Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima: Tamko la Kumi na Mbili

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya. Tena, ni kama wanyama wakitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu wakikimbilia usalama katika mapango ya milimani; ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wana laani siku waliozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kueleza; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kuenda mara moja yasionekane tena. Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kueleza kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa jivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya pekee katika makao ya joka kubwa jekundu, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa falme Zangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma milele kuwepo kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi. Joka kubwa jekundu limetumia njia zote za kuweza kufikiriwa ili kuvuruga mpango Wangu, akitumaini kufuta kazi Yangu duniani, lakini Naweza kukata tamaa kwa sababu ya mbinu zake za udanganyifu? Naweza kutishwa hadi kukosa kujiamini na vitisho vyake? Hakujawahi kuwa na kiumbe hata mmoja mbinguni ama duniani ambaye Simshiki katika kiganja cha mkono Wangu; ni kiwango gani zaidi ambacho huu ni ukweli kuhusu joka kuu jekundu, chombo hiki kinachotumika kama foili[a] Kwangu? Je, pia si kitu cha kutawaliwa na mikono Yangu?

Katika wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu alifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua akaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kuwa na yeyote ambaye ameuona uso Wangu, ambaye ameona umeme Mashariki; sembuse yule ambaye amesikia sauti inayotoka kwa kiti Changu cha enzi? Kwa kweli, kutoka siku za zamani, hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye amewasiliana na nafsi Yangu moja kwa moja; leo tu, wakati Nimekuja duniani, ndipo wanadamu wana nafasi ya kuniona. Lakini hata sasa, wanadamu bado hawanifahamu, jinsi wanavyouangalia uso Wangu na kuisikia tu sauti Yangu, lakini bila kuelewa Ninachomaanisha. Wanadamu wote wako hivi. Ukiwa mmoja wa watu Wangu, je huhisi fahari ya kina unapoona uso Wangu? Na je, huhisi aibu kwa sababu hunifahamu? Natembea kati ya wanadamu, na Naishi kati ya wanadamu, kwani Nimekuwa mwili na Nimekuja katika ulimwengu wa binadamu. Lengo Langu sio tu kuuwezesha binadamu kuutazamia mwili Wangu; cha maana zaidi, ni kuuwezesha binadamu kunifahamu Mimi. Zaidi, kupitia mwili Wangu uliopatwa, Nitauona binadamu na hatia kwa sababu ya dhambi zake; kupitia mwili Wangu uliopatwa, Nitashinda joka kuu jekundu na kuondoa pango lake.

Ingawa wanadamu ambao wanajaza dunia ni wengi kama nyota, Nawajua wote wazi kama Ninavyotazama kiganja cha mkono Wangu mwenyewe. Na, ingawa wanadamu ambao “wananipenda” ni wengi pia kama mchanga wa bahari, ni wachache tu ndio waliochaguliwa na Mimi: wale tu wanaotafuta mwanga unaong’aa, walio kando na wale “wanaonipenda.” Sithamini mno mwanadamu, wala Sikadiri upungufu wake; ila, Ninamwekea mwanadamu mahitaji kulingana na sifa zake za kiasili, na hivyo kile Ninachohitaji ni aina ya mwanadamu anayenitafuta kwa dhati—hii ni kwa ajili ya kufikia lengo Langu katika kuwachagua wanadamu. Kuna wanyama wa porini wasiohesabika milimani, lakini wote ni wapole kama kondoo mbele Zangu; mafumbo yasiyoeleweka yako chini ya bahari, lakini yanajiwakilisha Kwangu wazi kama vitu vyote vilivyo katika uso wa dunia; katika mbingu juu kuna ulimwengu ambao mwanadamu hawezi kufikia kamwe, ilhali Natembeatembea katika malimwengu hayo yasiofikika. Mwanadamu hajawahi kunifahamu katika mwanga, lakini ameniona tu katika ulimwengu wa giza. Huko katika hali sawa kabisa na hiyo leo? Ilikuwa katika kilele cha ghasia ya joka kuu jekundu ndipo Nilivaa kirasmi mwili ili kufanya kazi Yangu. Ulikuwa wakati ambapo joka kuu jekundu lilifichuliwa maumbile yake ya kweli kwa mara ya kwanza ndipo Nilipokuwa na ushuhuda kwa jina Langu. Nilipotembea katika barabara za binadamu, hakuna kiumbe hata mmoja, hata mtu mmoja, aliyebumburushwa hadi kuamka, kwa hivyo Nilipokuwa mwili katika ulimwengu wa mwanadamu, hakuna aliyejua. Lakini wakati, Nikiwa katika mwili Wangu ulipotwa, Nilianza kufanya kazi Yangu, halafu binadamu ukaamka, ulibumburushwa kutoka kwa ndoto zake na sauti Yangu ya radi, na kutoka wakati huu ukaanza maisha chini ya uongozi Wangu. Kati ya watu Wangu, Nimeanza tena kwa mara nyingine kazi mpya. Baada ya kusema kuwa kazi Yangu katika dunia haijaisha, hii inatosha kuthibitisha kuwa wale watu ambao Nilizungumza kuwahusu hapo awali sio wale Niliodhani Nawahitaji, lakini hata hivyo bado Ninahesabu waliochaguliwa kati ya watu hawa. Kutoka kwa hili, inakuwa dhahiri kwamba Nafanya haya sio tu kuwawezesha watu Wangu kujua Mungu mwenye mwili, bali pia kuwatakasa watu Wangu. Kwa sababu ya ukali wa amri Zangu za utawala, watu wengi bado wako katika hatari ya kuondolewa na Mimi. Isipokuwa ukifanya juhudi zote kujishughulikia, kuushinda mwili wako mwenyewe, isipokuwa ukifanya haya, utakuwa bila shaka kitu Ninachodharau na kukataa, cha kutupwa chini kuzimu, kama jinsi Paulo alivyopokea adabu moja kwa moja kutoka kwa mikono Yangu, ambapo hakukuwa na kutoroka kutoka hapo. Je pengine umegundua kitu kutoka kwa maneno Yangu? Kama hapo awali, bado ni nia Yangu kulitakasa kanisa, kuendelea kuwatakasa watu Ninaohitaji, kwani Mimi ni Mungu Mwenyewe, ambaye ni mtakatifu na safi kikamilifu. Nitafanya hekalu Langu lisiwe tu yenye rangi aina tofouti na rangi za upinde wa mvua, lakini pia liwe na usafi usiokuwa na doa, na ndani kufanane na nje yake. Katika uwepo Wangu, lazima nyote mfikirie nyuma kuhusu kile ambacho mmefanya hapo awali, na kuamua kama leo, mnaweza kuamua kunipa utoshelezo kamili katika moyo Wangu.

Sio tu kwamba mwanadamu hanifahamu Mimi katika mwili Wangu; kwa kuzidisha ubaya, ameshindwa kuielewa nafsi yake mwenyewe inayoishi katika mwili. Imekuwa miaka mingapi, na wakati huu wote, wanadamu wamenidanganya, wakinichukua kama mgeni kutoka nje? Ni mara ngapi wamenifungia nje ya mlango wao? Ni mara ngapi, hawajakuwa makini Kwangu wakisimama mbele Yangu? Ni mara ngapi wamenikataa miongoni mwa wanadamu wengine? Ni mara ngapi wamenikana mbele za Shetani? Ni mara ngapi wanenishambulia na midomo yao ya kugombanagombana? Ilhali siweki rekodi ya unyonge wa mwanadamu, wala kwa sababu ya kutotii kwake Sijataka kulipiza kisasi. Yote Nimetenda ni kuweka dawa kwa magonjwa yake, ili kutibu magonjwa yake yasiyotibika, hivyo kumrudisha kwa afya, ili mwishowe aje kunifahamu Mimi. Yote Nimetenda si kwa ajili ya kuishi kwa binadamu, kwa ajili ya kuupa binadamu fursa ya maisha? Mara nyingi Nilikuja katika ulimwengu wa wanadamu, lakini wanadamu, kwa sababu Nilikuja Mimi Mwenyewe katika dunia, hawakujishughulisha nami; badala yake, kila mmoja aliendelea na shughuli zake, akijitafutia njia ya kutoka. Ila hawajui kuwa kila moja ya barabara chini ya mbingu inatoka kwa mikono Yangu! Ila hawajui kuwa kila kitu kilichoko chini ya mbingu kinakabiliwa na uratibu Wangu! Yupi kati yenu anathubutu kuhifadhi chuki katika moyo wake? Yupi kati yenu anathubutu kwa urahisi kufikia makubaliano? Nimekuwa Nikiendelea na kazi Yangu kwa kimya miongoni mwa binadamu, ni hayo tu. Kama, katika wakati wa kupata mwili Kwangu, Singekuwa Nimejali kuhusu udhaifu wa ubinadamu, basi binadamu wote, kwa sababu ya kupata Kwangu mwili, wangetishwa kabisa, na kwa sababu hiyo, ungeingia kuzimu. Ni kwa sababu tu Nilinyenyekea na kujificha mbali ndiyo binadamu umeepuka janga, ukapata ukombozi kutoka kwa adabu Yangu, na kwa namna hii ukafika leo. Ukizingatia ilivyokuwa vigumu kufika leo, je, si ni heri uihifadhi kwa upendo mkubwa sana kesho ambayo haijafika bado?

Machi 8, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp