Watu Kote Ulimwenguni Wajifunza Kichina | Ukariri na Kwaya: Zingatia Hatima ya Wanadamu | Sauti za Sifa 2026

18/01/2026

1

Ninawahimiza watu wa mataifa yote na wa nchi zote, na hata wa tasnia zote wasikilize sauti ya Mungu, waitazame kazi ya Mungu, na wazingatie hatima ya wanadamu, na hivyo kumfanya Mungu kuwa ndiye mtakatifu zaidi, mwenye kuheshimiwa zaidi, mkuu zaidi, na wa pekee wa kuabudiwa miongoni mwa wanadamu, na kuwawezesha binadamu wote waishi katikati ya baraka za Mungu, kama tu vile uzazi wa Ibrahimu walivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu vile Adamu na Hawa, ambao Mungu aliwaumba hapo mwanzo, walivyoishi katika Bustani ya Edeni.

2

Kazi ya Mungu inasonga mbele kama wimbi kuu lenye nguvu. Hakuna anayeweza kumzuia, na hakuna anayeweza kusimamisha mwendo Wake. Ni wale tu wanaosikiliza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kumwonea kiu, ndio wanaoweza kufuata hatua Zake na kupokea ahadi Yake. Wale wasiofanya hivyo watakabiliwa na janga la kuangamiza na adhabu wanayostahili kabisa.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp