Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 389

17/08/2020

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, ilhali hakunung’unika kamwe wala kuwa na moyo wa kulalamika, na hata Ayubu hakuwa wa kulinganishwa naye. Kwa miaka na dahari watakatifu, pia, wamekuwa wenye upungufu kuliko yeye. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu lakini pia alinijua wakati ambapo Shetani alikuwa anaendeleza njama zake za udanganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakuweza kumnyonya. Petro alitumia imani ya Ayubu, bado pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ujuzi wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba maarifa yake bado hayakuwa ya kina, na hayakuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kupata hisia ya roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua kitu cha matakwa Yangu, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama za udanganyifu za Shetani, na hivyo elimu yake ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote katika enzi.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuulizi kwamba “utoe” kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani yote, upendo na uaminifu unaozungumzia ni ndoto tu, ni povu, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, ndipo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujitoa; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa chombo cha uharibifu. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Hii ni kweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofauti tofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakujaribu kuyashika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakutumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta maarifa Yangu kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea. Katika hili, je, wao si walinipinga moja kwa moja? Maneno Yangu ni nani? Ni nani Roho Yangu? Mara nyingi Mimi Nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Ninawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na wala hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtakuwa chombo cha kuadibu Kwangu! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp