Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 192

Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo muhimu wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimefifia sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya kinyama ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa Amejawa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha chochote. Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama kando na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kabisa kwamba siku moja ambapo Mungu atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atauelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kwa ajili ya ustawi wa binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ili binadamu aweze kuishi vizuri. Ujio wa Mungu umeambatana na majaribu, na Mungu pia Anakuja na uadhama na ghadhabu. Mungu anapomwacha mwanadamu, Atakuwa tayari Amepata utukufu, na Ataondoka Akiwa Amejawa na utukufu mwingi na furaha ya kurudi. Mungu anayefanya kazi duniani Hazingatii mambo moyoni Mwake haijalishi watu wamemkataa kiasi gani. Yeye anafanya tu kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu ulianza maelfu ya miaka iliyopita, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa na ulimwengu wa kibinadamu. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunja kabisa moyo wa Mungu tangu zamani. Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka, kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu amepitia Akiwa katika mwili—Mungu amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka shida za ulimwengu wa wanadamu kikamilifu. Kwa muda mrefu Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akapumzika, Akisubiri Mwana Wake mpendwa arudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu hana wasiwasi, pasipo kuzingatia kabisa kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp