Wimbo wa Kusifu | Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu (Music Video)

13/04/2020

Kwa ajili ya mwanadamu Muumba anakimbia huku na kule.

Kwa kimya Anaiweka kila sekunde ya maisha Yake,

na kutoa kila kipande cha maisha Yake bila neno.

Hajui jinsi ya kuyahurumia maisha Yake mwenyewe,

lakini Anamtunza sana binadamu.

Anatoa kila kitu Alichonacho kwa binadamu huu.

Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa.

Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.

Muumba pekee ndiye anayeweza kumhurumia mwanadamu huyu

na kuthamini viumbe Wake wote.

Huruma na subira ambavyo Anatoa, bila sharti wala fikira ya thawabu,

Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake,

kupokea toleo Lake la maisha;

Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake

na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu

na kuruzuku maisha ya viumbe vyote.

Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa.

Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.

Muumba pekee ndiye anayeweza kumhurumia mwanadamu huyu

na kuthamini viumbe Wake wote.

Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu:

Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa

juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu;

Ameshukuru, amefurahia,

amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia kutokana

na kutubu na kuamini kwa binadamu;

kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote vipo juu ya na vinazungukia mwanadamu;

kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu;

uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu.

Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa.

Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.

Muumba pekee ndiye anayeweza kumhurumia mwanadamu huyu

na kuthamini viumbe Wake wote.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp