kuanza kazi, kupata watoto, au kupitia panda shuka za maisha—hali ya maisha ya kawaida. Mungu kuja duniani ni Roho wa Mungu kuletwa katika mwili, na kuja katika mwili, bali Mungu Haishi maisha ya kawaida ya binadamu. Yeye Huja tu kukamilisha sehemu moja katika mpango wa usimamizi Wake. Baada ya hapo Atamwacha mwanadamu. Atakapokuja katika mwili, Roho wa Mungu hakamilishi ubinadamu wa kawaida wa mwili. Badala Yake, kwa wakati Alioweka, Uungu unafanya kazi moja kwa moja. Kisha, baada ya kufanya yote ambayo Yeye Anahitajika kufanya na kukamilisha huduma Yake, kazi ya Roho wa Mungu katika hatua hii imekamilika, na wakati huo maisha ya Mungu katika mwili yanaisha, haijalishi kama mwili Wake umekamilisha maisha yake au la. Hiyo ni, hatua ya maisha ambayo mwili unafika, muda ambao unaishi duniani, yote hutegemea kazi ya Roho. Haihusiani kwa vyovyote na kile mwanadamu anachoona kuwa ukawaida wa ubinadamu. Chukua Yesu kama mfano. Yeye Aliishi katika mwili kwa miaka thelathini na mitatu na nusu. Katika suala la urefu wa maisha ya mwili wa binadamu, Yeye Hakupaswa kufariki Akiwa na umri huo na Hakupaswa kuondoka. Lakini Roho wa Mungu hakujali kuhusu hayo yote. Wakati kazi Yake ilimalizika, mwili ulichukuliwa, ukatoweka na Roho. Hii ni kanuni ya jinsi Mungu Hufanya kazi katika mwili. Hivyo, kusema kwa kweli, Mungu katika mwili Hana ubinadamu wa kawaida. Tena, Yeye Haji duniani kuishi maisha ya kawaida ya binadamu. Yeye Haimarishi kwanza maisha ya kawaida ya binadamu kisha Aanze kufanya kazi. Badala Yake, mradi tu Amezaliwa katika familia ya kawaida ya binadamu, Yeye Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Yeye hana nia za mwanadamu hata kidogo; Yeye si wa mwili, na yeye hakika Hajihusishi na njia za jamii au kujihusisha katika mawazo ya mwanadamu au fikra, au kujiunga na falsafa ya maadili ya binadamu. Hii ni kazi ambayo Mungu mwenye mwili Anataka kufanya na umuhimu wa vitendo vya mwili wake. Mungu Anakuja katika mwili kimsingi kufanya hatua ya kazi inayohitaji kufanyika katika mwili. Yeye Hajihusishi na michakato isiyo na maana, na Yeye hapitii matukio ya kawaida ya mwanadamu. Kazi ambayo Mungu katika mwili Anahitaji kufanya haina hali ya kawaida ya binadamu. Hivyo, Mungu Anakuja katika mwili ili kutimiza kazi Anayohitaji kukamilisha katika mwili. Mengine yote Hayamhusu. Hafuati hatua zisizo za maana. Mara kazi Yake inapokamilika, umuhimu wa mwili Wake unaisha. Kumaliza hatua hii kuna maana kazi ambayo Yeye Anahitajika kufanya katika mwili imekamilika, huduma ya mwili Wake imekamilika. Lakini Yeye hawezi kuendelea kufanya kazi katika mwili kwa muda usiojulikana. Yeye lazima Aende mahali pengine kufanya kazi, mahali ambapo ni nje ya mwili. Ni kwa njia hii tu ndio anaweza kukamilisha na kupanua zaidi kazi Yake. Mungu hufanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Yeye Anajua Anayohitaji kufanya na Aliyohitimisha kama kiganja cha mkono wake. Mungu Humwongoza kila mwanadamu kwenye njia ambayo Yeye tayari Amechagua. Hakuna anayeweza kuepuka hili. Ni wale tu ambao hufuata uongozi wa Roho wa Mungu ndio watakaokuwa na uwezo wa kuingia katika pumziko. Huenda ikawa katika kazi ya baadaye, sio Mungu Anayemwongoza mwanadamu kwa kuongea katika mwili, ila ni Roho anayeonekana ndiye anayeongoza maisha ya mwanadamu. Hapo tu ndipo mwanadamu atakuwa na uwezo wa uthabiti wa kugusa Mungu, kuona Mungu, na kwa kikamilifu zaidi kuingia katika hali halisi ambayo Mungu Anataka, ili aweze kukamilishwa na Mungu wa vitendo. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Anataka kukamilisha, Ambayo amepanga kwa muda mrefu. Kutokana na hili, mnapaswa nyote kuona njia ambayo mnapaswa kuchukua!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp