Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 149

Wakati Mungu anapokuwa mwili, Roho Wake anamwingia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake nchini, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo ambalo linazidi maumbile kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawa—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hali hii iliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu Alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii iliweza pia kutekeleza kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kuamua kupumzika siku ya saba; hoja hizi haziko hivi kamwe. Hakusema hivyo, wala Hakupanga hivi. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imepangiwa kuwa hivyo hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia sawa na hiyo. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapatia bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Ndiyo maana Nasema kwamba hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisia; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia nzima sita na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wasio aminifu, kama kuwa na mwili, tabia za kishetani zilizopotoka, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa awali, lakini yalitokana na upotovu wa kishetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mashiko ya Mungu? Mungu naye alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu angepanga awali Shetani hasa ili kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Basi kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwa vipi kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mashiko ya Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mashiko ya Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisia; hayaeleweki wala hayana urazini na hayafanyi kazi! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kukabiliwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atafanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi katika siku za mwisho haikuamuliwa awali kabla ya enzi ya Neema; haikuamuliwa awali katika mpangilio unaofuatana kama huu: Kwanza, fanya tabia ya nje ya binadamu kubadilika; pili, fanya binadamu kupokea kuadibu na majaribio yake; tatu, fanya binadamu kupitia kifo; nne, fanya binadamu kupitia zile nyakati za kumpenda Mungu na kuelezea uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, fanya binadamu kuyaona mapenzi ya Mungu na kujua Mungu kabisa, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kupanga mambo haya katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na hii ndiyo kanuni sawa inayofanya kazi na iliyotumika kwenye siku za kale baada ya ulimwengu kuumbwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp