Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima: Tamko la Tano

Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu? Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia za aibu, pia, bila mantiki yoyote! Wakati mmoja au mwingine, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu! Je, hili ni jambo ambalo binadamu ana uwezo wa kufanya? Iwapo hakungekuwa na kitu kilichobakia katika nia na malengo yako, ungekuwa tayari umeshika njia tofauti. Je, unafikiri kuwa Sijui ni kiasi gani moyo wa binadamu unaweza kustahimili? Kuanzia wakati huu kuendelea, katika mambo yote lazima ujiweke katika ukweli wa mazoezi; kupiga tu domo, kama ulivyokuwa ukifanya, hakutakusaidia. Katika siku zilizopita, wengi wenu mlifaulu kudoea chini ya paa Langu; Kwa sababu ya ukali wa maneno Yangu, wewe umeweza kusimama imara mpaka leo. Je, unafikiri kwamba maneno Yangu huzungumzwa tu kiholela bila sababu? Haiwezekani! Mimi huangalia chini juu ya mambo yote kutoka juu, na Ninatoa mamlaka juu ya mambo yote kutoka juu. Kwa njia iyo hiyo, Nimeutuma wokovu Wangu juu ya dunia. Kamwe hakuna wakati ambapo Mimi Sitazami, kutoka mahali Pangu pa siri, kila hatua ya binadamu, kila wanachosema na kutenda. Binadamu Kwangu ni kama kitabu kilicho wazi: Mimi Nawaona na kuwajua kila mmoja. Mahali hapo pa siri ni makaazi Yangu, na mbingu ndiyo kitanda ambamo Mimi hujilaza. Jeshi la shetani haliwezi kunifikia, kwa maana Mimi nimejawa na ukuu, haki na hukumu. Siri isiyoelezeka imo katika maneno Yangu. Wakati Naongea, unakuwa kama ndege waliotupwa majini, wakazidiwa na kuchanganyikiwa, au watoto ambao wamepatwa na hofu hivi karibuni, wakionekana kutojua lolote, kwa sababu roho yako imeingia katika hali ya mshangao. Kwa nini Nasema kwamba mahali pa siri ni makaazi Yangu? Je, unajua maana ya ndani ya yale Ninayosema? Ni nani katika binadamu wote ana uwezo wa kunijua Mimi? Nani ana uwezo wa kunijua Mimi kama vile anavyomjua baba yake na mama yake? Ninapopumzika katika makaazi Yangu, Mimi huchunguza kwa karibu: Watu wote duniani wamo katika pilka pilka, “kusafiri duniani kote” na kukimbia huku na kule, yote kwa ajili ya hatima yao, maisha yao ya baadaye. Lakini hakuna hata mmoja anayeweka nguvu yake kwa ajili ya kujenga ufalme Wangu, hata nguvu kiasi cha ile mtu anayotumia kuvuta pumzi. Mimi Niliumba wanadamu, na Nimewaokoa mara nyingi kutoka katika dhiki, lakini hawa binadamu ni wasio na shukrani wote: Hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeweza kuhesabu matukio yote ya wokovu Wangu. Imekuwa miaka mingapi, zimekuwa karne ngapi tangu kuumbwa kwa dunia mpaka wa leo, na ni miujiza ngapi Niliyofanya, mara ngapi Nimeweka wazi hekima Yangu? Lakini mwanadamu, kama mwendawazimu anayeteseka na shida ya akili na kiwewe au, wakati mwingine kama kongoni anayeputa huku na kule katika msitu, hana nia hata kidogo ya kuyajali mambo Yangu. Mara nyingi Nimempa mwanadamu hukumu ya kifo na kumhukumu afe, lakini mpango wa usimamizi wa kazi Yangu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Kwa hivyo mwanadamu bado yuko katika mikono Yangu, akiegemea vile vitu vya kale alivyokwamilia. Kwa sababu ya hatua za kazi zangu, mimi, kwa mara nyingine tena, Nimewaokoeni, ninyi viumbe mliozaliwa katika familia kubwa zenye ufisadi, uozo, uchafu, na aibu.

Kazi Niliyopanga inaendelea kusonga mbele bila kukoma hata kwa muda kidogo. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme, na baada ya kukuweka katika ufalme Wangu kama watu Wangu, Nitakuwa na madai mengine ya kuweka dhidi yako; Hiyo ni kusema, Nitaanza kutangaza rasmi na kueneza mbele yako katiba ambayo Nitatumia kuongoza enzi hii:

Kwa sababu mnaitwa watu Wangu, mnapaswa kuwa na uwezo wa kulitukuza jina Langu, kumaanisha, kusimama katika ushuhuda wakati wa majaribio. Mtu yeyote akijaribu kunidanganya na kunificha ukweli, au kushiriki katika shughuli zisizo za heshima nyuma Yangu, bila ubaguzi Nitamfukuza nje, aondolewe kutoka kwa nyumba Yangu awe akisubiri hukumu. Wale ambao hawajakuwa waaminifu na watiifu Kwangu katika siku za mbeleni, na leo hii wanainuka na kunihukumu hadharani, wao pia watafukuzwa kutoka kwa nyumba Yangu. Wale ambao ni watu Wangu lazima wajali kuhusu mizigo Yangu kila mara na vile vile kutafuta kujua maneno Yangu. Ni watu kama hawa tu ndio Nitakaowapa nuru, na wao kwa hakika wataishi chini ya uongozi Wangu na kupata nuru, na kamwe hawatakutana na kuadibu. Wale ambao, kwa kutojali mizigo Yangu, wanamakinika na mipango ya hatima yao wenyewe, yaani, wale ambao hawalengi kwa matendo yao kukidhi Moyo Wangu bali wanataka kuomba omba vya bure, viumbe hawa wanaofanana na waombaji, Ninakataa kata kata kuwatumia, kwa sababu tangu walipozaliwa hawajui chochote kuhusu maana ya kujali mizigo Yangu. Wao ni watu wenye akili isiyokuwa ya kawaida; watu kama hawa wanaugua kutokana na “utapiamlo” wa ubongo, na wanastahili kwenda nyumbani wapate “lishe.” Siwahitaji watu wa aina hii. Miongoni mwa watu Wangu, kila mtu atatakiwa kuzingatia kuwa kunijua ni wajibu unaotakiwa kutekelezwa mpaka mwisho, kama kula, kuvaa, na kulala, mambo ambayo mtu kamwe hawezi kusahau hata kwa muda mfupi, ili kwamba mwishowe kunijua litakuwa jambo la kawaida kama vile kula, jambo ambalo wewe hufanya bila jitihada yoyote, kwa mkono uliozoea. Kuhusu maneno Ninayoyanena, Kila neno lazima lichukuliwe kwa uhakika mkubwa na lichukuliwe kikamilifu; hakuwezi kuwa na hatua nusu za uzembe katika kutimiliza haya. Mtu asiyekuwa makini na maneno Yangu ataonekana kama ananipinga Mimi kwa uwazi; mtu yeyote asiyeyala maneno Yangu, au hatafuti kuyajua, ataonekana kama ambaye hanizingatii, na bila kusita atafagiliwa nje ya mlango wa nyumba Yangu. Kwa maana, kama Nilivyosema zamani, Ninachotaka sio watu wengi ila wateule wachache. Kati ya watu mia, kama mmoja tu ataweza kunijua kupitia maneno Yangu, basi bila kusita Ningewatupilia mbali wengine wote ili Nizingatie kumpa nuru na kumweka katika mwanga mmoja huyu. Kutokana na hili unaweza kuona kuwa si mbali na ukweli kwamba idadi kubwa pekee ndio inaweza kunidhihirisha, kuishi kwa maisha ya Kimungu. Ninachotaka ni ngano (hata ingawa viini vya mbegu havijajaa) na sio vigugu mwitu (hata kama viini vyake vimejaa vya kutosha na ni vya kutamanika). Na kwa wale wasiojali kuhusu kutafuta lakini badala yake kuwa na tabia za kuzembea, wanapaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe; Mimi sitaki kuwaona tena, wasije wakaleta aibu kwa jina Langu. Kuhusu yale Ninayohitaji kutoka kwa watu Wangu, Nitakomea katika maagizo hayo kwa sasa, na Nitasubiri kuweka vikwazo zaidi kulingana na jinsi mabadiliko ya hali yatakavyokuwa.

Katika siku zilizopita, idadi kubwa ya watu walifikiri Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye hekima, kwamba mimi ndiye Nilikuwa Mungu aliyeona ndani kwa kina ya mioyo ya watu; lakini yote yalikuwa maneno ya juu juu tu. Kama mwanadamu angenijua kwa kweli, hangedhania na kurukia mambo bila kuzingatia kikamilifu, ila angezidi kujaribu kuendelea kunijua kupitia maneno Yangu. Wakati tu alifika katika hatua ambapo kweli angepata kuona matendo Yangu, ndipo angestahili kusema kwamba Nilikuwa mwenye busara, kwamba Mimi ni wa ajabu. Ufahamu wako kunihusu ni mdogo mno. Katika enzi zote, ni watu wangapi wamenihudumia na kwa miaka mingapi, baada ya kuona matendo Yangu, wakaja kujua kwa hakika kitu kunihusu; na basi daima wakawa na moyo wa unyenyekevu Kwangu, na kutokuwa na nia hata kidogo ya upinzani Kwangu, kwa sababu ni vigumu jinsi gani kutafuta nyayo Zangu. Kama uongozi Wangu ungekosekana miongoni mwa watu hawa, hawangethubutu kutenda bila kufikiria, na hivyo, baada ya kuishi kwa uzoefu wa miaka mingi, hatimaye walijumlisha sehemu ya ufahamu kunihusu, wakisema kwamba Mimi ni wa Hekima, wa Ajabu na Mshauri, kwamba maneno Yangu ni kama upanga wenye makali pande mbili, kwamba matendo Yangu ni makuu, ya kustaajabisha, na kupendeza, kwamba Mimi Nimevikwa adhama, kwamba hekima Yangu inafika juu kuliko anga, na ufahamu mwingine. Lakini leo wewe unanijua tu kwa misingi ambayo wao walitengeneza, kwa hivyo idadi kubwa kati yenu, kama walivyo kasuku, mnayarudia tu maneno waliyosema. Ni kwa sababu Mimi huzingatia jinsi ufahamu wako Kwangu ni mdogo na udogo wa “elimu” yako ndio maana Nimekusamehe kuadibu kwingi. Lakini hata hivyo, idadi kubwa kati yenu bado hawajijui wenyewe, au unafikiri tayari ushayafikia mapenzi Yangu katika matendo yako, na kwa sababu hii umeepuka hukumu. Au unafikiri kwamba, baada ya kuwa na mwili, Nimekosa kujua kabisa mwelekeo wa matendo ya mwanadamu, na kwa sababu hii pia umeepuka kuadibu. Ama unafikiri kwamba Mungu unayemwamini hayuko katika maeneo yote ya ulimwengu, na kwa hivyo umeweka kumjua Mungu kama shughuli ya kufanya wakati huna shughuli nyingine badala ya kuweka kumjua Mungu katika moyo wako kama wajibu ambao lazima utekelezwe, na kutumia imani katika Mungu kama njia ya kuchangamsha wakati ambao labda ungetumiwa kwa kuzembea. Kama Singeuonea huruma ukosefu wako wa sifa za kustahili, mantiki, na ufahamu, basi nyote mngeangamia katika kuadibu Kwangu, na kutoweka kabisa ulimwenguni. Lakini hadi wakati Kazi Yangu hapa duniani itamalizika, Mimi Nitabaki mwenye huruma kwa mwanadamu. Hili ni jambo ambalo lazima nyote mlijue. Komeni kuyachanganya mazuri na mabaya.

Februari 25, 1992

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?