Filamu za Kikristo | Ukanaji Dini ni Nini? (Dondoo Teule)

18/09/2018

Kwenye Biblia, Paulo alisema, “Nashangaa kwamba mmejiondoa upesi hivi kwake yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kuelekea injili nyingine” (Wagalatia 1:6). Wachungaji na wazee wa kanisa huyafasiri vibaya maneno haya ya Paulo na kuwashutumu watu wote wanaoikubali injili ya kurudi kwa pili kwa Bwana Yesu, wakisema kwamba huu ungekuwa uasi wa dini na kwamba ungekuwa kumsaliti Bwana. Baadhi ya waumini hivyo basi huikosa fursa ya kumkaribisha Bwana, kwa sababu wamedanganywa. Ni dhahiri kwamba kuupata ufahamu wazi wa maana ya kweli ya maandiko haya ni muhimu sana kwa sisi kukaribisha kurudi kwa Bwana. Hivyo, ni nini maana ya kweli ya fungu hili la Maandiko? Video hii itakufichulia jibu.

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp