Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 598
Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Leo, kazi Nifanyayo ndani yenu inakusudiwa kuwaongoza hadi katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; ni kazi ya kukaribisha enzi mpya na ya kuwaongoza wanadamu katika maisha ya enzi mpya. Kazi hii inatekelezwa na kukuzwa miongoni mwenu hatua kwa hatua na moja kwa moja: Nawafunza ana kwa ana; Nawaongoza moja kwa moja; Nawaambia chochote msichokielewa, Nawapa chochote msicho nacho. Inaweza kusemekana kwamba, kwenu, hii kazi yote ni kwa ajili ya ruzuku yenu ya maisha, kuwaongoza pia katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; inakusudiwa hasa kuruzuku maisha ya kundi hili la watu wakati wa siku za mwisho. Kwangu Mimi, hii kazi yote inakusudiwa kukamilisha enzi ya kale na kukaribisha enzi mpya; kumhusu Shetani, Nilipata mwili hasa ili nimshinde. Kazi Nifanyayo miongoni mwenu sasa ni ruzuku yenu ya leo na wokovu wenu wa wakati mzuri, lakini katika miaka hii michache mifupi, Nitawaambia ukweli wote, njia nzima ya maisha, na hata kazi ya siku zijazo; hili litatosha kuwawezesha mpitie mambo kwa njia ya kawaida katika siku zijazo. Nimewaaminia maneno Yangu yote pekee. Sitoi ushawishi mwingine wowote; leo, maneno yote Ninayowazungumzia ni ushawishi Wangu kwenu, kwa sababu leo hamjapitia maneno mengi Ninenayo, na hamwelewi maana yake ya ndani. Siku moja, uzoefu wenu utatimika jinsi tu Nilivyosema leo. Maneno haya ni maono yenu ya leo, na ndiyo mtakayotegemea katika siku zijazo; ni ruzuku ya maisha leo na ushawishi wa siku zijazo, na hakuna ushawishi unaoweza kuwa bora zaidi. Hii ni kwa sababu muda Nilio nao kufanya kazi duniani si mrefu kama muda mlio nao kupitia maneno Yangu; Namaliza kazi Yangu tu, wakati ninyi mnafuatilia maisha, mchakato unaohusisha safari ndefu katika maisha. Ni baada tu ya kupitia mambo mengi ndipo mtaweza kupata njia ya maisha kikamilifu; ni hapo tu ndipo mtaweza kubaini maana ya ndani ya maneno Nizungumzayo leo. Mtakapokuwa na maneno Yangu mikononi mwenu, wakati kila mmoja wenu amepokea maagizo Yangu yote, punde Nitakapowaagizia yote Nipasayo, na wakati kazi ya maneno Yangu imemalizika, basi utekelezaji wa mapenzi ya Mungu pia utakuwa umetimizwa, bila kujali jinsi matokeo makubwa yamefanikishwa. Siyo jinsi unavyodhani, kwamba ni lazima ubadilishwe hadi kiwango fulani; Mungu hatendi kulingana na fikira zako.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya...
Kadiri watu wanavyokubali maneno ya Mungu zaidi, ndivyo wanavyopata nuru zaidi, na ndivyo wanavyokuwa na njaa na kiu zaidi katika...
Kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu...
Midomo yako ni mikarimu zaidi kuliko njiwa, lakini moyo wako ni mwovu zaidi kuliko yule nyoka wa zamani. Midomo yako ni ya kupendeza hata...