Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. Maana halisi ya shinda ni kushinda, kufedhehesha. Katika namna Waisraeli walivyoeleza, ni kushinda kabisa, kuharibu, na kumfanya mwanadamu kutoweza kunipinga zaidi. Lakini leo kama linavyotumika kati yenu binadamu, maana yake ni kushinda. Unapaswa kujua dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, wala kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, ina maana ya kushinda. Haijalishi kidokezo cha neno hili, kazi Yangu ni kumshinda mwanadamu. Kwa kweli mwanadamu ni kijalizo cha usimamizi Wangu, lakini kwa usahihi zaidi, mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni mwovu Anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya binadamu wote ni yenye giza na kuhuzunisha, bila ya hata ya dalili ya uwazi. Ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, na wanapoishi ndani yake hakuna anayeweza kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake na hawezi kuona jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake ni matope na imejaa mashimo makubwa, na ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Na pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Pembe zenye baridi na giza zimejaa magenge ya mapepo yaliyoshika makazi. Katika ubinadamu wote, magenge ya mapepo pia yanakuja na kwenda. Kizazi cha wanyama wengi sana waliojawa na uchafu wanapigana mkono kwa mkono, katika mapambano ya kikatili, na sauti inayosikika ni ya kuleta hofu moyoni. Wakati kama huo, katika dunia kama hiyo, na “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kujua hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa akitenda kwa mfano wa Shetani—hata kuwa na mwili wake. Wao ni ushahidi wa kuwa shahidi wa Shetani, wa uwazi. Aina hii ya Mwanadamu, uchafu kama huu, au watoto wa familia hii ya binadamu potovu, ni jinsi gani wangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Shahidi Wangu yuko wapi? Adui ambaye anasimama dhidi Yangu na kuwapotosha wanadamu tayari amewachafua wanadamu, viumbe Wangu, waliojawa na utukufu Wangu na wanaoishi kulingana na Mimi. Ameiba utukufu Wangu, na kujaza binadamu na sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alikuwa wa kugusika na mwenye umbo, na aliyejawa na uhai, aliyejawa na nguvu ya maisha, na zaidi sana, akiwa pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, pia babu wa binadamu, na hivyo watu wa uumbaji Wangu walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasilia aliumbwa kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha umbile Langu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilipaswa kuwa kiumbe Changu kilichojaa uhai Wangu, kilichojaa utukufu Wangu, kinachoonekana katika hali nzuri, kikiwa na roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee aliyejaliwa na roho ambayo ingeweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi Niliyekusudia kuumba, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe cha kuendeleza utukufu Wangu, kilichojazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo kilichojawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana halisi ya “Hawa” ilikuwa kuwa kiumbe hai, aliyepewa roho, aliye katika mwili na mifupa, kuwa ushuhuda Wangu wa pili na pia picha Yangu ya pili katika mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina yake safi na ya thamani, na awali viumbe hai wanao roho. Hata hivyo mwovu alikikanyaga na kupora kizazi cha mababu wa wanadamu, na kuufunga ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, hivi kwamba kizazi hiki hakikuamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba mwovu anapowapotosha na kuwakanyaga watu Wangu, pia kwa ukatili akachukua utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowapa watu, pumzi na maisha Niliyowapulizia ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na juhudi zote za kuchosha Nilizowekeza katika mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu Nilioweka juu yake. Wangewezaje milele kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa uumbaji? Wangewezaje kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wangewezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu na vitukuu wangeweza kumchukua vipi Mungu wa mababu zao Anayeheshimiwa kama Bwana wa uumbaji? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu utukufu kwa yule mwovu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewapa Adamu na Hawa, na maisha Niliyompa binadamu nayo ambayo wanategemea, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, na kumtuza utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani mwanadamu wa aina hii, mapepo mabaya, maiti inayotembea, takwimu za Shetani, maadui Wangu kama hao wana utukufu Wangu? Nami Nitauchukua tena utukufu Wangu, ushuhuda Wangu miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyokuwa mali Yangu, Niliyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—na kumshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu tena. Kwa sababu Ninataka kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika ushindi Wangu dhidi ya Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kitu cha starehe Yangu. Hii ndiyo nia Yangu.

Mwanadamu ameendelea kwa maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia walipo leo. Hata hivyo, wanadamu wa uumbaji Wangu wa awali kwa muda mrefu uliopita wameshazama katika upotovu. Tayari wao wamecha kuwa kile Nilichotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, tayari ni wasiostahili jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, walioporwa na Shetani, na ni maiti mbovu zinazotembea ambamo Shetani anaishi na Shetani kuvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuwasili Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki katika furaha ya maisha na huzuni kwa kweli pamoja na Mimi. Kama vile binadamu wanavyoniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, na kusaliti namna yao ya kujidekeza kwa madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, wala ule wa nia Yangu leo. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote—siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote anayeniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yako Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—na hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—hivyo katika siku zinazokaribia za moto, utapata mateso zaidi kuliko ya Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kali zaidi kuliko ya wale viongozi 250 waliompinga Musa, na mateso zaidi kuliko Sodoma chini ya moto mkali wakati wa uharibifu wake. Musa alipougonga mwamba, na maji aliyokuwa Ameyatoa Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza muziki wa sifa Kwangu, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake wote kote milimani, akapoteza mali yenye thamani kwa familia yake, na mwili wake kujawa na majipu, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Watu wanaojulikana kama wa taifa la Mataifa walipopokea ufunuo Wangu, walipojua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na neno Langu kali na hivyo kufarijiwa na kuokolewa wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu na kupitia mateso, je si pia wanakabiliwa na kukataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, waliokimbia mateso ya majaribu, si wao wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale na pasipo na pahali pa kupumzika, wala pasiwe na neno Langu la kufutia machozi. Ingawa kuadibu Kwangu na usafishaji hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wanatangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kupata tabasamu dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka kuadibu Kwangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kama maficho ya utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nawashauri: ni heri kutumia nusu ya maisha yako Kwangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kutakuwa na faida gani ya wewe kujipenda sana mpaka kiwango cha kuikimbia kuadibu Kwangu? Utafaidi nini ukijificha kutoka kwa kuadibu Kwangu kwa muda mfupi tu, na mwishowe upate aibu ya milele, na kuadibu kwa milele? Mimi, kwa hakika, Sitamlazimisha yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yako inazidi ile ya Tomaso, basi imani yako itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wako utapata furaha Yangu, na wewe hakika utapata utukufu Wangu katika siku zako. Hata hivyo watu, wanaoamini katika dunia na wanaomwamini shetani, wamefanya mioyo yao kuwa migumu, kama vile halaiki za mji wa Sodoma, chembe za mchanga zikivuma katika macho yao na sadaka za Shetani zikiwa zimeshikiliwa vinywani mwao. Nyoyo zao zilizodanganywa kwa muda mrefu uliopita zimemilikiwa na yule mwovu aliyekuwa ameipora dunia, na karibu mawazo yao yote yameporwa na pepo za kale. Kwa hivyo imani ya mwanadamu imekwenda na upepo, na wao hawawezi hata kuitambua Kazi Yangu. Wanachoweza kufanya ni kuvumilia tu au kuchambua kwa kukisia sana, kwa sababu wao tayari wamejawa na sumu ya Shetani.

Mimi Nitamshinda mwanadamu kwa sababu waliumbwa na Mimi wakati mmoja na pia, kilicho cha ziada, walifurahia vitu vyote karimu vya uumbaji Wangu. Hata hivyo, wamenikataa Mimi, na nyoyo zao haziko na Mimi ndani yao, na wao huniona kama mzigo maishani mwao, hadi kwa kiwango ambacho, wakiwa kwa kweli wameniona, watu bado wananikataa, na wanawaza kila njia inayoweza kuwawezesha kunishinda Mimi. Watu huwa hawaniruhusu Mimi kuwachukulia kwa umakini au kuweka madai kali juu yao, wala kukubali hukumu au kuadibu Kwangu wa udhalimu wao. Hawaoni kuchukuliwa kwa namna hiyo kuwa ya kuvutia, lakini badala yake, wanaona ni kama kero kwao. Hivyo Kazi Yangu ni kushinda mwanadamu ambaye anakula, anakunywa kwa ajili Yangu na kusherehekea Kwangu, lakini hanijui. Nitawapokonya zana wanadamu, na kisha, Nitarejea kwenye makao Yangu pamoja na malaika Wangu na utukufu Wangu. Kwa kuwa tabia ya watu imenivunja moyo kabisa na kuitawanya kazi Yangu kwa vipande muda mrefu uliopita. Nataka kuumiliki tena utukufu uliokuwa umeibwa na yule mwovu kabla ya kuondoka kwa furaha, na kuwaacha wanadamu waendelee na maisha yao, waendelee na “maisha na kazi yao kwa amani,” waendelee “kulima mashamba yao,” wawe huru kutokana na kuingilia kati Kwangu katika maisha yao. Lakini Mimi sasa kwa ukamilifu Nitaumiliki tena utukufu Wangu kutoka kwa mkono wa yule mwovu, niurejeshe ukamilifu wa utukufu Niliouumba ndani ya mwanadamu wakati wa kuumbwa kwa dunia, na kamwe tena sitauweka juu ya mwanadamu wa dunia. Kwa kuwa binadamu hawajashindwa tu kuuhifadhi utukufu Wangu, bali pia wao wameugeuza kuwa mfano wa Shetani. Watu hawathamini kuwasili Kwangu, wala hawangetuza siku za utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kukubali kwa kuadibu Kwangu, wala kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, na wao bado huvaa tabasamu zao za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambao wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuondoka miongoni mwao, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui kuwa wakati utukufu Wangu ulitoweka kutoka Israeli kulikuwa na huzuni nyingi, kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani. Je, umesahau kwamba wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kupitia mateso hayo? Huu ndio wakati ambao utaweza kuuona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo utashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katika giza wakati utukufu Wangu unaondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapita katika nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp