Waovu Lazima Waadhibiwe

Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Jinsi mnavyozidi kukubali maneno ya Mungu wakati huu, ndivyo mnavyozidi kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo mnavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake. Haya ndiyo maagizo ya Mungu kenu na kile mnapaswa kufikia. Mkitumia dhana kupima na kufafanua kwa Mungu kwa maneno, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika Bibilia, na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu katika mioyo yao, Wayahudi wa Agano la Kale walimtazama Mungu kama sanamu wa udongo, kana kwamba Mungu anaweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee anayeitwa Masihi ndiye Mungu, na kwa sababu walitumikia na kumwabudu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (kisicho na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—wakimhukumu Yesu Asiyekuwa na hatia kwa kifo. Mungu hajatenda uhalifu wowote, ilhali mwanadamu hakumsamehe Mungu, na kumhukumu Yeye kifo bila kusita. Na ndivyo Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habalidiliki na humfafanua kulingana na Bibilia, kana kwamba mwanadamu ameona ndani ya usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha pakubwa, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, Bado Nasema kwamba bado humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili ya Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hajui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi na kwa sababu badala ya kufuata ukweli, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kutoka kwenye chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine msalabani na mwanadamu. Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu Amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejifahamu. Wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao na watoto wao, kazi zao, matarajio, hali katika jamii, majivuno na pesa, kwa sababu ya nguo, kwa sababu ya chakula na mwili—matendo ya nani kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao matendo yao ni kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni wangapi wanaotenda matendo yasiyo kwa maslahi yao? Ni wangapi wasiobagua na kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hali yao? Ndivyo Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, mahakimu katili wasiohesabika wamemhukumu Mungu na mara nyingine wakamsulubisha msalabani. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu kwa ukweli wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu?

Mbele za Mungu, je, ni rahisi vile kufanywa mtu mkamilifu, mtakatifu au mwenye haki? Ni ukweli kwamba, “hakuna wenye haki katika dunia hii, wenye haki hawapo katika dunia hii.” Mkija mbele za Mungu, fikiria kile mnachovaa, tafakarini juu ya neno lolote na pia matendo yako, juu ya fikira zenu na mawazo na hata ndoto mnazoota kila siku—zote ni kwa manufaa yenu. Je, hivi sivyo hali halisi ilivyo? “Haki” haimaanishi kutoa sadaka wala haimaanishi kumpenda jirani yako vile unavyojipenda na hakumaanishi kutopigana, kutogombana, kutoiba ama kutonyang’anya. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama kazi yako na kuiheshimu mipango na mipangilio ya Mungu kama wito utokao mbinguni, bila kujali wakati ama mahali, kama tu yote Bwana Yesu Alivyofanya. Hiyo ndiyo haki iliyozungumziwa na Mungu. Kwamba Lutu aliitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kujali alichopata ama kupoteza; alichotenda katika huo wakati kinaweza kuitwa haki, lakini hawezi kuitwa mwanadamu mwenye haki. Ilikuwa tu kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndipo akatoa wasichana wake wawili badala ya malaika. Lakini sio tabia yake yote ya hapo awali inaashiria haki, na ndivyo Nasema kwamba “hakuna wenye haki katika dunia hii.” Hata katika wale ambao wako katika mkondo wa urejesho, hakuna hata mmoja anayeweza kuitwa mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri vipi, haijalishi jinsi unavyooneka kulisifu jina la Mungu, kutowapiga ama kuwalaani wengine, ama kuiba na kunyang’anya kutoka kwa watu, huwezi kuitwa mwenye haki bado, kwa sababu vitu hivyo vinaweza kumilikiwa na mtu yeyote aliye wa kawaida. Siku ya leo, kilicho muhimu ni kwamba wewe humfahamu Mungu. Inaweza kusemekana leo tu kwamba uko na ubinadamu wa kawaida kiasi kidogo tu, ilhali hauna haki iliyozungumziwa na Mungu, na hakuna utakachotenda kitakachokuwa ushuhudawa ufahamu wako wa Mungu.

Hapo awali, Mungu Alipokuwa mbinguni, mwanadamu alijaribu kumdanganya Mungu kwa matendo yake; leo, Mungu Amekuja miongoni mwa mwanadamu —hakuna anayejua ni kwa muda upi—ilhali mwanadamu bado anapitia mizunguko kwa ajili ya Mungu, na kujaribu kumdanganya Mungu. Je, mwanadamu yuko nyuma kwa fikira zake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angewadanganya ndugu zake, na hata Yesu alipokuja, bado hakubadilika; hakuwa na maarifa yoyote ya Yesu, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, ilikuwa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hamumfahamu Mungu, basi utakuwa Yuda, na msiba wa tanzia ya usulubishaji wa Yesu katika Enzi ya Neema, maelfu ya miaka iliyopita, utarudiwa tena. Je, hamuyaamini hayo? Ni ukweli mtupu! Siku hizi watu wanatoka katika hali hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema—na watu wa aina hii wanachukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi bila kujali, bali ni kulingana na ukweli—na unapaswa kuamini. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila kidimbwi cha maji yanayonuka. Sasa, wengi katika kanisa wako vile. Mnafikiri Sijui lolote; leo, Roho Wangu ananiongoza na kunitolea ushuhuda. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, mnafikiri Sielewi fikira zenu za ujanja katika nyoyo zenu na vitu vilivyowekwa katika nyoyo zenu? Je, Mungu hudanganywa kwa njia rahisi vile? Je unafikiri kwamba unaweza kumtendea vile unavyotaka? Hapo zamani Nilikuwa na wasiwasi kwamba mlikuwa mmefungwa, na hivyo Nikaendelea kuwapa uhuru, lakini hakuna aliyetambua kuwa Nilikuwa mzuri kwao. Niliwapa inchi moja na wakachukua maili. Ulizana wenyewe kwa wenyewe: Sijajishughulika na yeyote, na Sijakuwa na haraka ya kumkaripia yeyote—ilhali Sina tashwishi juu ya motisha na dhana za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe ambaye Mungu Anamtolea ushuhuda ni mjinga? Iwapo ni hivyo basi Nitasema wewe ni kipofu sana. Sitakulaumu, na basi wacha tuone utakavyopotoka. Hebu tuone iwapo ujanja wako utakuokoa, ama iwapo kujaribu uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi yasiyo muhimu, na sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako, buu kama wewe hufai kuchukua muda wa Mungu Akikushugulikia—kwa hivyo wacha tuone kiwango utakachojiendekeza. Watu kama hao hawafuati ufahamu wa Mungu hata kidogo, na hawana upendo wowote kwa Mungu, ilhali wanataka kuitwa wenye haki na Mungu—je huu si utani? Kwa sababu kuna idadi ndogo ya watu walio waaminifu, Mimi sijishughulishi na kingine ila kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile kilichohitajika kukamilika leo, na baadaye, adhabu italetwa kwa kila mmoja kulingana na tabia yake. Nimesema kile Ninachopaswa kusema, kwa sababu hii ndio kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile Ninachopaswa kufanya, ila Sifanyi Nisichopaswa kufanya, ilhali Natumai kwamba utatumia muda mwingi kwa kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako wa Mungu ni wa kweli? Je wewe ni mmoja wa wale ambao wamemsulubisha Yesu msalabani tena? Mwisho, Ninasema hivi: Ole wao wamsulubishao Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp