Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 406

16/10/2020

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima kwanza umpe Yeye moyo wako, na kuutuliza moyo wako mbele za Mungu. Ni baada tu ya kuumimina moyo wako mzima kwa Mungu ndipo unaweza kuingia hatua kwa hatua katika maisha ya kiroho yanayostahili. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa, katika kuwatumia watu, Roho Mtakatifu hatumii tu hizo sehemu zao zinazopendeza ili kufanikisha mambo, pia Anazikamilisha na kuzibadilish sehemu zao zisizopendeza. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapompa Mungu moyo wako, katika upande chanya, unaweza kupata uingiaji wa kina zaidi na ufikie kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi. Katika kigezo cha kwamba moyo wako uko shwari mbele za Mungu, jambo muhimu kama unapokea sifa kutoka kwa Roho Mtakatifu au la na kama unampendeza Mungu au la ni kama unaweza kuingia ndani kwa utendaji. Wakati Roho Mtakatifu anampa mtu nuru na anamtumia mtu, Hamfanyi hasi kamwe, lakini mara zote Humfanya aendelee kwa utendaji. Hata kama ana udhaifu, anaweza kutoishi kulingana nao, anaweza kuepukana na kuchelewesha kukuza maisha yake, naye kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu. Hiki ni kiwango. Ukiweza kufikia hili, ni thibitisho la kutosha kwamba mtu ameupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa mtu yuko hasi daima, na hata baada ya kupata nuru ili kujijua bado yuko hasi na wa kukaa tu, bila uwezo wa kusimama na kutenda pamoja na Mungu, basi aina hii ya mtu anaipokea tu neema ya Mungu, bali Roho Mtakatifu hayuko naye. Mtu akiwa hasi, hii inamaanisha kuwa moyo wake haujamgeukia Mungu na roho yake haijaguswa na Roho wa Mungu. Hii inapaswa kutambuliwa na wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp