Swahili Praise and Worship Song 2020 | "Hisia za Kweli za Muumba kwa Binadamu"

Swahili Praise and Worship Song 2020 | "Hisia za Kweli za Muumba kwa Binadamu"

1511 |04/04/2020

Yafuatayo yamerekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11:

“Kisha Yehova akasema,

Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza;

ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja:

Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu,

ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua

kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto;

na pia mifugo wengi?”

Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu,

mazungumzo kati Yake na Yona.

Huku mabadilishano ya mazungumzo haya yakiwa mafupi,

yamejaa utunzaji wa Muumba kwa mwanadamu na kutotaka Kwake kukata tamaa.

Matamshi haya yanaonyesha mtazamo

na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kuhusu uumbaji Wake.

Kupitia kwa maneno haya yaliyowekwa wazi, ambayo yanasikizwa kwa nadra sana na binadamu,

Mungu anakariri nia Zake za kweli kwa binadamu.

Itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote,

kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima,

na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku.

Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu;

Fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya;

Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote.

Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya:

Mimi niko juu ya ulimwengu,

na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu.

Ninawaangalia, Ninawasubiri;

Niko kando yenu….

Mikono yake ni yenye joto na thabiti;

nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema;

Umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote;

Uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka.

Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu.

Utunzaji wake wa kujitolea na huba maalum kwa binadamu,

pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu,

vyote vilionyeshwa kwa utaratibu wakati Alipookoa mji wa Ninawi.

Haswa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona

yaliweza kuweka msingi wa huruma ya Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Aliumba.

Kupitia kwa maneno haya,

unaweza kupata ufahamu wa kina wa hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi