Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo yote husika na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kwa kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inapozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopotoka pakubwa na kudanganywa kabisa ndiyo shabaha ya aina hii ya hukumu. Binadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa kitambo na hajui kwamba kuna mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na bila shaka hajui kwamba yeye mwenyewe anang’ang’ana kwenye lindi kuu la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja ulimwenguni leo na anatafuta kundi la watu waliopotoka ambao Anaweza kuokoa? Hata baada ya binadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua ya mawe katili inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Kama isingekuwa ya kuhukumu watu hivi, kusingekuwa na matokeo yoyote na haingewezekana kabisa kuwaokoa watu dhidi ya janga la umaskini. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha maozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.

Miili yenu, matamanio yenu ya kupita kiasi, ulafi wenu, na ashiki yenu vyote vimekita mizizi ndani yenu. Mambo haya yanaidhibiti sana mioyo yenu kiasi kwamba hamna nguvu za kutupa huo utumwa wa mawazo hayo ya kikabaila na yaliyooza. Hamtamani kubadilisha hali yenu ya sasa, wala kuukimbia ushawishi wa giza. Mmefanywa kuwa watumwa tu wa mambo hayo. Hata kama mnajua kwamba maisha kama hayo ni yenye maumivu sana na kwamba ulimwengu kama huo ni wenye giza la kupindukia, bado, hakuna hata mmoja wenu anao ujasiri wa kubadilisha maisha ya aina hii. Mnatamani tu kutoroka aina hii ya maisha halisi, kuondoa nafsi zenu kutoka kwenye mahali pa mateso ya muda na kuishi katika mazingira yenye amani, furaha na yafananayo na mbinguni. Hamko radhi kuvumilia magumu ili kuweza kubadilisha maisha yenu ya sasa; vilevile hamko radhi kutafuta ndani ya hukumu hii na kuadibu huku maisha ambayo mnafaa kuyaishi. Badala yake, mnaziota ndoto zisizo na uhalisi kabisa kuhusu ulimwengu mzuri wa nje ya miili yenu. Maisha mnayotamani ni yale mnayoweza kupata kwa urahisi bila kupata maumivu yoyote. Hayo si ya kihalisi kamwe! Kwa sababu kile mnachotumainia si kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana katika mwili na kupata ukweli kwenye harakati ya maisha yenu, yaani, kuishi kwa ajili ya ukweli na kutetea haki. Haya siyo yale maisha ambayo mngedhani ni ya kupendeza, kusisimua. Mnahisi kwamba haya hayatakuwa maisha yanayovutia au ya maana. Kwenu nyinyi, kuishi maisha kama hayo kutakuwa ni kujidhalilisha! Hata Ingawa mnakubali kuadibu huku leo, hata hivyo kile mnachofuatilia si kupata ule ukweli au kuishi ukweli katika wakati wa sasa, bali kuweza kuingia katika maisha yenye furaha nje ya miili yenu baadaye. Hamtafuti ukweli wala hamtetei ukweli, wala hamtetei ukweli na bila shaka hampo kwa ajili ya kweli. Hamtafuti kuingia leo, lakini kila wakati mnafikiria siku ijapo ambapo mtaangalia kwenye mbingu ya samawati na kudondokwa na machozi machungu, huku mkitarajia kuchukuliwa kuenda mbinguni. Je, hamjui kwamba kufikiria huku kama kwenu tayari kumeondokwa na uhalisi? Mnaendelea kufikiria kwamba Mwokozi mwenye upole na huruma isiyoisha bila shaka atakuja siku moja kukuchukua pamoja na Yeye, wewe ambaye umevumilia ugumu na mateso ulimwenguni humu, na kwamba Yeye bila shaka atalipiza kisasi kwa ajili yako wewe ambaye umedhalilishwa na kunyanyaswa. Je, si kweli kwamba umejaa dhambi? Wewe pekee ndiwe ambaye umeteseka ulimwenguni humu? Umeanguka katika utawala wa Shetani wewe mwenyewe na kuteseka, na bado unahitaji Mungu kukulipizia kisasi? Wale wasioweza kutosheleza mahitaji ya Mungu—kwani wao wote si adui wa Mungu? Wale wasioamini katika Mungu mwenye mwili—kwani wao si wapinga Kristo? Matendo yako mazuri yana maana gani? Yanaweza kuchukua nafasi ya moyo unaoabudu Mungu? Huwezi kupokea baraka za Mungu kwa kufanya baadhi ya matendo mazuri tu, naye Mungu hatakulipizia kisasi yale mabaya uliyofanyiwa kwa sababu tu umeonewa na kukandamizwa. Wale wanaomwamini Mungu ilhali hawamjui Mungu, lakini wanaofanya matendo mazuri—kwani wao nao hawaadibiwi pia? Unamwamini Mungu tu, unataka Mungu akushughulikie na Akulipizie kisasi tu kwa mabaya uliofanyiwa wewe, na unataka Mungu kukupa njia ya kimbilio kutoka kwa umaskini wako. Lakini unakataa kutilia maanani ukweli; wala hutamani kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Sembuse, huwezi kuyakimbia maisha haya magumu na yasiyo na maana. Badala yake, huku ukiishi maisha yako katika mwili na maisha yako ya dhambi, unamwangalia Mungu kwa matarajio ya kusahihisha manung’uniko yako na kuondoa ukungu wa kuwepo kwako. Haya yanawezekanaje? Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unayo maisha, unaweza kufurahia baraka za Mungu. Wale walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka za Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani. Kunawezaje kuwa na wema miongoni mwa wale wasiopenda ukweli? Kunawezaje kuwa na haki miongoni mwa wale wanaopenda mwili tu? Si kweli kwamba haki na wema vyote vinarejelea ukweli? Si kweli kwamba vyote hivi vimehifadhiwa wale wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote? Wale wasiopenda ukweli na ambao ni maiti zinazooza—je, watu hawa wote huwa hawajaficha maovu? Wale wasioweza kuishi ukweli—hawa wote si adui wa ukweli? Na je ninyi?

Kama unaweza kutoroka ushawishi huu wa giza na kujitenga na mambo hayo machafu, kama unaweza kuwa mtakatifu, inamaanisha kwamba unao ukweli ndani yako. Si kwamba maumbile yako yamebadilika, lakini kilichopo ni kwamba unaweza tu kubadilisha ukweli ule kuwa matendo na unaweza kuunyima mwili wako. Haya ndiyo yanayopatikana kwa wale waliotakaswa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kuwatakasa binadamu ili binadamu aweze kuwa na ukweli, kwa sababu binadamu kwa sasa anao ukweli mdogo sana! Kufanya kazi ya kushinda kwa watu hawa ni jambo la umuhimu mkubwa mno. Nyote mmeanguka katika ushawishi wa giza na mmeumizwa mno. Shabaha ya kazi hii, basi, ni kuwawezesha kujua maumbile ya binadamu na hivyo basi kuishi kwa ukweli. Kufanywa kuwa mtimilifu ni kitu ambacho viumbe vyote vinafaa kukubali. Kama kazi ya awamu hii inahusu tu kufanya watu kuwa watimilifu, basi inaweza kufanywa Uingereza, au Amerika, au Israeli; inaweza kufanywa kwa watu wa taifa lolote. Lakini kazi ya kushinda ni yaupambanuzi. Hatua ya kwanza ya kazi ya kushinda ni ya mudamfupi; aidha, itatumika kudhalilisha Shetani na kuushinda ulimwengu mzima. Hii ndiyo kazi ya mwanzo ya kushinda. Mtu anaweza kusema kwamba kiumbe chochote kinachomwamini Mungu kinaweza kufanywa kuwa kiimilifu kwa sababu kufanywa kuwa mtimilifu ni kitu ambacho mtu anaweza kufikia tu baada ya mabadiliko ya muda mrefu. Lakini kushindwa ni tofauti. Mfano wa kushinda ndio ambao lazima ni yule anayebaki nyuma kabisa, akiishi kwenye giza lile totoro kabisa, na vilevile ndiye aliyedhalilishwa, na asiyekuwa radhi kumkubali Mungu, na asiyetii Mungu kabisa. Huyu ndiye aina ya mtu anayeweza kutoa ushuhuda wa kushindwa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kumshinda Shetani. Shabaha kuu ya kufanya watu kuwa watimilifu, kwa upande mwingine, ni kuwapata watu wale. Ni kuwawezesha watu kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa kwamba kazi ya kushinda imefanywa hapa, kwa watu kama ninyi. Lengo ni kuwafanya watu kutoa ushuhuda baada ya kushindwa. Watu hawa walioshindwa watatumika kufikia shabaha ya kudhalilisha Shetani. Kwa hivyo, mbinu kuu ya ushindi ni gani? Kuadibu, hukumu, kutupilia mbali laana, na kufichua—kwa kutumia tabia ya wenye haki katika kuwashinda watu ili waweze kushawishika kabisa, kujawa na imanikatika mioyo yao na vinywa vyao kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu. Ili kutumia uhalisi wa neno na kutumia mamlaka ya neno ili kuwashinda watu na kuwashawishi kabisa—hivi ndivyo ilivyo kushindwa. Wale waliofanywa kuwa watimilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa na kubadilisha tabia yao. Wanamjua Mungu, wamepitia njia ya Mungu mwenye upendo, na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo mapenzi yao wenyewe. Wale waliofanywa kuwa watimilifu ni wale walio na uelewa halisi wa ukweli kutokana na kuwa na ukweli ulio na uzoefu. Wale walioshindwa ni wale walio na ukweli lakini hawajakubali maana halisi ya ukweli. Baada ya kushindwa, wanatii, lakini utiifu wao unatokana na hukumu waliopokea. Hawana uelewa kabisa wa hali halisi ya ukweli mwingi. Wanautambua ukweli kwa matamshi, lakini bado hawajaanza kuonyesha ukweli; wanauelewa ukweli, lakini hawajapitia ule ukweli. Kazi inayofanywa kwa wale wanaofanywa kuwa watimilifu inajumuisha kuadibiwa na kuhukumiwa, pamoja na toleo la maisha. Mtu anayethamini kuonyesha ukweli ni mtu wa kufanywa kuwa mtimilifu. Tofauti kati ya wale watakaofanywa kuwa watimilifu na wale walioshindwa inapatikana katika hoja kama wataendeleza ukweli huu. Wale wanaouelewa ukweli, wameanza kuonyesha ukweli, na wanauishi ukweli huo ndio wale waliofanywa kuwa watimilifu; wale wasioelewa ukweli, hawauingii ukweli, yani, wale wasioishi ukweli, ni watu wasioweza kufanywa watimilifu. Watu kama hao wanaweza sasa kutii kabisa, basi wameshindwa. Kama wale walioshindwa hawatatafuta ukweli—kama watafuata tu lakini wasiishi kwa ukweli, kama wataushuhudia na kuusikia ukweli lakini wakakosa kuthamini kuishi kwa ukweli—hawawezi kufanywa kuwa watimilifu. Wale wa kufanywa kuwa watimilifu wanaendeleza ukweli kulingana na njia ya kuwa watimilifu, yani wanaendeleza ukweli kutokana na njia ya kuwa watimilifu. Kupitia haya, wanatimiza mapenzi ya Mungu, na wanapata kufanywa kuwa watimilifu. Yeyote anayefuata hadi mwisho kabla ya kazi hiyo ya ushindi kuhitimishwa ni mshinde, lakini hawezi kusemekana kuwa ndiye aliyefanywa kuwa mtimilifu. Kufanywa kuwa watimilifu kunarejelea wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kufaidika kutoka kwa Mungu. Kunaashiria wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanasimama imara katika majaribio na wanaishi kwa kudhihirisha ukweli. Kile kinachotofautisha kushindwa na kufanywa kuwa mtimilifu ni zile tofauti kwenye hatua za kufanya kazi na tofauti katika kiwango ambacho ukweli unashikiliwa. Wale wote ambao hawajaanza kushughulikia njia ya kuwa watimilifu, kumaanisha wale wasio na ukweli, kwa hakika wataishia kuondolewa kabisa. Ni wale tu walio na ukweli na wanaoishi ukweli wanaoweza kumilikiwa kabisa na Mungu. Yani, wale wanaoishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro ndio wanaofanywa kuwa watimilifu, huku wengine wote ndio wameshindwa. Kazi inayofanywa kwa wale wote wanaoshindwa inajumuisha tu uwekwaji laana, adibu, na kuonyesha hasira, na kile kinachowapata vyote vinahusu tu uadilifu na laana. Kushughulikia mtu kama huyo ni kufichua waziwazi—kufichua tabia potoshi iliyo ndani yake ili aweze kujitambua na kushawishika kabisa. Punde binadamu anapokuwa mtiifu kabisa, kazi ya ushindi inakamilika. Hata kama wingi wa watu wangali wanatafuta ukweli, kazi ya ushindi itakuwa imekamilika.

Kunao mpangilio wa kutimizwa kama itabidi ufanywe kuwa mtimilifu. Kupitia kwa utatuzi wako, ustahimilivu wako, na dhamiri yako, na kupitia ufuatiliaji wako, utaweza kupitia maisha na kutimiza mapenzi ya Mungu. Haya ndiyo kuingia kwako na kile kinachohitajika kwenye njia ya kuwa mtimilifu. Kazi ya kuwa mtimilifu inaweza kufanywa kwa watu wote. Yeyote anamyetafuta Mungu anaweza kufanywa kuwa mtimilifu na anayo fursa na sifa za kufanywa kuwa mtimilifu. Hakuna sheria ngumu na ya haraka hapo. Kufanywa kuwa mtimilifu kimsingi kunategemea kile ambacho mtu hutafuta. Watu wanaopenda ukweli na walio na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli bila shaka wanaweza kufanywa kuwa watimilifu. Na watu wasiopenda ukweli na hawatajwi na Mungu hawamiliki maisha ambayo Mungu anataka. Watu hawa hawawezi kufanywa kuwa timilifu. Kazi ya kufanywa kuwa mtimilifu ni kwa minajili tu ya kuwamiliki watu, na wala si hatua ya kupigana na Shetani; kazi ya ushindi ipo tu kwa minajili ya kupigana na Shetani, kumaanisha kwamba kutumia ushindi kwa binadamu ili kumshinda Shetani. Sehemu hii ya nyuma ndiyo kazi kuu, kazi mpya zaidi ambayo haijawahi kufanywa katika enzi zote. Mtu anaweza kusema kwamba shabaha ya awamu hii ya kazi kimsingi ni kuwashinda watu wote ili kuweza kumshinda Shetani. Kazi ya kufanya watu kuwa watimilifu—hiyo si kazi mpya. Kazi yote katika kipindi hiki ambapo Mungu anafanya katika kwa mwili inayo shabaha lake kuu katika ushindi wa watu. Hii ni sawa na ile Enzi ya Neema. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubishwa ndiyo iliyokuwa kazi kuu. “Kuwapata watu” kulikuwa nyongeza katika kazi ya mwili na kulifanywa tu baada ya kusulubishwa. Wakati Yesu alipokuja na kufanya kazi Yake, shabaha Yake ilikuwa kimsingi kutumia kusulubishwa Kwake katika kushinda uchungu na utumwa wa kifo na Kuzimu, kuweza kushinda ushawishi wa Shetani, kumaanisha kumshinda Shetani. Ilikuwa tu baada ya kusulubishwa kwa Yesu ndipo Petro alipoanza hatua kwa hatua kushika njia ya kuwa utimilifu. Bila shaka alikuwa miongoni mwa wale waliomfuata Yesu wakati Yesu alipokuwa akifanya kazi, lakini hakufanywa kuwa mtimilifu wakati huo. Badala yake, ilikuwa ni baada ya Yesu kumaliza kazi Yake ndipo Petro alipoanza kuelewa taratibu ukweli wa mambo na kisha akafanywa kuwa mtimilifu. Mungu mwenye mwili na huja ulimwenguni tu kukamilisha awamu muhimu na ya kipekee ya kazi kwenye kipindi kifupi cha muda, na wala si kuishi kwa kipindi kirefu miongoni mwa watu hapa ulimwenguni na kuwa na kusudio la kuwafanya kuwa watimilifu. Huwa hafanyi kazi hiyo. Hasubirii mpaka wakati ule ambao binadamu amefanywa kuwa mtimilifu kabisa ili kuhitimisha kazi Yake. Hiyo siyo shabaha na umuhimu wa kupata mwili Kwake. Yeye huja tu ili kufanya kazi ya kipindi kifupi ya kuwaokoa binadamu, na wala si kufanya ile kazi ya kipindi kirefu sana ya kuwafanya binadamu kuwa watimilifu. Kazi ya kuwaokoa binadamu ni wakilishi, inayoweza kuzindua enzi mpya na inaweza kukamilishwa kwenye kipindi kifupi cha muda. Lakini kuwafanya binadamu kuwa watimilifu kunahitaji kuwaleta binadamu hadi kiwango fulani na ni kazi inayoweza kuchukua muda mrefu. Kazi hii lazima ifanywe na Roho wa Mungu, lakini inafanywa kwa msingi wa ukweli unaozungumzwa wakati wa kazi Yake akiwa mwili. Au aidha huwainua mitume kufanya kazi ya uchungaji ya kipindi kirefu, ili kufikia shabaha yake ya kuwafanya binadamu kuwa watimilifu. Mungu mwenye mwili hafanyi kazi hii. Huongea tu kuhusu njia ya maisha ili watu waweze kuelewa na kuwapatia tu binadamu ukweli, badala ya kuandamana na binadamu bila kusita katika kuendeleza ukweli kwani kufanya hivyo hakumo ndani ya huduma Yake. Kwa hivyo Hatakuwa akiandamana na binadamu mpaka siku ile ambayo binadamu ataelewa kabisa ukweli na kupata kung’amua kabisa ukweli. Kazi Yake akiwa mwili inahitimishwa wakati binadamu anapoingia rasmi kwenye njia iliyo sawa ya ukweli wa maisha, wakati binadamu anapoingia kwenye njia iliyo sawa ya kufanywa kuwa mtimilifu. Hapa, bila shaka ndipo pia ambapo atakuwa Ameshinda Shetani kabisa na kuutawala ulimwengu. Hajali kama binadamu ameingia kimsingi kwenye ukweli wakati huo, wala kujali kuhusu kama maisha ya binadamu ni makubwa au madogo. Vyote hivi si vile ambavyo Yeye akiwa katika mwili anafaa kusimamia; vyote hivi havimo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili. Punde anakapomaliza kazi aliyonuia, huhitimisha kazi Yake katika mwili. Kwa hiyo, kazi ambayo Mungu mwenye mwili anafanya ni kazi ile tu ambayo Roho wa Bwana hawezi kufanya moja kwa moja. Aidha, ni ile kazi ya wokovu ya kipindi kifupi, na wala si kazi ya kipindi kirefu hapa ulimwenguni.

Kuinua ubora wa tabia zenu hakumo ndani ya himaya ya kazi Yangu. Ninawaomba kufanya hivi tu kwa sababu ubora wa tabia yako uko chini sana. Kwa ukweli hii si sehemu ya kazi ya kuwa mtimilifu; badala yake, ni kazi ya ziada mnayofanyiwa. Kazi inayokamilishwa kwenu leo inafanywa kulingana na vile unavyohitaji. Imebinafsishwa, na wala si njia fulani inayofaa kutembelewa na kila mtu ambaye anafanywa kuwa mtimilifu. Kwa sababu ubora wa tabia zenu uko chini zaidi kuliko yeyote yule aliyefanywa kuwa mtimilifu kitambo, kazi hii, inapokuja kwako, inashughulikiwa kwa vizuizi vingi. Nimo miongoni mwenu mnaofanya kazi hii ya ziada kwa sababu vilengwa vya kuwa watimilifu ni tofauti. Kwa kawaida wakati Mungu anapokuja ulimwenguni, Anaishi ndani ya mipaka myembamba ili kutekeleza kazi Yake, bila kubugudhi na kusumbua sana shughuli nyingine. Hahusiki katika masuala ya familia au kushiriki katika maisha ya watu. Hajali chochote kabisa na hajishughulishi na mambo hayo madogomadogo; yote haya si sehemu ya huduma Yake. Lakini ubora wako wa tabia uko chini zaidi kuliko vile Nilivyohitaji—hakuna ulinganifu kamwe—kiasi cha kwamba unachangia changamoto kubwa katika kazi. Aidha, kazi hii lazima ifanywe miongoni mwa watu katika nchi hii ambayo ni Uchina. Hamjapata elimu sana kiasi cha kwamba Sina chaguo lolote ila kuamuru kwamba muweze kupata elimu. Nimewaambieni kwamba hii ni kazi ya ziada, lakini pia ni kitu ambacho lazima muwe nacho, kitu kinachowafaidi nyinyi katika kufanywa kuwa mtimilifu. Kwa hakika, mnafaa kupata elimu, maarifa ya kimsingi kuhusu mienendo yenu binafsi, na maarifa ya kimsingi kuhusu maisha yaliyo mbele yenu; Sifai kuwazungumzia kuhusu mambo haya. Lakini kwa sababu hamna mambo haya, Sina chaguo jingine ila kufanya kazi ya kuyaongezea mambo haya kwenu baada ya ukweli. Hata kama mnashiriki dhana nyingi kunihusu, bado Ninahitaji hiki kutoka kwenu, bado nahitaji kwamba muweze hadhi yenu. Si nia Yangu kuja na kufanya kazi hii, kwa sababu kazi Yangu ni kuwashinda tu, ili kuweza kupata imani yenu kamili kwa kuwahukumu nyinyi, hivyo basi kupambanua njia ya maisha mnayofaa kuishi. Nikisema kwa njia nyingine, vile ambavyo mmeelimika na kama mna maarifa kuhusu maisha visingenihusu Mimi kamwe kama isingekuwa kwamba Nahitaji kuwashinda kwa neno Langu. Vyote hivi vinaongezewa ili kuhakikisha kuwa matokeo yanapatikana kutoka kwenye kazi ya ushindi na kwa minajili ya kufanywa kwenu kuwa watimilifu kutakakofuata. Si hatua ya kazi ya ushindi. Kwa sababu ubora wenu wa tabia ni wa hali ya chini, na nyie ni wazembe, na wenye mapuuza, na wajinga, na wasio na maono, na wasio na mipango yoyote, na wenye upumbavu—kwa sababu nyie mmekithiri mipaka ya kutokuwa wenye akili razini—nahitaji kwanza muinue ubora wenu wa tabia. Yeyote anayetaka kufanywa mtimilifu lazima atimize mpangilio fulani. Ili kufanywa kuwa mtimilifu, lazima mtu awe na akili razini na yenye umakinifu na lazima awe radhi kuishi maisha yenye maana. Kama wewe ni mtu usiyekuwa radhi kuishi maisha yasiyo wazi, wewe si mtu anayetafuta ukweli, mtu aliye mwaminifu katika kila kitu anachofanya, na mtu aliye na ubinadamu wa kawaida wa kipekee, basi wewe umefuzu kufanywa kuwa mtimilifu.

Kazi hii miongoni mwenu inatekelezwa kwenu kulingana na ile kazi inayohitajika kufanywa. Baada ya ushindi wa watu hawa binafsi, kundi la watu litafanywa kuwa timilifu. Kwa hivyo, wingi wa kazi ya sasa umo katika matayarisho ya shabaha ya kuwafanya kuwa watimilifu, kwa sababu wapo wengi sana wanaohitaji kuupata ukweli na ambao wanaweza kufanywa kuwa watimilifu. Kama kazi ya ushindi itatekelezwa kwenu na baadaye hakuna kazi ya ziada itakayofanywa, basi si ni kweli kwamba baadhi ya wale wanaotamani ukweli hawataupata? Kazi ya sasa inalenga kufungua njia ya kuwafanya watu kuwa watimilifu baadaye. Ingawa kazi Yangu ni ya ushindi tu, njia ya maisha iliyotamkwa na Mimi bila shaka ni katika matayarisho ya kuwafanya watu kuwa watimilifu baadaye. Kazi inayokuja baada ya ushindi inatilia maanani kuwafanya watu kuwa watimilifu, na hivyo basi ushindi unafanywa ili kuweka msingi wa kule kufanywa kuwa watimilifu. Binadamu anaweza kufanywa kuwa mtimilifu tu baada ya kushindwa. Sasa hivi kazi kuu ni kushinda; baadaye wale wanaotafuta na kutamani ukweli watafanywa kuwa watimilifu. Kufanywa kuwa mtimilifu kunahusisha dhana nzuri za watu kuhusu maisha: Je, unao moyo unaopenda Mungu? Kina cha yale umepitia ulipotembea kwenye njia hii ni kipi? Upendo wako katika Mungu ni safi vipi? Mwenendo wako wa ukweli ni mpevu kiasi kipi? Ili kufanywa kuwa mtimilifu, lazima mtu awe na maarifa ya kimsingi ya dhana zote za ubinadamu. Hili ni hitaji la kimsingi. Wale wote wasioweza kufanywa kuwa watimilifu baada ya kushindwa hugeuka na kuwa vifaa vya kuhudumu na hatimaye bado watatupwa kwenye ziwa la moto na kibiriti na bado wataanguka kwenye lile shimo lisilokuwa na mwisho kwa sababu ya tabia yao ambayo haijabadilika na wangali watakuwa wa Shetani. Kama mtu atakosa sifa za kufuzu za kuwa mtimilifu, basi yeye ni bure bilashi—hana manufaa, ni chombo, kitu ambacho hakiwezi kustahimili majaribio ya moto! Upendo wako kwa Mungu sasa hivi ni mkubwa vipi? Chukizo lako kwa nafsi yako ni kubwa kiasi kipi? Unamjua Shetani kwa mapana yapi? Umelegeza uamuzi wenu? Maisha yenu katika ubinadamu yamethibitiwa vyema? Maisha yenu yamebadilika? Unayaishi maisha mapya? Mtazamo wenu wa maisha umebadilika? Kama mambo haya hayajabadilika, huwezi kufanywa kuwa mtimilifu hata kama hutabadilisha mwenendo; badala yake, wewe umeshindwa tu. Wakati ukifika wa kukujaribu, unakosa ukweli, ubinadamu wako si wa kawaida, na wewe ni wa kiwango cha chini kama mnyama. Umeshindwa tu, wewe ndiwe umeshindwa tu na Mimi. Kama vile tu, punde punda anapopitia mjeledi wa mmiliki wake, yeye huwa na woga na wasiwasi wa kufanya chochote kila wakati anapomwona bwana wake, ndivyo pia, wewe ulivyo kama punda huyo aliyeshindwa. Kama mtu atakosa vipengele hivyo vizuri na badala yake yeye ni wa kutoonyesha hisia na mwenye wasiwasi, mwepesi kutishwa na wa kusitasita katika mambo yote, asiyeweza kutambua chochote kwa njia iliyo wazi, asiyeweza kukubali ukweli, ambaye bado hana njia ya kuendeleza mwenendo wake, na hata zaidi asiye na moyo wa upendo wa Mungu—kama mtu hana uelewa wa namna ya kumpenda Mungu, namna ya kuishi maisha yenye maana, au namna ya kuwa mtu halisi—mtu kama huyu anawezaje kumshuhudia Mungu? Hii inaonyesha kwamba maisha yako yanayo thamani ndogo na wewe si kingine ila punda aliyeshindwa. Wewe umeshindwa, lakini hilo linamaanisha tu kwamba umelikataa lile joka kubwa jekundu na umekataa kunyenyekea katika uwanja wake; hiyo inamaanisha kwamba wewe unaamini kuwa kunaye Mungu, unataka kutii mipango yote ya Mungu na huna malalamiko yoyote. Lakini je, dhana zile ni nzuri? Uwezo wa maisha ya kudhihirisha neno la Mungu, uwezo wa kumdhihirisha Mungu—huna vyote hivi, kumaanisha bado hujamilikiwa na Mungu, na kwamba wewe si mwengine ila punda aliyeshindwa. Hakuna chochote cha kutamanika ndani yako, na Roho Mtakatifu hayumo kazini ndani yako. Ubinadamu wako unakosa mengi na haiwezekani Mungu kukutumia. Lazima uidhinishwe na Mungu na kuwa mara mia moja bora zaidi kuliko wanyama wale wasioamini na kuliko wale wanaotembea wakiwa wamekufa—wale tu wanaofikia kiwango hiki ndio wanaofuzu kufanywa kuwa watimilifu. Pale tu ambapo mtu anao wema na utu na dhamiri ndipo anapofaa kutumiwa na Mungu. Pale ambapo tu mnafanywa kuwa watimilifu ndipo mtakapochukuliwa kuwa binadamu. Wale waliofanywa kuwa watimilifu tu ndio wale wanaoishi maisha yenye maana. Watu kama hawa tu ndio wanaoweza kushuhudia hata vizuri zaidi kuhusu Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp