Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache. Je, si hili linakurudisha nyuma? Kuna zaidi katika kuingia kwa njia nzuri dhahiri na vitendo ambavyo mnapaswa kuving’amua, na vilevile unapaswa kuelewa mambo kadha katika maono ya kazi Yake kama vile umuhimu wa kazi Yake ya ushindi, njia ya kufanywa mkamilifu katika siku za usoni, kinachofaa kupatikana kupitia uzoefu wa majaribu na masaibu, umuhimu wa hukumu na kuadibu, kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na kanuni za ukamilifu na ushindi. Huu wote ndio ukweli wa maono. Hayo mengine ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme pamoja na ushuhuda wa baadaye. Huu pia ni ukweli kuhusiana na maono, na ni wa msingi na muhimu sana pia. Kwa sasa, kuna mengi sana mnayopaswa kujihusisha nayo na kutenda, na kwa sasa yana safu nyingi na maelezo ya kina. Kama huna ufahamu wa ukweli huu, ni thibitisho kwamba bado hujaingia. Mara nyingi, ufahamu wa mwanadamu kuhusu ukweli huwa wa juujuu; mwanadamu hushindwa kuweka ukweli wa kimsingi katika vitendo na hajui jinsi ya kushughulikia hata maswala madogo. Kwa sababu ya tabia yake ya uasi, mwanadamu hushindwa kutenda ukweli, na ufahamu wake kuhusu kazi ya sasa ni wa juu juu na wa kuegemea upande mmoja. Kwa hivyo, si kazi rahisi kwa mwanadamu kufanywa mkamilifu. Uasi wako ni wa hali ya juu, na unashikilia sana hali yako ya zamani; umeshindwa kusimama katika upande wa ukweli, na umeshindwa kutenda hata ukweli ulio wazi. Wanadamu kama hao ndio ambao hawawezi kukombolewa na ni wale ambao hawajashindwa. Ikiwa kuingia kwako hakuna kina au malengo, kukua kwako kutakujia polepole. Ikiwa kuingia kwako hakuna uhalisi hata kidogo, basi kazi yako itakuwa bure. Ikiwa hujui kiini cha ukweli, hutabadilishwa. Ukuaji katika maisha ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia zake hupatikana kwa kuwa ndani ya ukweli na, zaidi ya hili, kwa kuwa katika tajriba ya kina. Ukiwa na tajriba pana katika wakati wa kuingia kwako, na ukiwa na ufahamu halisi kuhusu kuingia, tabia yako itabadilika haraka. Hata kama kwa sasa hujapata nuru katika vitendo, unafaa angalau uwe na nuru ya maono ya kazi. La sivyo utashindwa kuingia, na hutaweza kufanya hivyo isipokuwa uufahamu ukweli. Ni baada ya kuangaziwa nuru na Roho Mtakatifu katika tajriba yako ndipo utakapopata ufahamu wa kina kuhusu ukweli na uingie kwa kina. Ni sharti uifahamu kazi ya Mungu.

Baada ya uumbaji wa mwanadamu hapo mwanzoni, Waisraeli ndio waliokuwa kielelezo cha kazi, na Israeli nzima ilikuwa ngome ya kazi ya Yehova duniani. Kazi ya Yehova ilikuwa imwongoze mwanadamu moja kwa moja na kumchunga kwa kuweka wazi sheria ili kwamba mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida na kumwabudu Yehova kwa njia ya kawaida duniani. Katika Enzi ya Sheria Mungu alikuwa Asiyeonekana wala kuguswa na mwanadamu. Alikuwa tu Anawaongoza wanadamu waliokuwa mwanzo wamepotoshwa na Shetani, na Alikuwepo kuwaagiza na kuwaongoza wanadamu, kwa hivyo maneno yote Aliyoyanena yalikuwa ya kisheria, amri na uelewa wa kawaida wa kuishi maisha kama mwanadamu, na wala sio kuhusu ukweli unaomruzuku mwanadamu. Waisraeli chini ya uongozi Wake hawakuwa wale waliopotoshwa zaidi na Shetani. Kazi yake ya kisheria ilikuwa tu hatua ya kwanza kabisa katika kazi ya ukombozi, mwanzo hasa wa kazi ya wokovu, na haikuwa inahusiana kamwe na mabadiliko katika tabia za kimaisha za mwanadamu. Kwa hivyo, mwanzoni mwa kazi ya ukombozi hapakuwa na haja Kwake kuwa katika mwili kwa ajili ya kazi Yake katika Israeli. Ndiyo maana Alihitaji kiungo, yaani, chombo ambacho kwacho Angemfikia mwanadamu. Kwa hivyo kukazuka miongoni mwa viumbe waliozungumza na kufanya kazi kwa niaba ya Yehova, na hivi ndivyo wana wa wanadamu na manabii walikuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Wana wa wanadamu walifanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa niaba ya Yehova. Ili waitwe na Yeye inamaanisha kuwa hao watu walipanga sheria kwa niaba ya Yehova na walikuwa miongoni mwa watu wa Israeli; na watu kama hao walikuwa makasisi walioangaliwa na kulindwa na Yehova, na Roho wa Yehova alifanya kazi ndani yao; walikuwa viongozi miongoni mwa wanadamu na wahudumu wa Yehova wa moja kwa moja. Manabii kwa upande mwingine ndio waliokuwa na jukumu la kunena na mataifa na makabila yote kwa niaba ya Yehova. Ndio vilevile waliotoa unabii kuhusu kazi ya Yehova. Wote wanadamu na manabii walikuzwa na Roho wa Yehova Mwenyewe na walikuwa na kazi ya Yehova ndani yao. Miongoni mwa wanadamu, walikuwa ndio wale waliomwakilisha Yehova moja kwa moja; walifanya kazi tu kwa kuwa waliinuliwa na Yehova wala si kwa kuwa walikuwa miili ambamo Roho mtakatifu Mwenyewe alikuwa kapata mwili. Kwa hivyo, ingawa wao walifanya kazi na kuongea kwa niaba ya Mungu, hao wana wa mwanadamu na manabii wa Enzi ya Sheria hawakuwa mwili wa Mungu mwenye mwili. Hii ilikuwa kinyume kabisa katika Enzi ya Neema na hatua ya mwisho, kwani kazi ya ukombozi na hukumu ya mwanadamu vilifanywa na Mungu katika mwili Mwenyewe, na hapakuwa na haja ya kukuza manabii na wanadamu kufanya kazi kwa niaba Yake. Machoni pa mwanadamu, hamna tofauti kubwa kati ya kiini na mbinu za kazi zao. Ni kwa sababu hii mwanadamu anachanganya kati ya kazi ya Mungu kuwa mwili na ile ya manabii na wanadamu. Kimsingi, umbo la Mungu mwenye mwili lilikuwa sawa na lile la manabii na wanadamu. Mungu kuwa mwili alikuwa wa kawaida na halisi zaidi kuliko manabii. Kwa hivyo mwanadamu anashindwa kabisa kuwatofautisha. Mwanadamu huangazia umbile peke yake bila kugundua kuwa japo wote hufanya kazi na kuongea, kuna tofauti kubwa kati yao. Kwa sababu uwezo wa mwanadamu wa kung’amua ni duni, mwanadamu anashindwa kung’amua mambo ya kimsingi na hata zaidi hawezi kubainisha kitu changamano. Maneno na kazi za manabii na za wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu zote zilikuwa zinafanya wajibu wa mwanadamu, kufanya jukumu lake kama kiumbe na kufanya ambacho mwanadamu anapaswa kufanya. Hata hivyo, maneno na kazi za Mungu mwenye mwili ilikuwa ni kuendeleza huduma Yake. Japo umbile Lake lilikuwa lile la kiumbe, kazi Yake haikuwa kutimiza majukumu Yake bali Huduma Yake. Dhana “wajibu” inarejelea viumbe ilhali “huduma” inarejelea mwili wa Mungu mwenye mwili. Kuna tofauti kubwa kati ya haya mawili, na haya mawili hayabadilishani nafasi. Kazi ya mwanadamu ni kufanya wajibu wake, ilhali kazi ya Mungu ni kusimamia, na kuendeleza huduma Yake. Kwa hivyo, japo mitume wengi walitumiwa na Roho Mtakatifu na manabii wengi wakajazwa Naye, kazi zao na maneno yao yalikuwa tu kutimiza wajibu wao kama viumbe. Japo unabii wao ungeweza kuwa mkubwa kuliko maisha kama yanavyozungumziwa na Mungu mwenye mwili, na hata ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu kuliko wa Mungu kuwa mwenye mwili, walikuwa bado wanafanya wajibu wao na wala si kutimiza huduma yao. Wajibu wa mwanadamu unarejelea majukumu yake, na ni kitu kinachoweza kupatwa kwa mwanadamu. Hata hivyo, huduma ifanywayo na Mungu mwenye mwili inahusiana na usimamizi Wake, na haiwezi kupatikana kwa mwanadamu. Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu kuwa mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa nafsi asili ya Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu kuwa mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo Mungu ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake.

Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa kumhudumia Mungu, hupunguzwa taratibu jinsi uzoefu wake uongezekapo na namna ya uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake asili, na badala yake huzembea na kupitia katika mizunguko, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wana mengi ya kumshukuria, lakini wanageuka na kumkong’ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha Naye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Ikiwa mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo ndipo tu atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa dhati, na ni mwanadamu kama huyu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kufanywa mkamilifu na Mungu. Na wengi wenu je? Mnamchukuliaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje majukumu yenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, si mmepokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyatathimini haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna hisia mbovu kunihusu na mko shingo upande. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe kamwe? Mnawezaje kuitwa kiumbe? Je, hamtambui wazi mnachopaswa kuonyesha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno na kazi Yangu, malipo yenu yatakuwa adhabu. Kamwe hamtapata neema, baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia! Hao watu wapumbavu na mafidhuli hawajafanya kila wawezalo wala kutimiza wajibu wao tu, bali wameinyosha mikono yao wakitaka neema, kana kwamba wanastahili wanachoitisha. Na iwapo watashindwa kupata wanachokiomba, wanakuwa wakosa imani zaidi. Watu kama hawa wataitwaje wastaarabu? Ninyi ni sampuli mbaya isiyokuwa na urazini, isiyoweza kabisa kutimiza wajibu mnaotakiwa kutimiza wakati wa kazi ya usimamizi. Thamani yenu imeshuka pakubwa. Kwa kutonilipa kwa kuwaonea imani tayari ni tendo la uasi mkuu litoshalo kuwahukumu na kuthibitisha uoga, uovu, uzembe na uduni wenu. Mnawezaje kuendelea kustahili kunyoosha mikono yenu? Mmeshindwa kuwa hata msaada kidogo kwa kazi Yangu, mmeshindwa kuahidi imani yenu, na mmeshindwa kunitolea ushuhuda. Tayari haya ni makosa na kushindwa kwenu, na bado mnanivamia, mnanisemea uongo na kulalama kuwa Mimi si mwenye haki. Je, huu ndio uaminifu wenu? Haya ndiyo mapenzi yenu? Ni kazi gani nyingine mnayoweza kufanya zaidi ya hii? Mmechangia vipi katika kazi yote ambayo imeishafanywa? Mmegharamia kiasi gani? Ni huruma kubwa kwamba bado Sijawawekea lawama, na bado mnanipa visingizio na kulalama faraghani kunihusu. Kweli mna hata chembe ndogo ya ubinadamu? Japo wajibu wa mwanadamu umetiwa doa na fikira za mwanadamu na mitazamo yake, ni sharti ufanye wajibu wako na kuwa mwaminifu kwa imani yako. Unajisi katika kazi ya mwanadamu ni suala la hulka yake, ilhali, ikiwa mwanadamu hafanyi wajibu wake, unajisi huu unaonyesha uasi wake. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndiko huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Wacha niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hupitia mijadala tu katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika vitendo vya ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao. Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi ya mtu na athari inazoacha kwa mwanadamu. Unabii uliotolewa na Isaya wakati ule, haukuongeza kitu katika uzima wa mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angelifanya hiyo kazi, kwani haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Yeye Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika upeo wa kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kwa upande mwingine, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hii ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huu ulikuwa mwazo wa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu Alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyopewa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke yake, wala hata Mungu kuwa mwili hafahamu yote; unaweza kuthibitisha kama Yeye ni Mungu[a] kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye Ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu katika mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu. Isaya, Danieli na wengine wote walikuwa ni watu walioelimika na kustaarabika vilivyo; walikuwa watu wa kipekee chini ya uongozi wa Yehova. Mwili wa Mungu mwenye mwili pia ulikuwa na utambuzi na haukupungukiwa na akili ila ubinadamu wake ulikuwa wa kawaida. Alikuwa mwanadamu wa kawaida na jicho la mwanadamu lisingeweza kubaini ubinadamu wowote wa pekee kumhusu au kugundua kitu chochote katika ubinadamu Wake tofauti na wa wale wengine. Kamwe hakuwa kabisa wa kimiujiza au wa kipekee na hakuwa na elimu ya juu, ujuzi au nadharia kupita kiasi. Maisha Aliyoyazungumzia na mienendo yake hakuipata kinadharia, kielimu, kitajriba au kupitia malezi ya kifamilia. Badala yake, ilikuwa kazi ya moja kwa moja kutoka kwa Roho pamoja na uungu kuwa mwili. Ni kwa kuwa mwanadamu ana dhana kuu kumhusu Mungu, na hasa kwa kuwa fikira hizi hutungwa kutokana na vipengele vingi visivyo yakini na kimiujiza hivi kwamba, katika macho ya mwanadamu, Mungu wa kawaida mwenye udhaifu wa kibinadamu, ambaye hawezi kutenda miujiza, kwa hakika si Mungu. Je, si hizi ni fikra potovu za mwanadamu? Mwili wa Mungu mwenye mwili usingekuwa wa kawaida, basi ingesemekanaje kwamba Alipata mwili? Kupata mwili ni kuwa wa kawaida; mwanadamu wa kawaida; Iwapo angekuwa wa kupita uwezo wa binadamu, basi Asingeweza kuwa wa kimwili. Kuthibitisha kuwa Yeye ni wa kimwili, Mungu kuwa mwili alihitaji kuwa na mwili wa kawaida. Hili lilikusudiwa kutimiza umuhimu wa kupata mwili. Hata hivyo, mambo hayakuwa hivyo kwa manabii na wanadamu. Manabii walikuwa wanadamu waliopewa vipawa na kutumiwa na Roho Mtakatifu; machoni mwa mwanadamu, ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu, walitenda matendo mengi yaliyovuka mipaka ya ubinadamu wa kawaida. Kwa ajili hii mwanadamu aliwachukulia kama Mungu. Sasa ni sharti nyote mlione hili kwa uwazi zaidi, kwani limekuwa jambo ambalo liliwakanganya sana wanadamu wote katika enzi zilizopita. Aidha, kuwa mwili ndicho cha ajabu zaidi kwa vitu vyote, na Mungu katika mwili ni vigumu zaidi kukubaliwa na mwanadamu. Ninachokisema kinasaidia katika kutimiza majukumu yenu na kuelewa muujiza wa kupata mwili. Haya yote yanahusiana na usimamizi wa Mungu, kwa maono. Ufahamu wenu wa hili jambo utakuwa wa faida zaidi kwa kupata ufahamu wa ono, yaani kazi ya usimamizi. Kwa njia hii, mtafahamu zaidi pia wajibu ambao wanadamu mbalimbali wanafaa kutimiza. Japo maneno haya hayawaonyeshi njia moja kwa moja, bado ni msaada mkubwa kwa kuingia kwenu, kwa kuwa maisha yenu ya sasa yamepungukiwa sana na maono na hili litakuwa kikwazo kikubwa kwa kuingia kwenu. Kama hamjaweza kuyafahamu masuala haya, basi hakutakuwa na motisha ya kuuchochea kuingia kwenu. Na ni vipi kazi kama hii yaweza kuwawezesha kutimiza wajibu wenu vyema zaidi?

Tanbihi:

a. Matini asili iliondoa “kama Yeye ni Mungu.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp