Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 57

Kama Moyo wa Mwanadamu Una Uadui na Mungu, Mwanadamu Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu?

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, sembuse kiini cha asili yao, na mtazamo wao kwa Mungu? Wanamcha Mungu? Wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza kujumuishwa tu kwa maneno matatu: “adui wa Mungu.” Mara nyingi ninyi husema maneno haya matatu, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “ni adui wa Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona mwanadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, watu wanapoanza kumwamini Mungu, ni yupi kati yao asiyekuwa na nia, motisha na tabia yake binafsi ya makuu? Ingawa sehemu moja yao inaamini uwepo wa Mungu, na imeona uwepo wa Mungu, imani yao katika Mungu bado ina hiyo motisha, na nia yao kuu ya kumwamini Mungu ni kupokea baraka Zake na vitu wanavyotaka. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wao hufikiria, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipa nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteseka sana—je, Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je, Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na yeye hutoa madai yake kwa Mungu yanayoonyesha motisha yake, malengo na mawazo ya mabadilishano. Hii ni kusema, ndani ya moyo wake mwanadamu siku zote humweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, akijitetea kwa Mungu kila wakati kwa sababu ya mwisho wake binafsi na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribu yanawapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu lake la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha mwanadamu kiko wazi. Kiini hiki ni kipi? Ni kwamba moyo wa mwanadamu ni mwovu, unaficha udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki na kile kilicho chanya, nao ni wenye kustahili dharau na ulafi. Moyo wa mwanadamu umemfungia Mungu nje sana, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu. Haijalishi jinsi gharama ambayo Mungu amelipia ilivyo kubwa, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa mwanadamu, mwanadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali kuyahusu. Mwanadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kuujali moyo wake yeye mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—sababu ikiwa kwamba mwanadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo hali ya mwanadamu ilivyo leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, je, alifanya mabadilishano na Mungu? Je, alikuwa na nia zozote fiche katika kushikilia njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho unaokuja? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kunazo tofauti nyingi sana; wamo katika viwango tofauti. Ingawa Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa amempa Mungu moyo wake na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kufanya mabadilishano na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya kupita kiasi au madai kwa Mungu; badala yake, aliamini kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Hiki ndicho alikuwa ameona na kupata kutokana na kushikilia njia ya kumcha Mungu kwa uaminifu na kujiepusha na maovu katika miaka yake mingi ya maisha. Vivyo hivyo, alikuwa pia amepata matokeo yanayowakilishwa katika maneno: “Nasi tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mtazamo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alitumia kushinda wakati wa vishawishi vya Shetani, na ndizo zilikuwa msingi wa kusimama kwake imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, je, bado mnamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je, mnatumaini kuwa mtu kama huyo? Je, mnaogopa kupitia vishawishi vya Shetani? Je, mnaamua kumwomba Mungu ili aweze kuwapitisha katika majaribu kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuombea mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yenu ni ndogo kiasi cha kusikitisha; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yenu haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui wa Mungu, hamumchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na hamwezi kuyashinda mashambulio, mashtaka, na vishawishi vya Shetani. Ni nini kinachowafanya mstahili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kumwokoa mwanadamu na maana ya wokovu wa mwanadamu, je, sasa mna imani ya kukubali majaribu sawa na ya Ayubu? Je, hampaswi kuwa na kusudio kidogo mjiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp