Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 99
Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Mnalichukia kwa kweli? Mbona Nimewauliza mara nyingi? Mbona Nimewauliza swali hili, mara tena na tena? Kuna picha gani ya joka kuu jekundu katika mioyo yenu? Picha hiyo kwa kweli imeondolewa? Hamchukulii kwa kweli kama baba yenu? Watu wote wanafaa kuona nia Yangu katika maswali Yangu. Sio kuwafanya watu wawe na hasira, au kuchochea uasi kati ya mwanadamu, au ili mwanadamu agundue njia yake mwenyewe, bali ni kuwawezesha watu wote wajifungue kutoka kwa minyororo ya lile joka kuu jekundu. Ila mtu yeyote asiwe na wasiwasi. Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu. Hivyo inaweza kuonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaziangalia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!
Kipindi cha hukumu kitakapofika kilele, Sitaharakisha kumaliza kazi Yangu, bali Nitajumuisha ndani ushahidi wa enzi ya kuadibu na kuruhusu ushahidi huo kuonekana na watu Wangu wote; na katika haya kutazaliwa matunda mengi zaidi. Ushahidi huu ndio njia ambayo kwayo Naliadibu lile joka kuu jekundu, na Nitafanya watu Wangu kuliona kwa macho yao ili wajue zaidi kuhusu tabia Yangu. Wakati watu Wangu wananifurahia ni wakati joka kuu jekundu linaadibiwa. Kuwafanya watu wa joka kubwa jekundu kusimama na kuliasi joka ndiyo nia Yangu, na ndiyo njia ambayo Ninawakamilisha watu Wangu, na ni nafasi nzuri ya watu Wangu wote kukua maishani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata...
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi...
Katika dhana za mwanadamu za kitamaduni, upendo wa Mungu ni neema Yake, fadhili, na huruma kwa udhaifu wa mwanadamu. Ingawa mambo haya pia...
Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia...